Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,118
Anatala kuhama na bahari aende nayo DodomaKama mzee-baba aliropoka tu, hii ngoma inakwenda kumpasukia kichwani. Atanangwa na kuzodolewa sana. Amezoea kukurupuka?
Wenzie wametangulia Dodoma yeye bado anangojea nini Dar?
Mtukufu kuhama Dar ni kama hataki tena lakini njia rahisi ya yy kuhama Dsm ni kuwambia Marekani na ulaya watume Nyambizi zije baharini chini kwa chini zimchungulie zipige picha kisha wamtumie kwenye Whatsapp yake akiona picha za kijasusi toka baharini kesho yake atahama haraka sana tena kwa speed ya ajabu kweli kinyume na hapo hawezi kuhamia Dodoma ataendelea kuvuta harufu ya samaki wa Feri.Mheshimiwa rais, nakukumbusha tu kwamba una siku nne tu zimebaki utimize ahadi yako ya kuhamia Dodoma. Tafadhali , usimsahau kipenzi chako Bashite. Nakushauri pia ukihamia Dodoma uhamie kwelikweli, sio kila leo kiguu na njia kurudi Dar. Sisi wananchi unaopenda kutuita wanyonge hatupo tayari kubeba gharama hizo. Labda mtumie mishahara yenu mkitaka kueudi Dar kujivinjari. Ni hayo tu Mh na Mrukufu sana Rais.
Anangojea kuchunguliwa na nyambizi za Marekani toka baharini usikuKama mzee-baba aliropoka tu, hii ngoma inakwenda kumpasukia kichwani. Atanangwa na kuzodolewa sana. Amezoea kukurupuka?
Wenzie wametangulia Dodoma yeye bado anangojea nini Dar?
Atasema anahujumiwa na mabeberu ili asihamie Dodoma
Ni hatari sana kwa Rais kutoa ahadi ya Uongo na endapo hatahamia Dodoma 2018 ajue ahadi yake itakuwa feki na huenda wananchi wakaanza kukariri Uongo toka kwake na kuwa kisingizioZimebaki siku 4 tu kwa mtu muongo kudhihirika uongo wake mwingine
Ah ah ah mshamkumbusha,itakua breaking news atahamia before 2019
DAR itabaki kuwa dar, mtu ni bora apange chumba kimoja na mke na watoto watatu ila akae dar, bora nishindie mihogo na miguu ya kuku na maji ya kandoro ila nikae dar. KWELI DAR ITABAKI KILELENI(in piere voice).
Asipohamia ujue msemo mpya na msamiati mpya unakuja yaani neno Dodoma litatumika ka ahadi ya Uongo, mfano utasikia jamaa akisema yule jamaa ni muongo sana akiwa na maana jamaa ni mdodoma sana, neno Mdodoma litasimama kama Ahadi feki ahadi ya Uongo yaani Udodoma maana yake ni Uongo kuanzia leo endapo mtukufu malaika toka chato hataenda Dodoma kabla ya 2019
Cha kumfanya hakuna zaidi ya kucopy Uongo wake na kuwa ni Uongo wa kitaifa na kimataifa na pia neno Uongo litaitwa Udodoma, yaani ukipiga watu fix wanasema jamaa ana Udodoma hatari agome tu na kusaidia kuleta misamiati mipya.Amegoma sasa, kwani mtafanya nini?
Wacha udodoma mkuu. Yote haya ya nini?
Huu utakua uongo wake wa 4. 1 Sukari kua 5,000 kwa kilo, 2. Milioni 50 kila kijiji, 3. Kujenga SGR kwa fedha za ndani, 4. Kuhamia DodomaNi hatari sana kwa Rais kutoa ahadi ya Uongo na endapo hatahamia Dodoma 2018 ajue ahadi yake itakuwa feki na huenda wananchi wakaanza kukariri Uongo toka kwake na kuwa kisingizio
[emoji848] [emoji848] Nimewaza kitu ila naamini kitakuwa vile nilivyowaza.