Rais Magufuli, sheria mbovu ya Manunuzi inapoteza fedha nyingi kuliko wafnykazi hewa, ifumue haraka

mwana wa mtemi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
374
204
Katika kuunga mkono mazuri anayofanya ya Kizalendo ni kukumbusha kuhusu sheria mbovu zinazotumiwa ovyo na watendaji wasiona na huruma kwa Watanzania.

Mojawapo ya sheria mbovu na sijui kwanini asiianzie kuifumua ni ile ya manunuzi( Procurement Act). Katika sheria hii kalamu ya shilingi 200 inanunuliwa kwa 1000 nk. Sasa hili ni jipu kubwa kwani fedha nyingi zinapotelea kwenye manunuzi na ugavi wa vitu hewa.

Kama Mtanzania anayeunga mkono juhudi za Rais aitupie haraka sheria hii ili kinachokusanywa kisitumike ovyo kwa mwavuli wa manunuzi hewa.
 
Watendaji wa Halmashauri na idara za serkali nyingi wanaitumia vibaya unapokuwa unasitisha kuendelea kwa IPTL fumua na kilichoikaribisha IPTL na uozo mwingine kupitia sheria hizi mbovu ambazo zina mianya ya kuibia serkali kupitia fedha zinazotoka hazina kwenda halmashauri na idara zingine
 
ni moja ya sheria nyonyaji na mbovu kuliko zote

naunga mkono ifumuliwe tu

haina msaada wowote kwa serikali zaidi ya wizi

hivi hawa wabunge wetu hasa wa ccm akili zao uwa wanaweka wapi kupitisha sheria mbovu kama hii??

shame

jpm tungua kama unaweza
 
ni moja ya sheria nyonyaji na mbovu kuliko zote

naunga mkono ifumuliwe tu

haina msaada wowote kwa serikali zaidi ya wizi

hivi hawa wabunge wetu hasa wa ccm akili zao uwa wanaweka wapi kupitisha sheria mbovu kama hii??

shame

jpm tungua kama unaweza
TRA watakusanya lakini zitatumika vibaya ifumuliwe
 
Alishasema ataishugulikia hii! Tunasubiria bunge lianze aanze na hiyo na mahakama ya mafisadi
 
Alishasema ataishugulikia hii! Tunasubiria bunge lianze aanze na hiyo na mahakama ya mafisadi

Kama wazalendo na wananchi wa kawaida tushiriki kumkumbushia aanze nayo bunge lijalo wizi mkubwa unafanyika kupitia sheria hii
 
Kikosi kazi kinakesha kuiondoa hiyo sheria na kuna authority ya manunuzi nayo itavunjwa! Subiri bunge lije.......wanaifumua fumua! Wadau wengi wameshirikishwa
 
Ukitaka tuwe na sheria nzuri ya manunuzi ni lazima serikali iwe na cash muda wowote inapotaka kununua bidhaa. Kwamba zabuni zinatangazwa, anatafutwa mzabuni mwenye bei na viwango bora, bidhaa zinanunuliwa, vinakaguliwa alafu mzabuni analipwa. Hapo ndo utaondoa hilo unalolisema kununua bidhaa kwa bei isiyo ya soko. Lakini kama serikali itaendelea kununua bidhaa leo na kulipa baada ya miezi 6, hilo sahau. Kuna watu wamefanya kazi na serikali na wanakuja kulipwa baada ya mwaka (refer wazabuni wanaolisha shule za serikali za bweni) sasa unafikiria yule mzabuni atatender kwa bei ya soko au atakokotoa bei kwa kuangalia na mabadiliko ya bei hapo atakapokuja kulipwa? Tufikirie kwa pamoja.
 
Sheria ya wahuni kabisa, desktop ya 1.8 m wanauza 3m. Diary ya ts elfu 7000 wao wanauza 18,000/ yaaani haifai haifaiiiii
 
nisahihi,..ila mwakyembe alisema kuwa atashughulikia ni swala la muda tu

Mwakyembe yupi....huyu wa mabehewa eki?

DSC_3493.jpg
 
Mwana wa Mtemi; unapotosha umma. Hakuna kalamu ya Shs.200 ambayo Serikali na Taasisi zake wananunua kwa Shs.1,000. Tizama tovuti ya GPSA upate bei elekezi zote kabla hujatupotosha
 
Ni ngumu sana kuuza kwa bei ya soko kama hawatalipa CASH. Itabidi waende sokoni wenyewe wakanunue hakuna mfanyabiashara atakayekubali ukae na hela yake miezi bila faida
 
Kweli hii kitu mbaya
Kimsingi lazima uuze kwa bei ya juu kwani hela ya serekali inachelewa sana inavhukuwa hata mwaka kipata.

Jiulize kwanini hata serekali imeshindwa kukiendesha vhombo chake chenyewe GPSA ambacho ndicho kinapaswa kisheria kumunua kuhifadhi na kuwazia tasisi za umma.
 
Back
Top Bottom