Rais Magufuli: Niliivunja Bodi ya TRA baada ya kuidhinisha mabilioni ya pesa kwenda benki binafsi

sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
618
1,816
JPM+PICHA.jpg

Novemba 20 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu na kuivunja hiyo bila kueleza sababu zozote.

Rais John Magufuli ameeleza sababu za kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuwa ilitokana na bodi hiyo kuidhinisha mamlaka hiyo kuweka mabilioni ya fedha kwenye benki binafsi

Novemba 20 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu na kuivunja hiyo bila kueleza sababu zozote.

Akizungumza leo wakati wa sherehe za mahafali ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani, Rais Magufuli amesema kuwa TRA walichukuwa fedha mabilioni na kuweka fixed account benki 8 binafsi na bodi ikaidhinisha.

Chanzo: Mwananchi
Video
 
Source:
Mwananchi

watu hawaogopi
 
Kwani ni makosa kuweka pesa kwenye bank binafisi?.....

Na kama ni makosa kwanini waziri Wa fedha, katibu mkuu wizara ya fedha, Kamishina TRA,na Gavana Wa Bank kuu wote wameachwa bila kuondolewa wakati ni wajumbe Wa Bodi ya TRA?

Tatizo la wanasiasa kubishana na wachumi ........

Pesa kuwekwa bank binafisi sio kosa zinarudi mtaani kwenye mzunguko....

Ndio maana unaona hali ya uchumi ni tete.....

Tengeneza mfumo uliowazi Wa kuzifanyia auditing pesa za umma zilizo kwenye bank binafsi ili kukwepa udanganyifu sio kuzifungia kwenye makabati ya BOT.......

Kama magufuli unataka kufanikiwa acha kubishana na wachumi....
 
Novemba 20 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu na kuivunja hiyo bila kueleza sababu zozote.

Rais John Magufuli ameeleza sababu za kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuwa ilitokana na bodi hiyo kuidhinisha mamlaka hiyo kuweka mabilioni ya fedha kwenye benki binafsi

Novemba 20 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu na kuivunja hiyo bila kueleza sababu zozote.

Akizungumza leo wakati wa sherehe za mahafali ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani, Rais Magufuli amesema kuwa TRA walichukuwa fedha mabilioni na kuweka fixed account benki 8 binafsi na bodi ikaidhinisha.
Source: Mwananchi

Sasa adhabu yake ni kufukuza bodi, si mnakaa mnaongea, wanakupa sababu. Kama kuna sheria yoyote wamevunja inaweza kuwa ok lakini nadhani bado sio kigezo cha kufukuzwa especially kama performance yao ni nzuri.
 
Kwahiyo huo uamuzi ulihusisha baadhi tu ya wajumbe wa bodi ndio maana wengine wanaendelea na nafasi zao?

Hiyo akaunti walifungua kwa siri?

Kama walifungua kwa siri inakuwaje Gavana, Kamishana Mkuu wa TRA,Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar ambao ni wajumbe wa Bodi ya TRA wanaendelea na nyazifa zao?
 
Kwa hilo namuunga mkono Magufuri.

Atimue hata hao wakurugenzi wa fedha wa TRA, lakini sielewi Kidata nae hakujua kua Magu hataki pesa ya Serikali kuwekwa kwenye benk binafsi kama fixed deposit?

Benk za bongo zilizoea kujiendesha kimagumashi kwa kuhonga bodi za wakurugenzi na wakurugenzi wa mashirika ya umma waweke fixed deposit kwenye benk zao na hiyo riba ndio ilikua chakula ya hizo bodi na wakurugenzi.

kwa hili la serikali kuhamishia pesa zake zote BOT naiunga mkono asilimia 100.
 
Kwani ni makosa kuweka pesa kwenye benk binafisi?.....

Tatizo la wanasiasa kubishana na wachumi ........

Pesa kuwekwa benk binafisi sio kosa zinarudi mtaani kwenye mzunguko....

Ndio maana unaona hali ya uchumi ni tete.....

Kama magufuli unataka kufanikiwa acha kubishana na wachumi....
Unaongea pumba mno huo uchumi na finance unayoizungumzia huijui
 
Hivyo hivyo lazima waelewe kuwa tunataka asiwepo kiumbe wa kushindana na serikali kimapato, kuna watu waliwahi kusema "Kama serikali hawana pesa basi tuwakopeshe " kwa utaratibu huu, wote lazima tuiabudu serikali hii vinginevyo vipindi vya mapishi radioni na kwenye television watu tutafundishwa kupika ugali wa dona na mlenda, haya masuala sijui mahanjumati, kwisha habari yake! Nipo njiani nahamia kenya!
 
Serikali hii inajikaanga kwa mafuta yake yenyewe.

Ni wazi hawa wataalamu wameshaona hali ni mbaya na sasa wanajaribu kuweka mikakati ya muda mfupi na mrefu ili kuokoa uchumi lakini Raisi anawaingilia.

Nina hakika wangekuwa wamefungua akaunti hii kwa siri na kwa nia mbia sababu hii ya kuwafukuza ingewekwa hadharai siku ile ile bodi inavunjwa.

Hapa kwa wananchi wasioelewa wanaweza kuaminishwa kuwa walifungua hizo akaunti ili wapige hela na hawataki kufafanua ili mtukufu apate sifa za kisiasa kuwa kafukuza mafisadi kumbe sio.
 
Serikali itangaze rasmi kuvunja uhusiano na sekta binafsi na itangaze uadui rasmi.

Haiwezekani upande mmoja una mizizi ya kuichukia na kutoiamini sekta binafsi na kuwaona kama wezi.
Kama Private sector hawatatoa concern,muda si mrefu hata tenda za serikali zitafanywa na serikali.

Naona kuna mvutano,tutafikia mahali matangazo ya serikali yatatolewa na habari leo na daily news,sio star tv,jamhuri(mpaka manyerere kaomba matangazo ikulu)

Nafikiri sekta binafsi wakae na kuangalia jinsi ya ku react,either wahamie nchi jirani au na wao waubane uchumi usishuke kwa.mtu wa chini
 
Back
Top Bottom