Kwako Mh. Dr John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kwanza nakupongeza kwa mema unayoyafanya. Hivi karibuni umefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa na kufanya mabadiliko ya Makatibu Wakuu wa Wizara mabalimbali. Moja ya wizara zilizopata mabadiliko ni wizara kilimo. Kwenye Mabadiliko hayo Mh. Rais umembadilisha Dr Florens Turuka kwenda Wizara ya Ulinzi na kumleta Mhandisi Mathew Mtigumwe wizara ya Kilimo. Kwa heshima kubwa nakusihi umwache Dr Turuka hapa kilimo kwa sababu zifuatazo:
1. Huyu mtu anaifahamu sana hii secta na tangia afike hapa wizarani utendaji wake umeonekana kwa kuunganisha wafanyakazi tofauti na watangulizi wake wengi.
2. Dr Turuka ni mtu mchapakazi, muadilifu na mnyenyekevu. Kama mtendaji wa wizara ameweza kusimamia mambo ambayo yalikuwa hayaendi sawasawa.
3. Panapomstathili ni hapa wizara ya kilimo kwa sababu kitaaluma Dr Turuka ni Mchumi kwenye masuala ya kilimo (Agricultural Economist). Sisi kama watumishi tulioko chini yake tumemuona kama mtu mwenye ueledi na kazi yake, hana majungu, anaelekeza na kuonyesha uongozi.
Mwisho nitoe ushauri kuwa Mh. Rais hii wizara inahitaji taaluma, uzoefu na umahiri wa kazi wa hali juu kama alivyo Dr. Turuka. Hii wizara haiitaji mtawala bali kiongozi. Hivyo nakusihi kwa heshima nyingi umuongezee angalau miaka miwili Dr. ili yale mema aliyoanzisha aweze kuyasimamia na kukamilisha.
Nawasilisha