Rais Magufuli tunakuomba umwache Katibu Mkuu Dr. Turuka Wizara ya Kilimo

nyamagaro

JF-Expert Member
Feb 25, 2010
394
225
Kwako Mh. Dr John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Kwanza nakupongeza kwa mema unayoyafanya. Hivi karibuni umefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa na kufanya mabadiliko ya Makatibu Wakuu wa Wizara mabalimbali. Moja ya wizara zilizopata mabadiliko ni wizara kilimo. Kwenye Mabadiliko hayo Mh. Rais umembadilisha Dr Florens Turuka kwenda Wizara ya Ulinzi na kumleta Mhandisi Mathew Mtigumwe wizara ya Kilimo. Kwa heshima kubwa nakusihi umwache Dr Turuka hapa kilimo kwa sababu zifuatazo:

1. Huyu mtu anaifahamu sana hii secta na tangia afike hapa wizarani utendaji wake umeonekana kwa kuunganisha wafanyakazi tofauti na watangulizi wake wengi.

2. Dr Turuka ni mtu mchapakazi, muadilifu na mnyenyekevu. Kama mtendaji wa wizara ameweza kusimamia mambo ambayo yalikuwa hayaendi sawasawa.

3. Panapomstathili ni hapa wizara ya kilimo kwa sababu kitaaluma Dr Turuka ni Mchumi kwenye masuala ya kilimo (Agricultural Economist). Sisi kama watumishi tulioko chini yake tumemuona kama mtu mwenye ueledi na kazi yake, hana majungu, anaelekeza na kuonyesha uongozi.

Mwisho nitoe ushauri kuwa Mh. Rais hii wizara inahitaji taaluma, uzoefu na umahiri wa kazi wa hali juu kama alivyo Dr. Turuka. Hii wizara haiitaji mtawala bali kiongozi. Hivyo nakusihi kwa heshima nyingi umuongezee angalau miaka miwili Dr. ili yale mema aliyoanzisha aweze kuyasimamia na kukamilisha.

Nawasilisha
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,857
2,000

Hakuna mwenye hati miliki ya wizara fulani.Kwani hakuandaa wachapa kazi wengine kama yeye alipokuwa hapo wizarani?
 
BAFA

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
3,070
2,000
Hakuna mwenye hati miliki ya wizara fulani.Kwani hakuandaa wachapa kazi wengine kama yeye alipokuwa hapo wizarani?
Nadhani sio hatimiliki mtoa mada yupo kilimo na amekuja na hoja nzuri ya kuwa katibu ni mtaalam hasa mambo ya kilimo na alifanya mazuri wakati yuko wizarani which is good
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,857
2,000
Nadhani sio hatimiliki mtoa mada yupo kilimo na amekuja na hoja nzuri ya kuwa katibu ni mtaalam hasa mambo ya kilimo na alifanya mazuri wakati yuko wizarani which is good
Kufanya mazuri mahali sio cheo cha kifalme kuwa lazima mtu afie hapo. Hata wizara ya ulinzi kuna kilimo JKT wako chini yake utaalamu wake waweza takiwa huko pia KUFANYA mapinduzi ya kilimo JKT.hUKO AENDAKO kilimo pia kipo.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,782

Weka ukada na ushabiki pembeni kisha tumia common sense. Kama alivyosema mleta mada (nami nathibitisha kv namfahamu), Dr. Turuka ni Agricultural Economist na mimi binafsi ni mwalimu wangu wa Microeconomics. Dr. Turuka amefanya researches nyingi sana za field yake kiasi kwamba enzi hizo wakati tunasoma alikuwa hadi anaboa kwavile alikuwaga busy zaidi na researches kuliko kuingia darasani kufundisha!

On the other hand, Katibu Mkuu wa Wizara ndie Mtendaji Mkuu wa Wizara... kwamba, ni mtu anayetakiwa kufahamu shughuli za wizara husika nje ndani. Now tell me, hivi kwa kutumia tu akili ya kawaida; ni nani ana-fit Wizara ya Kilimo kati ya Agricultural Economist tena mwenye back ground ya general agriculture na mtu ambae taaluma yake ni Uhandisi?

Kwahiyo issue sio ufalme au kitu chochote kama hicho, bali ni nani ange-fit kwenye wizara hiyo muhimu kati Engineer na Agricultural Economist!
 
Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,310
2,000
Kwani Huyu Mathew Mtigumwe ni Engineer wa kitu gani hasa? ali-specialize kwenye kitu gani?

Huyu Dr. Florence Turuka umesema Rais amuongezee miaka miwili? kwani anakaribia kustaafu au amuongezee kwa kumrudisha hapo Kilimo?

Basi, kama wafanyakazi mnampenda kwa mazuri anayoyafanya ni busara tu ya kawaida arudishwe hapo Kilimo sasa, lakini ni lazima izingatiwe sababu za Rais kumhamisha ni zipi!!
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,857
2,000
Kwahiyo issue sio ufalme au kitu chochote kama hicho, bali ni nani ange-fit kwenye wizara hiyo muhimu kati Engineer na Agricultural Economist!

Inategemea kama unataka kilimo cha kisasa cha kulisha viwanda hutaki cha jembe la mkono unataka kufanya mechanization kwenye kilimo mtaalamu unayemhitaji ni engineer sio economist sababu kazi kubwa itahusika kwenye mechanization na sio kwenye kuangalia mambo ya demand and supply.

Lengo la serikali ni kuingia uchumi wa viwanda .Kuingia uchumi huo lazima mabadiliko makubwa kwenye kilimo hasa upande mechanization.Mambo hayo yanahitaji engineer zaidi.Kwa mlengo uliopo wa viwanda engineer wizara ya kilimo ni sahihi zaidi kwani tunaelekea kwenye viwanda vya maziwa vitakavyohitaji mitambo zaidi kuanzia ya kilimo,ufugaji,nk ili kupata mali ghafi za kutosha kulisha viwanda
 
Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,392
2,000
Nadhani sio hatimiliki mtoa mada yupo kilimo na amekuja na hoja nzuri ya kuwa katibu ni mtaalam hasa mambo ya kilimo na alifanya mazuri wakati yuko wizarani which is good

Kweli, FT ni mtu makini toka ujana. Ametumia taaluma yake kikamilifu. Hiyo wizara aliwahi pewa Prof Machunda toka SUA (mtaalamu kilimo) ikamshinda. Natumaini kwa kuwa tunaenda uchumi wa viwanda, Mhandisi anafaa. Pia kuisimamia sekta ya Irrigation MM atatufaa kwani ni mambo ya ujenzi wa miundombinu na usimamizi wa tenda zaidi. Yamkini tuna tatizo kubwa la procurement and its supervision in big projects..
 
Happy nation

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
679
1,000
Lazima abadilishwe,kumekuwa na matatizo ya Ruzuku mpya wamepewa makampuni hela nyingi bila ya kueleza wizara watauza bei gani vijijini,kuna mbegu huku bila ya ruzuku inauzwa 9000 na kuna yenye ruzuku inauzwa 10000,kwa habari zilizoko ni kwamba makampuni hayajaomba kwa kueleza ni shilingi ngapi watauza vijijini ili wizara ione ni ipi ni nafuu kwa mkulima,waliopewa asilimia 30 bado wanauza sh 10000 kwa kilo 2.ufisadi ni mkubwa sana wizara hii.
 
Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,131
2,000
Kuna agriculture engineers. Labda huyo ni Agricultural Engineer. Anaweza kuwa better than agricultural Economist kama kweli tunataka kilimo cha kisasa hususani cha umwagilizaji, usiotumia jembe la mkono, wenye viwanda vya mazao ya kilimo na kadhalika.
 
mugosha

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
766
500
Kwako Mh. Dr John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Kwanza nakupongeza kwa mema unayoyafanya. Hivi karibuni umefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa na kufanya mabadiliko ya Makatibu Wakuu wa Wizara mabalimbali. Moja ya wizara zilizopata mabadiliko ni wizara kilimo. Kwenye Mabadiliko hayo Mh. Rais umembadilisha Dr Florens Turuka kwenda Wizara ya Ulinzi na kumleta Mhandisi Mathew Mtigumwe wizara ya Kilimo. Kwa heshima kubwa nakusihi umwache Dr Turuka hapa kilimo kwa sababu zifuatazo:

1. Huyu mtu anaifahamu sana hii secta na tangia afike hapa wizarani utendaji wake umeonekana kwa kuunganisha wafanyakazi tofauti na watangulizi wake wengi.

2. Dr Turuka ni mtu mchapakazi, muadilifu na mnyenyekevu. Kama mtendaji wa wizara ameweza kusimamia mambo ambayo yalikuwa hayaendi sawasawa.

3. Panapomstathili ni hapa wizara ya kilimo kwa sababu kitaaluma Dr Turuka ni Mchumi kwenye masuala ya kilimo (Agricultural Economist). Sisi kama watumishi tulioko chini yake tumemuona kama mtu mwenye ueledi na kazi yake, hana majungu, anaelekeza na kuonyesha uongozi.

Mwisho nitoe ushauri kuwa Mh. Rais hii wizara inahitaji taaluma, uzoefu na umahiri wa kazi wa hali juu kama alivyo Dr. Turuka. Hii wizara haiitaji mtawala bali kiongozi. Hivyo nakusihi kwa heshima nyingi umuongezee angalau miaka miwili Dr. ili yale mema aliyoanzisha aweze kuyasimamia na kukamilisha.

Nawasilisha
Mtoa hoja ulitakiwa ulete ushauri ambao unaweza kufanyiwa kazi in future au kama ungekuwa umebahatika kunusa mabadiliko haya kabla hayajatekelezwa hii hoja yako ingeweza kuwa na mashiko lakini kwa sasa hakuna namna. Nadhani wizara ina watu wengi mahiri ambao watasaidiana na Eng. kufanya mambo yaende.
 
mugosha

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
766
500
Kuna agriculture engineers. Labda huyo ni Agricultural Engineer. Anaweza kuwa better than agricultural Economist kama kweli tunataka kilimo cha kisasa hususani cha umwagilizaji, usiotumia jembe la mkono, wenye viwanda vya mazao ya kilimo na kadhalika.
Engineer ni Engineer tu, akiwa CE, EE, ME, CPE, AE, nk nk. Jamaa wanaweza kufanya kazi yoyote na ikibidi hata kwa kutumia msuli. Engs ni mabingwa wa kutumia vizuri watu walio chini yao, na kama wizara inao wakurugenzi competent lazima mambo yataenda tena vizuri zaidi ILA baadhi ya Eng. hawataki blaa blaa, wanataka kuona kitu kwa macho. Kilimo kazi mnayo.
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,425
2,000
Kwako Mh. Dr John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Kwanza nakupongeza kwa mema unayoyafanya. Hivi karibuni umefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa na kufanya mabadiliko ya Makatibu Wakuu wa Wizara mabalimbali. Moja ya wizara zilizopata mabadiliko ni wizara kilimo. Kwenye Mabadiliko hayo Mh. Rais umembadilisha Dr Florens Turuka kwenda Wizara ya Ulinzi na kumleta Mhandisi Mathew Mtigumwe wizara ya Kilimo. Kwa heshima kubwa nakusihi umwache Dr Turuka hapa kilimo kwa sababu zifuatazo:

1. Huyu mtu anaifahamu sana hii secta na tangia afike hapa wizarani utendaji wake umeonekana kwa kuunganisha wafanyakazi tofauti na watangulizi wake wengi.

2. Dr Turuka ni mtu mchapakazi, muadilifu na mnyenyekevu. Kama mtendaji wa wizara ameweza kusimamia mambo ambayo yalikuwa hayaendi sawasawa.

3. Panapomstathili ni hapa wizara ya kilimo kwa sababu kitaaluma Dr Turuka ni Mchumi kwenye masuala ya kilimo (Agricultural Economist). Sisi kama watumishi tulioko chini yake tumemuona kama mtu mwenye ueledi na kazi yake, hana majungu, anaelekeza na kuonyesha uongozi.

Mwisho nitoe ushauri kuwa Mh. Rais hii wizara inahitaji taaluma, uzoefu na umahiri wa kazi wa hali juu kama alivyo Dr. Turuka. Hii wizara haiitaji mtawala bali kiongozi. Hivyo nakusihi kwa heshima nyingi umuongezee angalau miaka miwili Dr. ili yale mema aliyoanzisha aweze kuyasimamia na kukamilisha.

Nawasilisha
Huyo Turuka amekuwa mchapakazi baada ya kufika Kilimo? Huku kwingine alikopitia mbona hatukuona lolote? Hayo mambo ya kujifaragua kwa kuwa kaona kuna hatari inamfuta, ni adrenaline tu, lakini hakuna alikoonyesha historia ya utendaji mzuri. Ngoja tuchunguze, asijekuwa ni wale walioshikwa mkono kuingia kwenye nafasi na sasa anatetewa kwa kuchapakazi.

Kwa upande wangu ningemuomba rais ampumzishe tu maana sitegemei mtu aliyelemazwa kwa utawala uliopita, leo hii baada ya mwaka mmoja ageuke kuwa mchapakazi.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,782
2,000
Inategemea kama unataka kilimo cha kisasa cha kulisha viwanda hutaki cha jembe la mkono unataka kufanya mechanization kwenye kilimo mtaalamu unayemhitaji ni engineer sio economist sababu kazi kubwa itahusika kwenye mechanization na sio kwenye kuangalia mambo ya demand and supply.

Lengo la serikali ni kuingia uchumi wa viwanda .Kuingia uchumi huo lazima mabadiliko makubwa kwenye kilimo hasa upande mechanization.Mambo hayo yanahitaji engineer zaidi.Kwa mlengo uliopo wa viwanda engineer wizara ya kilimo ni sahihi zaidi kwani tunaelekea kwenye viwanda vya maziwa vitakavyohitaji mitambo zaidi kuanzia ya kilimo,ufugaji,nk ili kupata mali ghafi za kutosha kulisha viwanda
Maelezo yako yanaonesha uelewa mdogo wa sekta ya kilimo! Kwanza kabisa, Matthew Mtigumwe ni Civil Engineer... sasa Civil Engineer na agricultural mechanization wapi na wapi??!! Anyway, labda penye shida they can serve as a square peg in a round hole... lakini kama issue ni mechanization kwenye kilimo kwanini hakuteua Agricultural Engineers moja kwa moja?! Or at least Irrigation Engineers?!!

Kwahiyo hoja ya mechanization kwenye kilimo si tu kwamba ni assumptions bali pia haina nguvu manake kama hilo lingekuwa ndo lengo lake basi angeteua wabobezi kwenye eneo husika!!!

That's one but two unaposema kama tunataka kulisha viwanda anayetakiwa ni engineer na sio agricultural economist unaonesha wazi kwamba hufahamu roles za hawa watu wawili! Kimsingi Agricultural Economist ni Farm Manager... ni agricultural commercial manager! Yeye ndie mwenye wajibu wa kufahamu best inputs combination for commercial prodution...!!! Engineer na taaluma yake anaweza kuja na kusema, kutokana na ugumu wa udongo wa hapa with limited time iliyopo; hapa tunabidi kupitisha trekta... wala hajali cost ya ku-run hilo trekta; wala hataangalia tukishaapitisha trekta je output ita-cover costs na wala hafahamu hicho kitakacholimwa hapa at that unknown cost kitauzwa wapi... hana sababu ya kufahamu kwa sababu sio kazi na wala taaluma yake! Lakini huyo agricultural economist unayesema hahitajiki kwenye kilimo cha viwanda, taaluma yake inamfundisha anatakiwa ku-evaluate vyote hivyo ambavyo usishangae akatoa conclusion kwamba hapa itumike labor intensive instead of machine intensive kwa sababu ameshaona akitumia machine intensive itazalisha expensive outputs ambazo zitakuwa less competitive in the market na hivyo kuwafanya hao wenye viwanda uliowalenga waaamua ku-import bidhaa ile ile ambayo na wewe unazalisha!!!
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,782
2,000
Kuna agriculture engineers. Labda huyo ni Agricultural Engineer. Anaweza kuwa better than agricultural Economist kama kweli tunataka kilimo cha kisasa hususani cha umwagilizaji, usiotumia jembe la mkono, wenye viwanda vya mazao ya kilimo na kadhalika.
Katibu Mkuu ni Mtendaji/Meneja kwahiyo Agricultural Economist ndie ana-fit zaidi kwa sababu huyu anaandaliwa kuwa commecial manager. Hawa Engineers wana-fit zaidi as Wakurugenzi wa idara mbalimbali kama vile idara ya umwagiliaji for Irrigation Engineers, idara ya mechanization for Agricultural Engineers n.k. Sasa Katibu Mkuu ndo anatakiwa kufahamu best combination ya hizo idara... hizo ndo kazi za wachumi.

But all in all, Matthew ni Civil Engineer na sio Agricultural Engineer
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,857
2,000
Maelezo yako yanaonesha uelewa mdogo wa sekta ya kilimo! Kwanza kabisa, Matthew Mtigumwe ni Civil Engineer... sasa Civil Engineer na agricultural mechanization wapi na wapi??!!
ANYWAY hii vita nimeanza kuielewa kuna kamkoa fulani kakikaa mahali kanajijengea kaufalme wa milele.Wanufaika naona mmeanza kelele

Civil engineer ana uwezo mkubwa kuanzia ujenzi wa miundo mbinu ya umwagiliaji kwa ajili ya kilimo,ujenzi wa mabwawa ya ufugaji wa sammaki,ujenzi wa mabanda ya kuku,nguruwe,ngombe nk,civil engineer ni mjenzi wa maghala ya kuhifadhi vyakula,ujenzi wa miundo mbinu ya kilimo ya mashamba makubwa (estates) huangua chini yake,Huwezi kuongelea ujenzi wa miundo mbinu yoyote ya kilimo,mifugo au maji bila kumweka civil engineer.
 
Joto Balaa

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,142
2,000
Kuna agriculture engineers. Labda huyo ni Agricultural Engineer. Anaweza kuwa better than agricultural Economist kama kweli tunataka kilimo cha kisasa hususani cha umwagilizaji, usiotumia jembe la mkono, wenye viwanda vya mazao ya kilimo na kadhalika.
Ndo tatizo la wengi wetu humu JF hatufuatilii mambo vizuri. Kabla ya kuwa RC Singida Mhandisi Mtigumwe alikuwa Regional Manager wa Tanroads Ruvuma. Sasa huo uhandisi wa Kilimo kautoa wapi mkuu.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,782
2,000
ANYWAY hii vita nimeanza kuielewa kuna kamkoa fulani kakikaa mahali kanajijengea kaufalme wa milele.Wanufaika naona mmeanza kelele

Civil engineer ana uwezo mkubwa kuanzia ujenzi wa miundo mbinu ya umwagiliaji kwa ajili ya kilimo,ujenzi wa mabwawa ya ufugaji wa sammaki,ujenzi wa mabanda ya kuku,nguruwe,ngombe nk,civil engineer ni mjenzi wa maghala ya kuhifadhi vyakula,ujenzi wa miundo mbinu ya kilimo ya mashamba makubwa (estates) huangua chini yake,Huwezi kuongelea ujenzi wa miundo mbinu yoyote ya kilimo,mifugo au maji bila kumweka civil engineer.
Acha mawazo yasio na maana ndugu... mimi ni mtu wa Mwambao... je, kuna uhusiano wowote hapo na Dr. Turuka ambae hata anakotoka sikufahamu?!!

Kuhusu civil engineer na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji... nimekuambia utatumia civil engineer kwa shida tu kwa sababu hilo sio eneo lake! Kama shida ni ujenzi wa miundombinu ya kilimo; hii nchi ina irrigation and agricultural engineers kibao tu kwahiyo kama hoja ingekuwa ni miundo mbinu ya kilimo basi angechukua hao watu na sio mtu ambae kasomea ki-unit kimoja au viwili wakati kuna wengine wametumia miaka 4!

Lakini yote kwa yote naona unachanganya mambo!!! Katibu Mkuu hataingia field kujenga hiyo mitaro unayoema bali yeye ni mtendaji wa wizara... mtu ambae anatakiwa kuifahamu sekta ya kilimo na mapana yake! Mtu ambae anafahamu changamoto za sekta ya kilimo...!! Changamoto namba moja ya sekta ya kilimo sio malambo ya kunyweshea, au maghara ya kuhifadhia au mifereji ya umwagiliaji n.k bali changamoto ya kwanza na kubwa by far ni masoko!! Changamoto zingine zoooooooote ni zao la changamoto ya masoko!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom