Rais Magufuli, shirikisha wabunge wa upinzani ndio vita hii utashinda

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,316
72,742
Baada ya kusikia kuwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM ulilaumiwa kwa kuachia uchaguzi wa Meya wa Dar kufanyika kwa haki huku kukiwa na kauli kuwa" hao mawaziri na kiongozi yeyote asingepata nafasi kama sio CCM" ni wazi huwezi kupata msaada wowote zaidi ya vikwazo kutoka chama chako katika dhamira yako ya kutumbua majipu.

Ili ufanikiwe, wape uwanja huru wa bunge wa upinzani na wachache wa CCM wenye uthubutu wa kusema maovu hadharani nawe uchukulie hatua kuanzia hapo na kubwa ni kuruhusu mijadala ya bunge kuwekwa live ili ukweli uwe wazi kwa kila mtu badala ya kuchunjwa kwa habari.Live coverage inasaidia hata wananchi wako kushiriki mijadala katika mitandao ya kijamii jambo ambalo linawapa raia nayo kusema kule ambacho wanakijua.
 
Maneno kuntu
Akisubiri afanye kazi hiyo ya kung'amua viongozi na watendaji waovu itamchukua zaidi ya miaka 10 kutokana na ukubwa wa nchi, na wanaoweza kuwalipua watu hao bila woga na hadharani ni wabunge wa upinzani naye kazi yake itakuwa rahisi
 
Baada ya kusikia kuwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM ulilaumiwa kwa kuachia uchaguzi wa Meya wa Dar kufanyika kwa haki huku kukiwa na kauli kuwa" hao mawaziri na kiongozi yeyote asingepata nafasi kama sio CCM" ni wazi huwezi kupata msaada wowote zaidi ya vikwazo kutoka chama chako katika dhamira yako ya kutumbua majipu.

Ili ufanikiwe, wape uwanja huru wa bunge wa upinzani na wachache wa CCM wenye uthubutu wa kusema maovu hadharani nawe uchukulie hatua kuanzia hapo na kubwa ni kuruhusu mijadala ya bunge kuwekwa live ili ukweli uwe wazi kwa kila mtu badala ya kuchunjwa kwa habari.Live coverage inasaidia hata wananchi wako kushiriki mijadala katika mitandao ya kijamii jambo ambalo linawapa raia nayo kusema kule ambacho wanakijua.

Muda si mreefu ujao, Magu atakuwa CHAIRMAN wa hiyo CC wasi wasi wako ni nini?
 
Kuwa chairman haitoshi kwa chama ambacho mizizi ya uchafu imejichimbia. Anayofanya JK yanabaraka zote za chama chake ndio maana bado yupo pale. Kumbuka kwenye chama kama hutakubaliana na wenzako kikao cha NEC kinaweza kukung'oa kama walivyotaka kumng'oa JK wakati ule.
Hivyo dhamira ya JPM ambayo ni agenda ya kitaifa lazima awashirikishe wabunge ambao jukwaa la kusemea wanalo
 
Hapo a
Baada ya kusikia kuwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM ulilaumiwa kwa kuachia uchaguzi wa Meya wa Dar kufanyika kwa haki huku kukiwa na kauli kuwa" hao mawaziri na kiongozi yeyote asingepata nafasi kama sio CCM" ni wazi huwezi kupata msaada wowote zaidi ya vikwazo kutoka chama chako katika dhamira yako ya kutumbua majipu.
Ili ufanikiwe, wape uwanja huru wa bunge wa upinzani na wachache wa CCM wenye uthubutu wa kusema maovu hadharani nawe uchukulie hatua kuanzia hapo na kubwa ni kuruhusu mijadala ya bunge kuwekwa live ili ukweli uwe wazi kwa kila mtu badala ya kuchunjwa kwa habari.Live coverage inasaidia hata wananchi wako kushiriki mijadala katika mitandao ya kijamii jambo ambalo linawapa raia nayo kusema kule ambacho wanakijua.
Hapo atakuwa amefaulu mtihani na kazi yake itakua rahisi sana, hahitaji kutumia nguvu nyingi,kama kweli anauchukia ufisadi na anawatakia Wanzania maisha mazuri ajaribu kwa mwaka mmoja aone mafanikio yake.
 
Tumesikia na kusoma ktk Mitandao ya jamii JF Mh.Sugu akilalamika ya kuwa wabunge wa Upinzani waliyopata nafasi za kuteulewa walitoa/kuombwa Rushwa Naibu katibu mkuu Salim Maalim akihusishwa.Swali hapa hao wabunge wa upinzani waliyopata nafasi kwa Rushwa kweli watamsaidia Mh.Raisi kikweli kweli ktk vita ya Rushwa
 
Mkuu Chakaza huwa naheshimu sana thread zako japokuwa upo UKAWA lakini umeonyesha kuipenda nchi yako kuliko cha chako.Ushauri ulioutoa ni mzuri sana lakini naomba kutofautiana na wewe kidogo,siyo wapinzani wote ni wasafi na wanafa kushiriki vita dhidi ya ufisadi kwa mfano kuna baadhi ya wabunge wa upinzani wameungana na baadhi ya wabunge wa CCM kuanzisha kampeni ya kataa magufuli njaa ndani ya Bunge katika wabunge Msigwa na Zitto wametajwa kuhusika vilivyo sasa watu kama hawa tutawaamini vipi?.Kuwa mpinzani siyo tiketi ya kuwa muadilifu.
 
Baada ya kusikia kuwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM ulilaumiwa kwa kuachia uchaguzi wa Meya wa Dar kufanyika kwa haki huku kukiwa na kauli kuwa" hao mawaziri na kiongozi yeyote asingepata nafasi kama sio CCM" ni wazi huwezi kupata msaada wowote zaidi ya vikwazo kutoka chama chako katika dhamira yako ya kutumbua majipu.

Ili ufanikiwe, wape uwanja huru wa bunge wa upinzani na wachache wa CCM wenye uthubutu wa kusema maovu hadharani nawe uchukulie hatua kuanzia hapo na kubwa ni kuruhusu mijadala ya bunge kuwekwa live ili ukweli uwe wazi kwa kila mtu badala ya kuchunjwa kwa habari.Live coverage inasaidia hata wananchi wako kushiriki mijadala katika mitandao ya kijamii jambo ambalo linawapa raia nayo kusema kule ambacho wanakijua.

Mkuu mimi nakuunga mkono hoja yako 100%. kama Mh.JPM akikubali hoja yako yakushirikiana na wabunge werevu,makini,wasio na tamaa wa upande wa pili. Tena wale wenye uthubutu wakukataa mil.30 za taasisi mbalimbali ili kuongeza kelele za ndiyooohh..! ama kusimama na kuchangia uongo kwa kununuliwa na wawekezaji ama taasisi za umma- to advocate wrong in a positive way" ni sawa. Lakini labda tu tuweke angalizo, wasipewe issue ya kuanika wahusika wa ufisadi Fulani halafu wakaonyesha dalili za kupata taarifa za kiiteligensia side'A' halafu wakamtaja Mh.Rais, maana kuna mps wengine wa upinzani hawashindwi kutokwa tu na maneno na kujikuta wametaja source halafu waka create hostility na antagonistic kubwa kwa mh. na watendaji wake pamoja na chama chake. wajifunze kwa mzito kabwela master-mind of all the game"
 
Ili ufanikiwe, wape uwanja huru wa bunge wa upinzani na wachache wa CCM wenye uthubutu wa kusema maovu hadharani nawe uchukulie hatua kuanzia hapo na kubwa ni kuruhusu mijadala ya bunge kuwekwa live.

Haya majipu yanayotumbuliwa ni coverage ya bunge LIVE? Bunge wala halipo na majipu ni mengi yametumbuliwa hakuna mbunge aliyetoa.

Kama mtu anasubiri hadi bunge lianze apewe coverage live ndio ataje anatupotezea muda na wala hatumhitaji.Jamiiforums iko hapa aweke anasubiri hadii bunge huyo mwehu?

Magazeti yapo na yanafanya kazi nzuri ya kuanika kila wanapoona jipu!! Huyo anayesubiri kuuza sura kwenye tv afie huko.Ana majina na jipu ataje sasa.
 
Mkuu Chakaza huwa naheshimu sana thread zako japokuwa upo UKAWA lakini umeonyesha kuipenda nchi yako kuliko cha chako.Ushauri ulioutoa ni mzuri sana lakini naomba kutofautiana na wewe kidogo,siyo wapinzani wote ni wasafi na wanafa kushiriki vita dhidi ya ufisadi kwa mfano kuna baadhi ya wabunge wa upinzani wameungana na baadhi ya wabunge wa CCM kuanzisha kampeni ya kataa magufuli njaa ndani ya Bunge katika wabunge Msigwa na Zitto wametajwa kuhusika vilivyo sasa watu kama hawa tutawaamini vipi?.Kuwa mpinzani siyo tiketi ya kuwa muadilifu.
Mkuu nayo ya kuwa Ukawa au CCM we yaache, hayo ni sawa na Okwi Leo Yanga kesho Simba inategemea na hali ikoje.
Nakubaliana nawe kuwa sio kuwa wa bunge wrote wa upinzani ni watu wasema kweli kama ilivyo kwa CCM kuwa sio kwamba wa bunge wote wanatetea waovu.
Kila upande una wazuri na wa hovyo. Ila nasema awashirikishe wa upinzani kwani kwa mtazamo wa chama chake hao wanaonekana wabaya wa kuyatoa hadharani makosa ya watendaji wa serikali jambo ambalo ndio dhamira ya Magufuli.
Hebu fikiria kama JK angekuwa anayashughulikia yaliyokuwa yanaibuliwa bungeni hivi Magufuli angekutana na mauoza yote hata?
 
UKAWA nayo imekuwa na watu wa kumshauri Magufuli? Tuachieni ambao hatuna vyama tufanye kazi hiyo!
 
Kushirikisha akili za upinzani ni kumdhirikisha lowassa, kazi itakua bure bora aendelee na task force zake
 
Haya majipu yanayotumbuliwa ni coverage ya bunge LIVE? Bunge wala halipo na majipu ni mengi yametumbuliwa hakuna mbunge aliyetoa.

Kama mtu anasubiri hadi bunge lianze apewe coverage live ndio ataje anatupotezea muda na wala hatumhitaji.Jamiiforums iko hapa aweke anasubiri hadii bunge huyo mwehu?

Magazeti yapo na yanafanya kazi nzuri ya kuanika kila wanapoona jipu!! Huyo anayesubiri kuuza sura kwenye tv afie huko.Ana majina na jipu ataje sasa.
Katika society watu wa aina yako wapo tu, ingawa wanapungua kwa kazi sana kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Hivi wewe unadhani kuna jipya gani ambalo halikupata kutajwa humo nyuma? Halafu unasema eti wake JF waseme wanachojua? Wewe unajua maana ya kauli ya bungeni? Na unajua faida ya kuishuhudia ukitamkwa tofauti na kuambiwa maneno yaliyotamkwa kwa dakika 15 kwa sentensi mbili gazetini?
Anyway, kwa vile ni asili yako kubisha kama ulivyotumwa ngoja nikuache
 
Umenikumbusha Mzee Sitta alivyosakamwa na wabunge wa chama chake alichofanya ni kuwapa wabunge wa upinzani uhuru wa kutosha katika kuwasilisha hoja zao hatimaye alifanikiwa kuliongoza Bunge mpaka mwisho wa kipindi chake.
 
Haya majipu yanayotumbuliwa ni coverage ya bunge LIVE? Bunge wala halipo na majipu ni mengi yametumbuliwa hakuna mbunge aliyetoa.

Kama mtu anasubiri hadi bunge lianze apewe coverage live ndio ataje anatupotezea muda na wala hatumhitaji.Jamiiforums iko hapa aweke anasubiri hadii bunge huyo mwehu?

Magazeti yapo na yanafanya kazi nzuri ya kuanika kila wanapoona jipu!! Huyo anayesubiri kuuza sura kwenye tv afie huko.Ana majina na jipu ataje sasa.

Ishu si ni gharama ya kurusha matangazo siyo, au kuna mengine mnataka kuficha kupitia bunge....."watu wasiuze sura?"

Ngoja MCC wanakuja kufadhili matangazo ya "bunge live coverage" ili tuone mtasingizia nini tena!!

Halafu bahati mbaya sana, ufadhili huo hautapitia TBC - CCM, bali kupitia TV station nyingine tu na pia kupitia special social media live streaming channels!!

Lazima sura za kina Tundu Lissu, Saed Kubenea, John Mnyika, Zitto Kabwe, Lijualikali, Sugu na wengine ziuzwe tu na kama nyie hamtaki kuzinunua, acheni sisi wengine tutanunua!!
 
Ngoja MCC wanakuja kufadhili matangazo ya "bunge live coverage" ili tuone mtasingizia nini tena!!

Halafu bahati mbaya sana, ufadhili huo hautapitia TBC - CCM, bali kupitia TV station nyingine tu na social media live streaming channels!!

Kwani ili hizo TV zirushe si lazima zipewe kibali cha kuingia ndani ya bunge kufunga mitambo yake na kuruhusiwa kurusha? Ofisi ya bunge Wakiamua kuwa telecast za yaliyojiri bungeni watapewa vyombo vyote vya habari mwishoni baada ya bunge kufanya shughuli zake za siku na ofisi ya mawasiliano ya bunge watarusha live nini?

Au wakiamua kuwa anayetaka habari za yaliyojiri bungeni awasiliane na ofisa habari wa bunge na siyo kumulika mulika watu na vi-flash vya simu bungeni hiyo live watairushia wapi?
 
Yaani awashirikishe kina Msigwa, Lema, Kubenea, Sugu etc?? Huu utani sasa. Ebu tuwage serious muda mwingine.
 
Back
Top Bottom