Maoni ya mdau kutokana na hotuba ya Rais Magufuli juu ya Corona

omganya

Member
Feb 1, 2019
18
41
Habari ndugu?

Jana Rais wetu mpendwa ameongea na watanzania kupitia vyombo vya habari. Ni wazi watu wengi tulisubiri hotuba ya mkuu wa nchi baada ya malalamiko na maneno mengi ya kumtaka afanye hivyo. Hii ilikuwa ni the waiting speech.

Ni dhahili tulitegemea hotuba hii ituelekeze nini tufanye kama nchi ili kupambana na gharika hii. Rais aligusia mambo kadhaa ambayo yeye aliyaona ni muhimu sana kuyasema .

1. Hakuna haja ya kudaktari Dar (Lock down). Kwa kuwa Dar ndo inaendesha uchumi wa nchi.

Mkanganyiko.
Nafikiri kipaumbele chetu Sasa ni kupambana na covid 19. Kama ugonjwa ukisambaa sana hakuna uchumi utaendelea. Pia tutajikuta tunatumia pesa nyingi sana na kudidimiza uchumi. Mfano kwa nchi za Italia na Uhispania uchumi umeanguka kabisa kutokana na shida hii. Hivyo tupambane na corona ili tuwe na afya kwa afya ya uchumi wetu pia.

2. Ni vema Bank ya dunia ikatupunguzia au kutusamehe madeni badala ya kutukopesha kwani tunatumia takribani billion 7 kwa mwezi kulipa madeni ya taasisi za kimataifa.

Kwa hili raisi kanena vyema sana. Nakupongeza kwa hili. Lkn pia ni vema kutenga mapato ya ndani kupambana na kadhia hii.

3. Wizara ya afya itangaze idadi sahihi ya waliopona. Hadi kufikia jana waliopona kwa mujibu wa wizara ni 11, vifo 5, na maambukizi 284. Lkn Rais anasema ana taarifa waliopona ni zaidi ya 100.

Mkanganyiko.
Hii inathibitisha wazi kuwa serikali haitowi taarifa sahihi. Iweje waziri mkuu na waziri wa afya watoe taarifa tofauti,?? Je hakunana mawasiliano? Je hawaaminiani , na je wanahujumiana?? Maswali ni mengi sana.

4. Kutumia dawa za asili kama kufukiza mvuke make mvuke ni zaidi ya 100, za nyuzi joto. Kwani kwa joto hili huuwa virus kwenye njia ya hewa.

Mkanganyiko.
Hii haijathibitika kitaalam. Pia ni tofauti na ujumbe kutoka kwa naibu waziri ambaye ni mtaalam ya afya Dr Faustine Ndungulile. Pia inaonesha hakuna mawasiliano ya naibu waziri na Rais make ilikuwa ni mda mfupi sana kati ya kauli hizi.

5. Kutoamini barakoa kutoka nje ya nchi. Rais alionesha haamini barakoa kutoka nchi nyine. Ni kweli afya ni usalama na lazima tuwe makini. Lkn.

Mkanganyiko.
So vizuri Rais kutoa matamshi hadharani ya kutoamini baadhi ya nchi. Tanzania inahitaj na tunaomba na kupata misaada kutoka mataifa mbalimbal. Hospital zetu zote za kanda kuna vitengo vinavyoendeshwa na wahisani. Mfano kitengo cha moyo bugando. Kwa namna tatizo lilivyo tunahitaji kushirikiana na wengine.

6. Ushirikiano wa wanasiasa. Jana nimshukuru rais japo kidogo aligusia umuhimu wanasiasa kuungana.

Mkanganyiko.
Nilitegemea rais aseme namna nzuri ya kuwashirikisha wanasiasa wote kutoka vyama mbalimbali.

UHAURI. NINI KIFANYIKE.
Covid 19. Ni janga na ni hatari sana duniani kote. Kama nchi zilizoendelea kama Uchina, Italy, Wingereza, Uhispania , Marekani na kwingineko. Wametaabika hivyo ni vema tuchukue hatua kwa kuzingatia udhaifu na madhara yaliyotokea kwa wenzetu

1. Tusitishe usafiri wa ndani kwa abiria kutoka mkoa hadi mkoa. Hii itasaidia kutoeneza ugonjwa mikoani.

2. Tukate bajeti ya wizara nyingine kwa 20% na kuipeleka wizara ya afya ili kusaidia kununua vifaa na kulipia wahudumu kama madaktari, manesi, wafamasia nk.

3. Tutangaze ajira kwa kada ya afya kwa kuajiri wastaafu, waliohitimu ambao hawana ajira, na wanafunzi wa kada za afya waliokwisha soma zaidi ya nusu ya muda wao wa masomo. Hii itasaidia kupunguza uhaba wa wataalam. Kwani nchi nyingi zimeonesha uhaba wa watalam ni changamoto kubwa. Hii inatokana na watalaam wengi kupata maambikizi kutokana na kuwa mstari wa mbele wa mapambano.

4. Kila mtu avae barakoa na gloves kila mahali. Ni dhahiri kuwa hawa virus wanakuwa kwenye mate, makamasi na majimaji mengine ya mwili wa muathirka. Kuvaa barakoa kunapunguza kwa kiwango kikubwa kusambaza au kupokea mate au makamsi.

5. Jkt, magereza na viwanda binafsi vipewe ruzuku kutengeneza barakoa na kuzigawa bure kwa wananchi wote. Hizi zigawiwe kwenye mitaa kwa kuratibiwa na mitaa husika. Hii itasaidia kuweka katazo la mtu yeyote kutoonekana bila barakoa. Pia viwanda vinsvyohusika na dhana ya za kujikinga visamehewe kodi na material yawe imported Free of duty.

6. Tuwezeshe hospital za kanda zote ziweze kupima covid 19. Hili litasaidia kupima na kupata majibu kwa uharaka zaidi. Ikiwezekana na hospital za mikoa.

7. Kila kata ipewe daktari na nesi atakayeratubu na kuchukuwa vipimo kwenye kila kaya kwa watu wenye risk kubwa zaidi ya maambikizi. Ikiwezekana daktari na nesi iwe kwa kila mtaa au kijiji. Na hii ndo maana niliongelea kutangaza ajira kwa kada ya afya na kutata 20% ya bajeti ya wizara nyingine ili kuweza kupata bajeti. Hawa wataalam wapange ratiba ya kutembelea familia kila siku na kukusanya taarifa zitakazopelekwa wilayani, mikoani na taifa.

8. Kuendelea kuhamasisha michango ya hali na mali ili kuimalisha mfuko wa kupambana na covid 19.

9. Kuleta ushirikiano na uhamasishajo kutoka kada zote. Mfano kwenye kamati ya waziri mkuu waongezwe kiongozi wa upinzani bugeni na viongozi wa dini halkadhalka watu wengine maalfu kama wanamziki.

10. Kusitisha mikusanyiko yote kama Ibada zinazojumuisha watu wengi.
 
Mengine ni ngumu kuwezekana. Hasa namba 6 na 7.

Tuma bei ya chini uweze kujishindia simu toka tigo.
 
Kwa jinsi hali ya corona ilivyo kwa afrika halafu huu ugonjwa ungekuwa upo afrika tu basi nadhani corona isingeonekana kama sasa ambavyo inaonekana.
 
omganya,
Huo ni ushauri wako si wa jiwe watanzania mill 55 wanafuata ushauri wa mkuu sahivi kujifukiza tu ujasikia wagonjwa pia wametoroka huko amana wanaenda kujifukiza tu..
 
omganya, Mawazo yako yana mashiko sana,ila bahati mbaya wewe si sehemu ya watu wanaomzunguka Rais, hivyo yatabaki humu tu jamii forums bila kuwasaidia watanzania zaidi ya milioni 50.Wanaomzunguka Rais wetu wako bize kuimba pambio za kumsifu tu Rais na sasa wanaimba nyimbo za kuabudu kabisa e.g RPC wa Arusha kama sijakosea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
omganya, Mkanganyiko.
So vizuri Rais kutoa matamshi hadharani ya kutoamini baadhi ya nchi. Tanzania inahitaj na tunaomba na kupata misaada kutoka mataifa mbalimbal. Hospital zetu zote za kanda kuna vitengo vinavyoendeshwa na wahisani. Mfano kitengo cha moyo bugando. Kwa namna tatizo lilivyo tunahitaji kushirikiana na wengine.

Huko koote umebananga ila hapa ulaamua kuhara kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom