Ahsante sana kwa comment yako mazee. "Nayasapoti" maelezo yako kwa kuwa, kama ni kulinganisha tawala zote kwenye mizani, tangia R.i.p "Mchonga" hadi leo hii, Magufuli yupo juu.
Nyerere aliwagwaya wahujumu uchumi, hadi akakodi waziri mkuu R.i.p Sokoine kumwadhibia mafisadi hao. Alikuwa akitaka kutumbua waziri,ama aliyemkera,ilikuwa lazima asafiri nje ya Dar ama nje ya nchi kwenda kutoa tamko. Alikuwa hana ubavu wa kuua nyani kwa kumwangalia Usoni.
Awamu ya pili ni awamu ya mageuzi na mabadiliko. Ingetawala miaka 20 ingejipembua vizuri kiuchumi tukaithamanisha. Lakini miaka 10 haikuwatosha ku-"reshape" "gorvernment".
Ikaacha mizizi ya rukhsa ya 'Chukua chako mapema' inakomaa.
Wahujumu wakajiimarisha na kuanza kukatia rufaa kesi za uhujumu zilizowatia ndani enzi za awamu ya1, kuhalalisha uporaji wao.
Awamu ya3 ni awamu ya ukweli na uwazi wa uporaji uliotamalaki. Mheshimiwa alijitahidi kujenga uchumi imara, lakini hakuweza kudhibiti "mibaka uchumi".
Vurugu za 10% kwa mikataba ya hovyo hovyo ya kufukarisha nchi zilianzia hapo.
Awamu ya4 ilibeba sura zilezile za awamu ya3 kina Vijisenti na wapigaji wenzie kina Mramba na wengine kibao, waliolisha nyasi watu, kwa ajili ya kununua ndege ya mtukufu Che Nkapa na rada za mitumba. Ulitegenea nini kubaki na sura kama hizo kwenye utawala wako?
Lilaumiwe genge au ulaumiwe wewe uliyewachagua?
Eebw eeh! Mag kama ataendelea kuadhibia hilo rungu lake la plastiki isiyokatika na kuuwa nyani huku akimwangalia usoni,
wallah,asikwambie mtu,lazima tutafika.
Wengine hatuna kadi wala ushabiki wa vyama, lakini anatufariji sana kwa utendaji wake. Na ndiye raisi wa aina tuliyokuwa tunaitaka.