Rais Magufuli waite wapinzani wako ujue wanachotaka

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,336
21,435
Tangu Rais ameingia madarakani, ameshakutana na kada za watu tofauti na ameongea nao isipokuwa kwa upande wa wanasiasa bado.

Najua si lazima lakini kibusara kidogo angewaita akasikia maoni yao, nafikiri wana fikra nzuri tu ya kuisogeza nchi mbele ila wanapata hasira unapowapuuza. Labda tatizo vyombo vya habari vimekuwa ni wapinzani kuliko wapinzani wenyewe.

Mpaka sasa mazuri mengi umefanya ila kubwa ni hilo, kama ulivyokwishasema wewe ni Rais wa vyama vyote, basi waite hawa mabwana sidhani kama watakataa wito.
 
Magu anatumia nguvu nyingi kuua upinzani ana wachukulia ka maadui wakati mwanzo alijitanabaisha kuwa ni mpenda maskini lakini hataki kusikiliza maoni yao sasa sijui anatetea wanyonge gani. Kamwe hawezi kuwaita mana yeye ni jeuri kila kitu anakijua yeye. Na asahau ili aongoze vzuri anahtaji support ya wote upinzani na magroup yote hata mwaka Jana isingekuwa figisu figisu maji yalishazidi unga sasa sijui kwanini hafikirii hilo swala. Huko mbeleni yatazidi kumshinda tu asipobadilika
 
Kuwaridhisha wapinzani! Hakuna nchi yeyote imefanikiwa duniani katika hilo,labda awaachie kile kiti.....
Kumbuka huwezi kujua matatizo yako isipokuwa aliekua pembeni yako unaweza kuvaa nguo imechafuka wewe ukaona safi mwingine akakushitua nguo uliovaa ni chafu
 
Hakuna zuri ktk Upinzani maadamu fisadi Lowasa ndiyo nguzo yao, huyu Lowasa ameifilisi hii na sehmu kubwa ya matatizo ya nchi hii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na watu wa kaliba ya Lowasa, hivyo maadamu Lowasa &Co. ndiyo upinzani hakuna zuri ktk upande huwo!
Mkuu tusimuangalie mtu,ila awaite wapinzani,mpaka sasa nao kuna michango yao inahitajika kwake
 
Awaite watu waliosema hawamtambui kama Rais wa JMT?
Barbosa hivi sasa ukisikia hotuba nyingi bungeni zilizowasilishwa si unasikia wanataja neno rais,kama mtu mmoja hamtambui haijalishi kundi kubwa linamtambua
 
Tangu raisi ameingia madarakani,ameshakutana na kada za watu tofauti na ameongea nao isipokuwa kwa upande wa wanasiasa bado,najua si lazima lakini kibusara kidogo angewaita akasikia maoni yao,nafikiri wanafikira nzuri tu ya kuisogeza nchi mbele ila wanapata hasira unapowapuuza,labda tatizo vyombo vya habari vimekuwa ni wapinzani kuliko wapinzani wenyewe,mpaka sasa mazuri mengi umefanya ila kubwa ni hilo,kama ulivyokwisha sema wewe ni raisi wa vyama vyote basi waite hawa mabwana sidhani kama watakataa wito.
hapo angekuwepo zee la musoma tysoni lingesema wanataka kwenda kunywa juice, sahivi sijui juice linainwa wapi
 
Kiburi, Jeuri yana matokeo mabaya.. mungu aliposema "na tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu..." hakuwa na maana na sisi tutakuwa na maamuzi ya kimungu. Magu ni Philosophy Doctor ila anahitaji Psychology Doctor kutibu attitude zake.
 
Wakanye chai???

Mbona kila kitu kinajulikana!!
i) kunywa chai ikulu,
ii) asitumbue mafisadi,
iii) kumwachia babu seya gerezani,
iv) kumleta Balali kuzimu.

Sasa atakaa nao wapi. Kama wanataka wajisalimishe kama wenzao. Mbona Maalim Seif alienda?
Tangu raisi ameingia madarakani,ameshakutana na kada za watu tofauti na ameongea nao isipokuwa kwa upande wa wanasiasa bado,najua si lazima lakini kibusara kidogo angewaita akasikia maoni yao,nafikiri wanafikira nzuri tu ya kuisogeza nchi mbele ila wanapata hasira unapowapuuza,labda tatizo vyombo vya habari vimekuwa ni wapinzani kuliko wapinzani wenyewe,mpaka sasa mazuri mengi umefanya ila kubwa ni hilo,kama ulivyokwisha sema wewe ni raisi wa vyama vyote basi waite hawa mabwana sidhani kama watakataa wito.
 
Mpaka leo hii Lowasa hamtambui Raisi wa JMTZ na kila siku anakumbushia hilo na sijawahi kusikia hata siku moja chadema au Uongozi wa chdema ukimsahihisha au kukana anachosema hivyo ina maana chadema kama chama na ukawa kwa ujumla hawamtambui Raisi wa JMTZ, sasa kabla ya wao kuanza kulalama wafanye home work yao kwanza...
Mkuu ndio maana nigusia vyombo vya habari hivi sasa vimekuwa upinzani kuliko upinzani wenyewe,mikutano yake imepigwa marufuku na hakufanya ina maana si anajua nchi ina mtawala amekubali kimya kimya
 
Hatuna mda wa kucheka na nyani kwa sasa ni kazi tu mkitaka na nyinyi mfanye kazi na sio majungu. Magu usiachie uliposhikilia.
 
Mkuu tusimuangalie mtu,ila awaite wapinzani,mpaka sasa nao kuna michango yao inahitajika kwake
Mkuu nadhani mtoa hoja kasema vyema. Wapinzani ni wananchi wa nchi hii nao wanatakiwa kusikilizwa na mkuu wa nchi.

Lakini sasa tatizo ni kwamba wanagomea kushiriki vikao vya bunge ambapo ndipo penye forum ya kusemea. Hawakutoa maoni yao kwenye hotuba ya PM, hawataki kushiriki chini ya Naibu Spika.

Sasa Rais awaite ili aongee nao kuhusu kumkubali Naibu Spika? Au awaite ili akubaliane nao kumkataa Naibu Spika?

Wao wamalize mambo yao ndani ya chombo chao kisha washiriki vikao na kutoa hoja hapo hata Mkuu wa Nchi anaweza kusema sasa niwaite tukae pamoja tunywe kahawa na sharubati tukiongelea mambo ya nchi kama wanasiasa.
 
Upinzani wanazingua walikuwa wapi mda wote kwanza nao ni mafisadi wasubilie kutunbuliwa
 
Back
Top Bottom