G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Rais Magufuli sidhani kama unatamani mafuta ya waganda yachimbwe kuliko waganda wenyewe! Hivi nikuulize swali? Wale wenye mitambo ya kuchenjulia makinikia kule Japan ambapo umezuia makontena kwenda huko wakaja hapa nchini kisha wakahubiri weee na wakamalizia kwa kusema "Mfukuze huyo mkuu wa bandari kwa kuwa anatukwamisha kwa kuzuia hayo makinikia kuchenjuliwa, You have to lose "Litre" and gain more" Utakubali? Utakubali kuwa wenye smelter waseme kuwa mkuu wa bandari anakukwamisha hivyo mfukuze kazi?
Narudia tena, sidhani kama hayo mafuta ya waganda una uchungu nayo kuliko waganda wenyewe. Wewe unataka waganda waingie hasara kwa vile tu bomba linalopitisha hayo mafuta halina hasara yoyote kwani utalipwa kwa pipa linalopita pale? Wao wapate hasara ili waharakishe wewe uingize hela kwenye bomba na mambo ya ulinzi?
Ukiona kamishina wa mapato wa Uganda amekataa hilo ujue anaona kabisa hakuna maslahi, yeye siyo mjinga hadi akatae nchi yake kuchimbwa mafuta! Ukiona naye Museven kakaa kimya pia siyo mjinga! Kuna vingi anaangalia. Hawawezi kujiingiza mkenge ili kumnufaisha Magufuli kisiasa!
Haya uliyohubiri juzi kwakweli ni Ubeberu asilimia 100. Naamini sasa Waganda wamekuelewa na wameelewa kwanini unatumia nguvu kubwa sana kunyamazisha wanaoelewa na kisha kukosoa.
Nimeshangazwa sana, Rais wa nchi tena jirani unahubiri waziwazi kuifanya nchi jirani yako kuingia mkenge wakati huku kwako unazuia tena kila siku kuwalaumu watangulizi wako kwa kuingia mkenge? Tafadhali sana mheshimiwa Rais usionyeshe waziwazi kuwa umejiwekea ubinafsi sehemu fulani ya mwili wako. Kwa kasi hii angalia sana Kagame asije kuku....Maana kwa jinsi anavyojikomba atakuwa ameshakuelewa.
Halafu kusema vile mbele ya mkuu mwenzako wa nchi wala haijakaa poa kabisa kabisa.