Rais Magufuli: Nitahamia Dodoma mwaka huu, 2018

Rais Magufuli Kuhamia Dodoma Mwaka Huu

Rais John Magufuli amesema atahamia jijini Dododma kabla mwaka huu haujamalizika kama alivyoahidi serikali yake kuhamia huko.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi hati za viwanja kwa mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 30.

Amesema hadi sasa viongozi wengi wa serikali wameshahamia Dodoma akiwamo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, mawaziri na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kwamba Dar es Salaam amebaki yeye tu.

“Nimebaki mimi tu hapa. Nimepanga kabla mwaka huu haujamalizika nitahamia Dodoma, nilitaka nisihamie huko nikawaacha ndugu zangu wanaowakilisha nchi zao hapa Dar es Salaam, ndiyo mana nikahakikisha mnapata hati.

“Serikali imetoa maeneo mbalimbali jumla ya heka tano bure kwa ajili ya mabalozi, na ninyi ni mashahidi nimetoa hati hizi bila kudai chochote na mmepatiwa bila kusaini chochote, sijasema mhamie kesho, mtahamia wakati wowote mtakaotaka,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amesema, tayari viongozi wote na watumishi zaidi ya 6,000 wameshahamia hukoa ambapo pia amewatoa hofu mabalozi hao na wawakilishi wa kimataifa kuhusu usalama jijini humo.

“Tunaamini katika hatua tunazochukua mkihamia Dodoma itakuwa safi na kuhusu usalama tumehakikishiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa.

“Dodoma ni mahali pazuri na ni rahisi kwenda nchi yoyote kwa kuanzia Dodoma. Tunaboresha huduma za usafiri ikiwamo miundombinu na afya kwa Dodoma na mikoa jirani ukiwamo Singida.

“Nimeagiza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa msalato ili ndege zinazotua Dar es Salaam zitue Dodoma uanze kujengwa mara moja. Nataka niwahakikishie mabalozi Dodoma ni mahali pazuri nina uhakika patakuwa safi sana hasa baada ya ndege kutoka nchi zenu kutua hapa, tunataka kuitengeneza Tanzania mpya, yenye maendeleo na kushirikiana na sekta binafsi,” amesema.

Jiwe ni Muongo kama waongo wengine, na Ametudanganya mengi! Sina Imani naye tena kabisa!
 
Huyo mzee dodoma ataenda haraka tuu.Hivi wewe mama yako mzazi yupo icu dar unamwacha uende Dodoma?kweli kuongoza hii nchi ni kujitoa muhanga kupambana na matakataka.Huyu ndiye raisi wa ahadi na utashangaa ataenda Dodoma na ndoto ya mwalimu nyerere itatimia.

Sent using Jamii Forums mobile app
wewe mamako ulienda kumuona lini kijijini kwenu...
fanya kama unajikuna... afu sema ukonaye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani yeye daktari.
wapambe wake vichwa maji naaamini huyu jamaa anajitia kila course kasoma wakati chuo kapita mlango wa uwani......inawezekana mpaka dawa anaqapangia yeye

Sent from my TECNO K7 using Tapatalk
 
Rais Magufuli Kuhamia Dodoma Mwaka Huu

Rais John Magufuli amesema atahamia jijini Dododma kabla mwaka huu haujamalizika kama alivyoahidi serikali yake kuhamia huko.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi hati za viwanja kwa mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 30.

Amesema hadi sasa viongozi wengi wa serikali wameshahamia Dodoma akiwamo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, mawaziri na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kwamba Dar es Salaam amebaki yeye tu.

“Nimebaki mimi tu hapa. Nimepanga kabla mwaka huu haujamalizika nitahamia Dodoma, nilitaka nisihamie huko nikawaacha ndugu zangu wanaowakilisha nchi zao hapa Dar es Salaam, ndiyo mana nikahakikisha mnapata hati.

“Serikali imetoa maeneo mbalimbali jumla ya heka tano bure kwa ajili ya mabalozi, na ninyi ni mashahidi nimetoa hati hizi bila kudai chochote na mmepatiwa bila kusaini chochote, sijasema mhamie kesho, mtahamia wakati wowote mtakaotaka,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amesema, tayari viongozi wote na watumishi zaidi ya 6,000 wameshahamia hukoa ambapo pia amewatoa hofu mabalozi hao na wawakilishi wa kimataifa kuhusu usalama jijini humo.

“Tunaamini katika hatua tunazochukua mkihamia Dodoma itakuwa safi na kuhusu usalama tumehakikishiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa.

“Dodoma ni mahali pazuri na ni rahisi kwenda nchi yoyote kwa kuanzia Dodoma. Tunaboresha huduma za usafiri ikiwamo miundombinu na afya kwa Dodoma na mikoa jirani ukiwamo Singida.

“Nimeagiza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa msalato ili ndege zinazotua Dar es Salaam zitue Dodoma uanze kujengwa mara moja. Nataka niwahakikishie mabalozi Dodoma ni mahali pazuri nina uhakika patakuwa safi sana hasa baada ya ndege kutoka nchi zenu kutua hapa, tunataka kuitengeneza Tanzania mpya, yenye maendeleo na kushirikiana na sekta binafsi,” amesema.
...pipo yuzi tu dai... in.. in... ineeee View attachment pipo yuz tu dai.mp4View attachment sitatoa hela za katiba.mp4
FB_IMG_1546338668690.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa rais, nakukumbusha tu kwamba una siku nne tu zimebaki utimize ahadi yako ya kuhamia Dodoma. Tafadhali , usimsahau kipenzi chako Bashite. Nakushauri pia ukihamia Dodoma uhamie kwelikweli, sio kila leo kiguu na njia kurudi Dar. Sisi wananchi unaopenda kutuita wanyonge hatupo tayari kubeba gharama hizo. Labda mtumie mishahara yenu mkitaka kueudi Dar kujivinjari. Ni hayo tu Mh na Mrukufu sana Rais.
Note this ---Hakuna kiumbe Muongo kama jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hao waliohamia Dodoma misele ya Dar kila weekend haikauki. Afanye mpango ahamie huko haraka ndani ya hii 2019
 
Huyu ndiye raisi wa ahadi na utashangaa ataenda Dodoma na ndoto ya mwalimu nyerere itatimia.
Mwalimu hakuwa na ndoto ya kuhamia Dodoma na hata wazo la kuhamia Dodoma hakulitoa yeye. Tafuteni Historia sahihi ya nchi hii mtaelewa ukweli ulivyo.

Kama kuhamia Dodomna ndiyo ingekuwa ndoto ya Mwalimu angekuha ameshahamia zamani sana kabla hata ya vita ya Kagera kutokea.
 
Back
Top Bottom