BOB LUSE
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 3,585
- 2,895
Nchi yetu inakuwa Kwa kasi, Ujenzi wa Makazi, Biashara,Viwanda. zinaongezeka Kila kukicha, Tunashukuru Mungu.Viongozi wetu wanapaswa kwenda na kasi hiyo katika mipango yao.
Miaka michache ya utawala uliopita ilionekana tatizo la Umeme limedhibitiwa. Umeme wetu unatumia vyanzo vya maji, Gesi na mafuta.kuna mipango mizuri na ya uhakika ya kupeleke umeme Kila vijiji. Lakini hakuna mipango thabiti ya kuhuisha vyanzo vyetu vya umeme vya dharura, wakati tunasubiri mradi Makubwa wa maji, ambao pia hatuna uhakika na mvua, miradi ya dharura ingepewa kipaumbele Cha kuzarisha umeme katika kipindi hiki.
Tunajigamba na Madini ya Uranium, tunasafirisha yakazalishe umeme wa Nuklia huko Duniani, wakati sisi hatuna ufumbuzi wa kudumu! Kiongozi ambaye Hana maono Makubwa ya kutufanya tusahau kukatika Kwa umeme hana haja ya kuingizwa tena madarakani.
Usalama wa Taifa, unapaswa kujua mahitaji ya nchi na kuyapa kipaumbele, madalali wa madaraka hawapaswi kupitishwa Ili kuepusha nchi katika hasara zisizo za lazima.nguvu kubwa zinazozibiti wapinzani wasitawale, zitumike kuzuia Viongozi wa hovyo wasipitishwe na kikundi kidogo Cha watu wanaoamua mustakhabali wetu.
Umeme wa maji/ dharura sio ufumbuzi wa kudumu wa chanzo chetu Cha nishati. Tujifunze Kwa nchi zilizofanikiwa katika Hilo, nafuu tukope Ili kuimarisha eneo hilo Kuliko kujenga madarasa na matundu ya vyoo, yaliyo ndani ya uwezo wetu.
Mungu ibariki nchi yetu.