mulwanaka
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 5,262
- 12,835
"Katika kipindi Cha awamu ya tano Mimi pamoja na nyinyi wakati tukitekeleza ilani ya Chama chetu Cha Mapinduzi tulijiwekea mipango yetu na mipango hiyo ilitakiwa itekelezwe katika kipindi Cha miaka mitano, Mipango mingi Sana tumeitekeleza. Tuna mpango wa kuweka umeme katika kila Kijiji nchini, vijiji vilivyopokea umeme wa Rea Ni vijiji 9114 bado vijiji 3000 kila Kijiji lazima kiwe na umeme na huu ni mpango ambao bado hatujaukamilisha."