Rais Magufuli: Polisi fanyeni kazi yenu, hawa wanaoropoka wakamateni ili kusudi waisaidie polisi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotaka sifa za kisiasa kwa kushabikia waovu hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Rais amesema kuna watu wanashabikia maovu kwa kutoa matamko bila kuyapima madhara yake.

"Niwaombe wanasiasa wanaoshindwa kuzuia midomo yao, wanaosema kuwa hawa watu wameshikiliwa kwa muda mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu kule Marekani walikaa Guantanamo muda mrefu, katika hali hiyo kwanini usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao.

Msitufanye tukafika huko," Rais John Magufuli. "Kwanini hata siku moja mtu asijitokeze kulaani watu wanaouawa bila hatia kule. Lakini kwa kutafuta sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako ndani muda mrefu, kuna ndugu zetu wanakufa kule...nataka polisi mfanye kazi yenu, hawa wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, awe na mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni ili kusudi aisaidie polisi akiwa kule ndani," amesema Rais John Magufuli

"Juzi mtu amekamatwa na uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika na hao walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni mwa waliogiza hizo uniform za jeshi," Rais John Magufuli.

 
..wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, mkamateni ili kusudi aisaidie polisi akiwa kule ndani," amesema Rais John Magufuli.

Huu ndio udikteta wenyewe. Umkamate mtu aisaidie police ''akiwa kule ndani'' hata kama hana kosa? sheria zinasemaje kwenye kumkamata mtu na kumshikilia? hivi huyu anaelewa kweli na kuthamini utawala wa sheria?
 
Back
Top Bottom