Rais Magufuli, this is serious. Tafadhali usiruhusu hili!

Mhe. Rais,nina ujumbe mfupi tu kwako. Tafadhali usiruhusu Serikali yako kuwa ya visasi,kuchongeana na 'kucheza na jukwaa'. Pale ambapo watumishi wa umma watapaswa kushughulikiwa,Sheria za Utumishi wa Umma na zile za Ajira zisiwekwe kando na hasira,malengo na uharaka wa kutumbua majipu.

Utumbuaji wa aina ya wa Wilson Kabwe unatweza na kuchora picha ya visasi na kuchongeana. Watumishi wa umma wapewe nafasi kujieleza kabla ya kushughulikiwa. Kwa hali inayoendelea,it is serious and the country is heading to unpleasant situation.

Watumbuliwaji nao wanastahili staha na faragha! Kwanini heshima ilindwe kwa watumishi wa BOT tu?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mzee vp umeguswa nini maana majipu huwa na mizizi sehemu na wewe ndio mzizi wenyewe nini magufuli kakugusa. Vumilia au achia ngazi hizi ni zama mpya za uongozi.
 
Ina maana hujamuelewa? Pamoja na kumuunga mkono JPM kuwawajibisha wabadhirifu na wazembe, njia inayotumika kwa sasa siyo sahihi kabisa. Hakuna malaika duniani,sote tu wakosaji. Sheria ichukue mkondo wake. Sijui familia ya Kabwe leo itajisikiaje leo. Siyo vizuri kuona mwingine akipata kadhia tena kwenye kadamnasi.
Hiyo ndiyo haki yake. Hata kama kwa jicho la sheria itakuwa ni vigumu kumtia hatiani tutakuwa tumeokoa kiasi.
Ukiwa unafanya uhalifu fahamu kuwa utakuja kubainika na utaaibika. Mwisho wa ubaya aibu.
 
Pale mbele ya delegate yote ile na vyombo vya habari vya ndani na nje hapakuwa mahali sahihi pa ile sarakasi ya Magufuli na kijana wake hivi vitu havikuzingatiwa
-busara
-hekima
-Protocol
-weledi
-timing
-haiba na jinsi ya kuwajibishana
Mwanao hata akosee vipi huwezi kumuadhibu siku ya sherehe tena mbele ya wageni
what a comment
 
Asilolijiua ni kuwa atawafanya hata wale waliokuwa hawaamini kuwa anafanya haya kwa sifa nao waanze kuamini.Kuna ulazima gani wa kumsimamisha mtu kazi mbele ya Akadamnasi kama ile?

Fukuza/simamisha watu kazi lakini usipende kufanya hivyo kila wakati ukiwa mbele ya camera.
Inashangaza sana kuona watu wanawatetea wahalifu na mafisadi hawa. Hivi hamuoni ukubwa wa tatizo lenyewe? Watu wanaaminiwa na kupewa uongozi badala ya kutumikia taifa wanalihujumu? Kuwaumbua hadharani kutasaidia wengine wasithubutu kuihujumu serikali.
 
Kujieleza ndo ilileta nafasi ya madudu kufanyika kipind kile cha yule.
Em fikir tume imeundwa na watu wamedetect nyaraka zote. Hapo tunaenda kusikiliza nini
Kumpa nfasi mwiz ajiteteeee ni kuidharau sheria
 
eti mnamuonea huruma mchakachuaji ,mnataka uthibiyisho gani wakati mkataba miwili tofauti inaonesha jamaa namna alivyo mbinafi na mlafi...naunga mkono alivyotumbuliwa hao watu c wakuwaonea huruma iseee wanatunyonyo haswaaa..
 
NAUNGA MKONO KABWE KUTUMBULIWA.

By Malisa GJ,

Kwa mijibu wa RC Paul C. Makonda, Wilson Kabwe alisainisha mikataba miwili kwa wamiliki wa mabasi kwa sheria mbili tofauti (ya mwaka 2004 na 2006). ByLaw ya 2004 inataka bus likitoka Ubungo lilipe Sh.4,000/= na ya 2006 inataka bus lilipe Sh.8,000/=.

Wamiliki wa mabasi walisainishwa kulipa 8,000/= lakini jiji likarekodi kuwa wanalipa Sh.4,000/=. Maana yake ni kuwa kila bus lilikua likilipa Sh.8,000/=, lakini zilizokua zikiingia Halmashauri ya jiji ni Sh.4,000/= tu. Nyingine ziliingia mfukoni kwa Kabwe.

Kwahiyo katika magari 400 yanayotoka Ubungo kwa siku Kabwe alikua anaingiza 1,600,000/= kila siku mfukoni mwake. Hizi ni sawa na Milioni 48 kwa mwezi. Sawa na milioni 576 kwa mwaka.

Hii ni moja ya tuhuma kadhaa alizozieleza Makonda. Kwa kifupi Kabwe ni mpiga dili. Hata kule Mwanza alipiga dili nyingi akawa analindwa na "mkwere".. Kupitia dili hizo alijenga vitega uchumi kadhaa ikiwemo Hoteli ya kifahari ya "Royal Sunset Beach" kule Luchelele.

Hebu jiulize kama kwenye dili moja tu ya mabasi Ubungo anatengeneza Milioni 576 kwa mwaka, ukijumlisha na hizo dili nyingine ana earn kiasi gani? Ni ajabu kama tutamtetea mtu mwenye tuhuma kama hizi.

Yani wakati wewe una mwaka wa 4 unatafuta kazi bila mafanikio hata nauli ya kutembeza CV yako huna, mwenzio anaingiza Milioni 500+ kwa mwaka kupitia dili moja tu. Hakika utakua "zwazwa wa shahada ya juu ya uzamivu (PhD)" kama utamtetea.

Najua kuna "principle of natural justice" lakini hizi natural justice ndio zimetuharibia nchi na kutufikisha hapa tulipo. Mtu anaiba hela halafu anaundiwa Tume imchunguze na tume inalipwa tena hela. No. Si sawa.!

Naunga mkono Maamuzi ya Rais Magufuli kumuweka kando huyu Mkurugenzi mwenye tuhuma lukuki. Tangu akiwa jiji la Mbeya, Mwanza na hatimaye Dar amekuwa akituhumiwa tu.

Ezekia Wenje amewahi kumlalamikia bungeni, Kiwia amewahi kumlalamikia bungeni, viongozi na wananchi kibao wamewahi kumlalamikia lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake. Leo kaambiwa akae pembeni kupisha uchunguzi mnamtetea? Mtakuwa mmelogwa walahi.!

Kwanini atuhumiwe yeye tu? Haiwezekani watu wote wamchukie yeye tu.

Makonda kafanya jambo la msingi sana leo kuliko wakati mwingine wowote ktk historia yake. Katetea machozi ya wanyonge. Kakatisha dili za watawala kujishibisha kwa kutumia migongo ya maskini.

Mkumbuke huyu Kabwe ndiye aliyemvua Uraia Ezekiah Wenje mwaka 2010 kwenye uchaguzi mkuu ili Lawrence Masha apite bila kupingwa. Akasema Wwnje ni raia wa Kenya. Ktk kutetea haki yake Wenje akapeleleka malalamiko yake Makao makuu ya NEC na baada ya kupitia vielelezo wakadhibitisha Wenje ni raia. Sasa mtu wa aina hii bado mnamtetea?

Alipokua Mbeya alituhumiwa akahamishiwa Mwanza. Alipokuwa Mwanza alituhumiwa akahamishiwa Dar. Akiwa Dar ametuhumiwa, sasa mnataka ahamishwe tena? Eti principle of Natural justice. Sasa mnataka natural justice kwny tuhuma zilizo wazi?

Hata hivyo tujiulize Kabwe ni kweli Kabwe hajapewa haki ya kusikilizwa as per principle of Natural Justice?? Wanaojenga hoja hii labda hawaelewi vizuri maana ya Natural Justice.

Napenda kuwakumbusha kuwa Kabwe hajahukumiwa bado. Amewekwa kando kupisha uchunguzi. Kuhusu nafasi ya kujitetea ataitwa na kuhojiwa adhering na abtapewa hiyo haki ya "natura justice" mnayoitaka.

Alichokifanya Rais ni kumpumzisha Kabwe ili ahojiwe akiwa nje ya nafasi yake. Akichunguzwa akiwa bado kwny kiti cha ukurugenzi ataathiri uchunguzi. Kwahiyo ni vema akae pembeni kwanza ili achunguzwe vizuri kwa uhuru. Atendewe haki.!

Lakini im very sure hawezi kupona. Hii ndio byebye.!

Nimeichukua kwa (Malisa GJ.!)
Shikamoooo kaka
 
Mwanza alipiga dili nyingi akawa analindwa na "mkwere".. Kupitia dili hizo. Alichosema mtoa mada ni kwamba taratibu na kanuni zifuatwe, si kama alivyofanya Rais. Mtumishi wa umma anatimuliwa jukwaani.???
 
Pale mbele ya delegate yote ile na vyombo vya habari vya ndani na nje hapakuwa mahali sahihi pa ile sarakasi ya Magufuli na kijana wake hivi vitu havikuzingatiwa
-busara
-hekima
-Protocol
-weledi
-timing
-haiba na jinsi ya kuwajibishana
Mwanao hata akosee vipi huwezi kumuadhibu siku ya sherehe tena mbele ya wageni
mkuu inategemea na Baba, wazaz wengine haangalii leo ijumaa,jmos u j2, au kunamgen au ni skukuu, as longer as imefanya upuuzi, ni papo kwa hapo, baadae ndo utasema ila baba pale asee hukufanya vyema..

hyo ndo magu, wengine tulimjua mapema na tulivote tukijua aje ili awe hvyo ili mambo yaende..
 
Mkuu JPM hanaga na haelewi kuwa kuna mamlaka za utumishi kanuni na sheria husika. Kweli mmetuletea mchapa kazi, lakini mngempa stadi za uongozi kwa sababu za utendaji tayari anazo. Kumbukeni nchi inaongozwa na maono yanayoelekeza utendaji. Nchini kwetu kwa sasa nchi inaongozwa na utendaji usio na maono.

Kama ulivyosema huko tunakoelekea hakueleweki; ni mshike mshike jahazi kuzama. Tulipoyasema haya hamkutaka kutusikiliza, ila sisi tutaendelea kuwa wananchi watiifu hatutaki vurugu ingawa tunavurugwa.
Nchi inaongozwa na mihemko ni hatari mno.
 
Asilolijiua ni kuwa atawafanya hata wale waliokuwa hawaamini kuwa anafanya haya kwa sifa nao waanze kuamini.Kuna ulazima gani wa kumsimamisha mtu kazi mbele ya Akadamnasi kama ile?

Fukuza/simamisha watu kazi lakini usipende kufanya hivyo kila wakati ukiwa mbele ya camera.
Hivi na yule Makonda siku zoote kashindwa kumripoti mpaka kwenye makamera meengi(mbona kama muvi hii.)
 
Style unayoitaka ndiyo imelea uozo huu kwa hiyo hatutaki hayo tena na kila nabii na kitabu chake. Usikariri formula na hiyo pia ndiyo dawa kwa wezi wengine wataogopa kuadhirika hadharani ni sawa na mgogoro wa mpAka kati ya malawi na Tza uliisha kwa style gani kama unakumbuka? Au magari ya majimoto ya polisi yalivyoingia uliona nani alikwenda kulinda kura wakati wa uchaguzi?Pamoja na kuwa chama fulani kiliapa kulinda kura nani alitoka NA unadhani kwa nini hawakutoka kwenda kulinda kura jibu unalo na hiyo ndiyo administration style ya Prezidaa Magufuli kwamba kama na wewe unaiba basi jiandae kuabika kama kabwe kabla ya kushitakiwa.
Huko ni kupotosha. Style ya kufuata sheria ndo imetufikisha hapa, kivipi?.Haiwezekani utumie sheria ipasavyo halafu upate matokeo hasi, siamini katika hilo
 
Uku niliko watumishi wa umma wamekuwa waoga.hakuna anayemgusa mwananchi kila mtu anafanya vyake
 
NAUNGA MKONO KABWE KUTUMBULIWA.

By Malisa GJ,

Kwa mijibu wa RC Paul C. Makonda, Wilson Kabwe alisainisha mikataba miwili kwa wamiliki wa mabasi kwa sheria mbili tofauti (ya mwaka 2004 na 2006). ByLaw ya 2004 inataka bus likitoka Ubungo lilipe Sh.4,000/= na ya 2006 inataka bus lilipe Sh.8,000/=.

Wamiliki wa mabasi walisainishwa kulipa 8,000/= lakini jiji likarekodi kuwa wanalipa Sh.4,000/=. Maana yake ni kuwa kila bus lilikua likilipa Sh.8,000/=, lakini zilizokua zikiingia Halmashauri ya jiji ni Sh.4,000/= tu. Nyingine ziliingia mfukoni kwa Kabwe.

Kwahiyo katika magari 400 yanayotoka Ubungo kwa siku Kabwe alikua anaingiza 1,600,000/= kila siku mfukoni mwake. Hizi ni sawa na Milioni 48 kwa mwezi. Sawa na milioni 576 kwa mwaka.

Hii ni moja ya tuhuma kadhaa alizozieleza Makonda. Kwa kifupi Kabwe ni mpiga dili. Hata kule Mwanza alipiga dili nyingi akawa analindwa na "mkwere".. Kupitia dili hizo alijenga vitega uchumi kadhaa ikiwemo Hoteli ya kifahari ya "Royal Sunset Beach" kule Luchelele.

Hebu jiulize kama kwenye dili moja tu ya mabasi Ubungo anatengeneza Milioni 576 kwa mwaka, ukijumlisha na hizo dili nyingine ana earn kiasi gani? Ni ajabu kama tutamtetea mtu mwenye tuhuma kama hizi.

Yani wakati wewe una mwaka wa 4 unatafuta kazi bila mafanikio hata nauli ya kutembeza CV yako huna, mwenzio anaingiza Milioni 500+ kwa mwaka kupitia dili moja tu. Hakika utakua "zwazwa wa shahada ya juu ya uzamivu (PhD)" kama utamtetea.

Najua kuna "principle of natural justice" lakini hizi natural justice ndio zimetuharibia nchi na kutufikisha hapa tulipo. Mtu anaiba hela halafu anaundiwa Tume imchunguze na tume inalipwa tena hela. No. Si sawa.!

Naunga mkono Maamuzi ya Rais Magufuli kumuweka kando huyu Mkurugenzi mwenye tuhuma lukuki. Tangu akiwa jiji la Mbeya, Mwanza na hatimaye Dar amekuwa akituhumiwa tu.

Ezekia Wenje amewahi kumlalamikia bungeni, Kiwia amewahi kumlalamikia bungeni, viongozi na wananchi kibao wamewahi kumlalamikia lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake. Leo kaambiwa akae pembeni kupisha uchunguzi mnamtetea? Mtakuwa mmelogwa walahi.!

Kwanini atuhumiwe yeye tu? Haiwezekani watu wote wamchukie yeye tu.

Makonda kafanya jambo la msingi sana leo kuliko wakati mwingine wowote ktk historia yake. Katetea machozi ya wanyonge. Kakatisha dili za watawala kujishibisha kwa kutumia migongo ya maskini.

Mkumbuke huyu Kabwe ndiye aliyemvua Uraia Ezekiah Wenje mwaka 2010 kwenye uchaguzi mkuu ili Lawrence Masha apite bila kupingwa. Akasema Wwnje ni raia wa Kenya. Ktk kutetea haki yake Wenje akapeleleka malalamiko yake Makao makuu ya NEC na baada ya kupitia vielelezo wakadhibitisha Wenje ni raia. Sasa mtu wa aina hii bado mnamtetea?

Alipokua Mbeya alituhumiwa akahamishiwa Mwanza. Alipokuwa Mwanza alituhumiwa akahamishiwa Dar. Akiwa Dar ametuhumiwa, sasa mnataka ahamishwe tena? Eti principle of Natural justice. Sasa mnataka natural justice kwny tuhuma zilizo wazi?

Hata hivyo tujiulize Kabwe ni kweli Kabwe hajapewa haki ya kusikilizwa as per principle of Natural Justice?? Wanaojenga hoja hii labda hawaelewi vizuri maana ya Natural Justice.

Napenda kuwakumbusha kuwa Kabwe hajahukumiwa bado. Amewekwa kando kupisha uchunguzi. Kuhusu nafasi ya kujitetea ataitwa na kuhojiwa adhering na abtapewa hiyo haki ya "natura justice" mnayoitaka.

Alichokifanya Rais ni kumpumzisha Kabwe ili ahojiwe akiwa nje ya nafasi yake. Akichunguzwa akiwa bado kwny kiti cha ukurugenzi ataathiri uchunguzi. Kwahiyo ni vema akae pembeni kwanza ili achunguzwe vizuri kwa uhuru. Atendewe haki.!

Lakini im very sure hawezi kupona. Hii ndio byebye.!

Nimeichukua kwa (Malisa GJ.!)
Hakuna mtu anapinga kabwe kusimamishwa kinachogomba ni jinsi au njia iliyotumika kumsimamisha! Mr malisa ungemwelewa mzee tupatupa sidhani kama ungepost ulichopost
 
Hakuna aliyedhalilishwa na hakuna aliye onewa according to Administrative law na principle mama ya Natiral justoce ndiyo anayotembea nayo Raisi, kwa hiyo katika kipengere cha Hear both side kitatimizwa na mahakama.
wadau binafsi naomba nikili pamoja na kuwa tunasema mifumo ni dhaifu au mibovu lakini pamoja na ubovu wake hakuna mfumo unaruhusu ufujaji wa mali ya umma, hakuna mfumo unao dai kiongozi kumnyonya kapuku, mifumo yetu iko imara lakini ili lega lega kwa sababi ilikosa watu imara wa kuisimamia mifumo hiyo
 
Huko ni kupotosha. Style ya kufuata sheria ndo imetufikisha hapa, kivipi?.Haiwezekani utumie sheria ipasavyo halafu upate matokeo hasi, siamini katika hilo
Hizi sheria , kanuni na taratibu watu wanataka zifuatwe wakati wa kumsimamisha mtu kazi . Tukumbuke pia umuhimu wa kuzifuata tunapokuwa ofisini. Ukivunja taratibu na wewe tunakusimamisha kinyume na utaratibu , mambo mengine yataendelea baadaye. Kumbuka Msemo " yaliyofanyika gizani yatawekwa nuruni '' pale darajani palikuwa na nuru ya kutosha.
 
Back
Top Bottom