leipzig
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 2,766
- 1,707
Mh. Rais tunakupongeza kwa juhudi zako za kupambana na wizi, ubadhirifu na ufisadi wa mali za umma ambapo imepelekea kuokoa fedha nyingi za serikali kupotea mikononi mwa watumishi wachache wenye tamaa na ubinafsi.
Lakini sasa tuangalie na sisi wakulima, tunakuomba Mh. Rais na serikali yako utujengee malambo au mabwawa vijijini ambayo yatahifadhi maji ya mito na maji ya mvua ili yatumike katika umwagiliaji mashambami na kunyweshea mifugo.
Nasema hivi kwa sababu kilimo ndio tegemeo letu kubwa kwa watanzania tulio wengi. Hapo nyuma tulikuwa tunalima lakini pia tulikuwa tunawategemea watoto wetu walioko mjini kwa kututumia misaada ya fedha lakini tangu uwatumbue hatupati hiyo misaada tena na ukiwauliza hawatoi jibu.
Pia ningekushauri uwaelekeze wataalamu mbalimbali wa kilimo waje huku vijijini ili watupe utaalamu wa kilimo cha umwagiliaji na ufugaji. Sisi watanzania huku vijijini tuna nia sana ya kulima isipokuwa tunakosa misaada ya utaalamu wa kilimo bora na masoko ya mazao yetu.
Mwisho naamini kama Mh. Rais utatusaidia kwa hilo basi hali zetu kiuchumi zitakuwa bora. Pia vijana wengi wasio na kazi wanaozurura mijni watarudi vijijini kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji. Nakumbuka huko nyuma mkoani Kilimanjaro kulikuwa na mfano wa kilimo cha umwagiliaji eneo la Mabogini ambapo kampuni ya kijapani Konoike ilijenga mabwawa na mifereji.
Tunatanguliza shukurani endapo ombi letu litasikilizwa na kufanyiwa kazi.