Mulhat Mpunga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 27,263
- 16,288
Hahaha mungu anatuonaEehe Mungu tulikosea wapi??????
Hahaha mungu anatuonaEehe Mungu tulikosea wapi??????
Hahaha uwii I hate ccm with all my strength f*****Mfuko wa TAIFA wa maafa hauna senti yaani uhuru Na Museveni wanarespond haraka kuliko serikali.
Unaahirisha ziara alafu unajifungia Ikulu wiki nzima ......sibora angeenda Zambia akamuombe waachee kupitisha copper Durban Wakati Tazara iPo..
Rais akienda mahala Ni Tofauti Na Waziri Mkuu Au Makamu ...rais Ni rais na marais wanaongea Na marais mambo ya kuongea Na mtu ambaye Hana uamuzi wa mwisho hawapendi
Napata ukakasi. Kazi tayo.Lakini afadhali kawaeleza ukweli ingawaje mchungu. Nafikiri kipindi hiki watu watatia akili tu.
..ameingia kupitia ujinga wako...rudi soma quote yako ya kwanza...usizoee kujibu ujinga kwa kila post inayosoma....ficha upumbavu wako....mkuu huyo fuckn mother ameingiaje hapa?
hoja nyingine ni kuwa aliomba japo robo ya roho ya JK na SHEIN kwa nyakati tofauti je yeye ana roho ya aina gani??siku zote mwanaume unavyoonekana ukiwa na wenzio maneno na matendo yako vinakisi mbali sana ...
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.
Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.
Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.
Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
=======
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemoko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Mara kutoka kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Ikulu DSM.
Rais Magufuli akipokea taarifa pamoja na misaada iliyochangwa na nchi jirani
Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na takribani Shilingi za Kitanzania Milioni Mia nne na therathini na saba (Tshs-437,000,000/-) kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Katika taarifa yake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
Mhe. Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali zikiwemo kupeleka chakula, huduma za matibabu na hifadhi za dharura kwa waathirika na pia inaratibu ukusanyaji wa michango kutoka sehemu mbalimbali ambapo mpaka sasa kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni tatu nukta sita (Tshs Bilioni 3.6) zimepatikana.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya maafa na michango kwa ajili ya waathirika wa maafa hayo, Rais Magufuli amewashukuru wote waliojitoa kusaidia waathirika wakiwemo Marais Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mhe. Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda ambao wamempigia simu za kumpa pole na tayari wametoa misaada yao, na pia nchi mbalimbali, mashirika, wafanyabiashara, watumishi wa umma na watu binafsi na amesema michango hiyo ina umuhimu mkubwa katika kukabiliana na athari za maafa haya.
Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania na wote walioguswa na maafa haya kuendelea kutoa misaada kwa waathirika kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku akionya na kuvitaka vyombo vya dola kuwafuatilia watu wanaotaka kutumia maafa haya kukusanya michango kwa lengo la kujinufaisha.
Rais Magufuli amebainisha kuwa Serikali itahakikisha inarekebisha miundombinu iliyoharibika zikiwemo shule, vituo vya matibabu, barabara na huduma nyingine za kijamii na pia ametaka wananchi waliokumbwa na madhara ya tetemeko hususani nyumba zilizobomoka, wajipange kurekebisha nyumba zao kwa kuwa Serikali pekee yake haitaweza kujenga nyumba zote zilizobomoka.
Aidha, Rais Magufuli amewasihi Watanzania kuwapuuza watu wanaotaka kutumia maafa haya kueneza uchonganishi na chuki dhidi ya Serikali na ameweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna teknolojia ya kutabiri kutokea kwa tetemeko la ardhi na kwamba tetemeko hili halikuletwa na Serikali.
Dkt. Magufuli amesema hata mataifa makubwa yenye maendeleo makubwa ya uchumi na teknolojia yanakumbwa na tetemeko la ardhi na kusababisha vifo vya idadi kubwa ya wananchi na uharibifu mkubwa wa mali.
"Nilikuwa najaribu kuangalia kwa mfano nchi kama China kwenye mwaka 2014 watu 617 walipoteza maisha, Mwaka 2013 walipoteza watu 193, Mwaka 2010 walipoteza watu 2,998 Mwaka 2008 China ilipoteza watu 98,712.
Ukijaribu kuangalia Japan, nchi ambayo imeendelea na ina utaalamu wa hali ya juu sana, kwenye mwaka 2016 tarehe 14 mwezi wa nne ilipoteza watu 6, baada ya siku mbili tarehe 16 mwezi wa nne 2016 tetemeko likatokea tena na likaua watu 35, mwaka 2012 likaua watu 3, mwaka 2011 likaua watu 15,904 mwaka 2008 likaua watu 12, mwaka 2007 likaua watu 11, mwaka 2004 likaua watu 40, mwaka 1923 liliua watu 142,800 na hiyo ni Japan. Amesisitiza Rais Magufuli.
Shughuli ya kupokea taarifa ya Waziri Mkuu na michango kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na Mikoa jirani imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe. Dorothy Hyuha na Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Boniface Muhia.
Chanzo: IPP Media
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
You missed da points mkuu...Watanzania wamezoea kupata faraja hewa na hawataki kuambiwa ukweli. Rais kaongea kweli tupu mm namuunga mkono.
Nimependa ulivyoniita firauni japo hunijui, nakufundisha siku nyingine weka alama ili tujue kuwa hutaki kuwa quoted,We Firauni koma kuni Quote! Unafikir mie nimsukuma mwenzako?
Inawezekana kabisa kuna watu inabidi waelimishwe kuhusu hilo. Si unajua mambo ya shule za kata yalivyo na matatizo? Kama mtu anaweza kuishukuru serikali kwa kuuchagua Mkoa wa Mbeya kuwa ndiyo sehemu ya kupatwa na Jua, itashindikanaje watu wa aina hiyo kuamini kuwa Serikali hiyo hiyo imechagua Bukoba kuwa sehemu ya kupatwa na tetemeko? Halafu hapo unaambiwa elimu imepanda kiwango. Je ilipokuwa chini hali ilikuwaje?Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?