introvert
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 1,372
- 2,416
Naona nikuongezee kuhusu kipande hicho cha maelezo. Unajua kwa nini makandarasi wanaweka bei zao juu wanapokuwa wanachukuwa kazi za serikali? Huwa wanajitahidi kujilinda na ucheleweshaji huo. Ndiyo maana nikahisi unazungumzia pesa ya familia yako. Pesa ya serikali huwezi kuiweka kwenye kinga za kizembe na zenye mianya ya upotevu kiasi hicho.
Labda hutaki kuelewa na unabisha tu.
Hizo kinga (hedging) zinatumiwa na makampuni na mashirika yote duniani. Si jambo jipya.
Kuliko ukalie 26 au 37 billion cash kwenye current account ni bora uweke kwenye fixed deposit account. Hata rate ya 1% itakuarudishia pesa nzuri 0.26 au 0.37 billion ambayo utafanyia mambo mengine.
Upotevu ni hisia zako lakini mpaka sasa ni wakurugenzi wangapi wamekamatwa wameiba riba? Hao waliofukuzwa wameiba?
Ujenzi wa madarasa kwa mfano utachukua zaidi ya miezi mitatu mpaka uanze kufanya malipo na malipo ni mpaka uhakiki utekelezaji wa kazi na bado kuna 20% retention fee. Kwa nini uweke hiyo pesa current account?
Ucheleweshaji unaoongelea ni serikalini, serikali za kuu na serikali za mitaa na hii inasababishwa na ucheleweshaji wa fedha kutoka hazina. Usichanganye mambo.