Rais Magufuli ni mchochezi

Rais Magufuli ni mchochezi

Mkuu wa mkoa kada wilaya kada tarafa kada unategemea nini kwani hata kama makonda angepandishwa huo ukada alafu akapangiwa kwingine hao wabaya wake wasinge jua kapandishwa cheo cha ukuda zaid?
Mkuu point anazo Sema tu amesimama upande usio upenda.
 
Dk. Lwaitama ni UKAWA, unategemea azungumze nini kwa Mh. Magufuli; amsifie?
 
RAIS John Magufuli anatajwa kuwa ni rais mchochezi na anayefanya mambo yake ili kuonesha anaendesha mapambano dhidi ya wapinzani wake, anaandika

Happyness Lidwino.

Dk. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, yapo baadhi ya mambo ambayo Rais Magufuli amekuwa akiyafanya ili kukomoa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Mfano, siku chache baada ya kumteua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliongea kauli tata akaendelea na kauli hizo tata.
“Kuteuliwa kwa Makonda inatafsiri mpambano utakaokuwepo baina ya Meya mpya na yeye (Makonda) kwa kuwa, wanaoteuliwa na rais siku zote huwa wanajiona kuwa juu,” amesema Dk. Lwaitama.
“Hata Makonda nimemuacha Dar es Salaam ili wabaya wake wamuone akipanda cheo, wenye chuki wajinyonge zaidi,” amenukuliwa Rais Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi namba mbili.
Amesema Dk. Lwaitama, Rais Magufuli anatakiwa kufanya kazi bila upendeleo kwa kuwa lengo ni kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.
Dk. Lwaitama anasema hayo wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikilitumbikiza taifa kwenye sintofahamu ya kisiasa na kwamba, ni wakati wa wananchi kukataa utumwa,
Dk. Lwaitama anasema, wananachi wanapaswa kuondoka kwenye minyororo ya utumwa na kusimama katika kuhakikisha wanapigania haki pale inapoonekana kupokwa na watawala.
Anatoleo mfano ushindi wa vyama vinavyoundwana ukawa kuchukua Umeya wa Jiji la Dar es Salaam ambapo ndio Mji Mkuu wa Kibiashara Tanzania na kwamba, hatua hiyo inaanza kufungua minyororo.
“Wananchi wanatakiwa kujiandaa kimabadiliko na kuukataa utumwa kwani kwa muda mrefu walikuwa utumwani kwa kuongozwa na chama kimoja,” anasema Dk. Lwaitama.
Anasema, wananchi wa Dar es Salaam amekuwa wakijiuliza sababu za kughairishwa uchaguzi huo mara kwa mara “yote hii ni kwa sababu CCM inang’ang’ania madaraka.”
Akizungumza na mtandao huu leo Dk. Lwaitama anasema jeuri ya watawala wa nchi hii inatokana na ubovu wa Katiba na kwamba, udhaifu huo unakwenda mbali ikiwa ni pamoja na kuteua viongozi wabovu.
Miongoni mwa viongozi anaowaona kutokuwa na mantiki ya kuwepo kwao licha ya rais kuwa na mamlaka ya kuwateua ni pamoja na Wakuu wa Mikoa.
“Binafsi sioni kama kunahaja ya kuwa na wakuu wa mikoa wala wakuu wa wilaya kwani hao wanaonekana kuwepo kwa ajili ya kujitengenezea ulaji tu.
“Lakini kazi kubwa inatakiwa ifanywe na Meya wa Jiji ambaye ni mchaguliwa wa wananchi kwa kupitia madiwani.”
Dk. Lwaitama anasema, “Inatakiwa tukubali kurudi katika Katiba ya Warioba ili kuondoa mfumo huu wa kuwa na viongozi wengi ndani ya mkoa mmoja.
“Tunatakiwa kubaki na Mkurugenzi wa Jiji na Meya wa jiji tu ambaye amebeba ndoto za wananchi na sio Mkuu wa Mkoa ambaye ameteuliwa tu.”
Rais lazima awe mkweli na huo ukweli wa JPM naona inawaumiza sana wengine. Sasa, asiyependa ya JPM ajue kwa sasa hana namna mpaka 2020. Kama kweli, JPM hawatendei haki wananchi tutajua then ila kwa sasa you should take back seat and enjoy the ride.
 
magufuli ni mnafiki mkubwa. kama kweli amelenga kubana matumizi ya serikali kwanini aendelee kuwa na wakuu wa mikoa, wilaya na tarafa wanaotumia matrilioni ya fedha za umma bila sababu za msingi?
Hivi Rais anaongoza nchi kwa kutumia nini? Atakavyoamka siku hiyo au ushauri wa mke wake?
Mlikimbia bunge maalum la katiba,Magu afanyeje?
 
RAIS John Magufuli anatajwa kuwa ni rais mchochezi na anayefanya mambo yake ili kuonesha anaendesha mapambano dhidi ya wapinzani wake,

------

Dk. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, yapo baadhi ya mambo ambayo Rais Magufuli amekuwa akiyafanya ili kukomoa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Mfano, siku chache baada ya kumteua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliongea kauli tata akaendelea na kauli hizo tata.

“Kuteuliwa kwa Makonda inatafsiri mpambano utakaokuwepo baina ya Meya mpya na yeye (Makonda) kwa kuwa, wanaoteuliwa na rais siku zote huwa wanajiona kuwa juu,” amesema Dk. Lwaitama.

“Hata Makonda nimemuacha Dar es Salaam ili wabaya wake wamuone akipanda cheo, wenye chuki wajinyonge zaidi,” amenukuliwa Rais Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi namba mbili.

Amesema Dk. Lwaitama, Rais Magufuli anatakiwa kufanya kazi bila upendeleo kwa kuwa lengo ni kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.

Dk. Lwaitama anasema hayo wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikilitumbikiza taifa kwenye sintofahamu ya kisiasa na kwamba, ni wakati wa wananchi kukataa utumwa.

Dk. Lwaitama anasema, wananachi wanapaswa kuondoka kwenye minyororo ya utumwa na kusimama katika kuhakikisha wanapigania haki pale inapoonekana kupokwa na watawala.

Anatoleo mfano ushindi wa vyama vinavyoundwana ukawa kuchukua Umeya wa Jiji la Dar es Salaam ambapo ndio Mji Mkuu wa Kibiashara Tanzania na kwamba, hatua hiyo inaanza kufungua minyororo.

“Wananchi wanatakiwa kujiandaa kimabadiliko na kuukataa utumwa kwani kwa muda mrefu walikuwa utumwani kwa kuongozwa na chama kimoja,” anasema Dk. Lwaitama.

Anasema, wananchi wa Dar es Salaam amekuwa wakijiuliza sababu za kughairishwa uchaguzi huo mara kwa mara “yote hii ni kwa sababu CCM inang’ang’ania madaraka.”

Akizungumza na mtandao huu leo Dk. Lwaitama anasema jeuri ya watawala wa nchi hii inatokana na ubovu wa Katiba na kwamba, udhaifu huo unakwenda mbali ikiwa ni pamoja na kuteua viongozi wabovu.

Miongoni mwa viongozi anaowaona kutokuwa na mantiki ya kuwepo kwao licha ya rais kuwa na mamlaka ya kuwateua ni pamoja na Wakuu wa Mikoa.

“Binafsi sioni kama kunahaja ya kuwa na wakuu wa mikoa wala wakuu wa wilaya kwani hao wanaonekana kuwepo kwa ajili ya kujitengenezea ulaji tu.

“Lakini kazi kubwa inatakiwa ifanywe na Meya wa Jiji ambaye ni mchaguliwa wa wananchi kwa kupitia madiwani.”

Dk. Lwaitama anasema, “Inatakiwa tukubali kurudi katika Katiba ya Warioba ili kuondoa mfumo huu wa kuwa na viongozi wengi ndani ya mkoa mmoja.

“Tunatakiwa kubaki na Mkurugenzi wa Jiji na Meya wa jiji tu ambaye amebeba ndoto za wananchi na sio Mkuu wa Mkoa ambaye ameteuliwa tu.”

Lwaitama bado yupo tu, haya mwache aendelee kuzunguusha mikono
 
hii ni kweli kabisa. huu mfumo wa kuwa na makada chungu nzima wanaoteuliwa kuwa wakuu wa tarafa, wilaya na mikoa kiulaji unapaswa kukoma. ndio maana CCM wanang'ang!ania mfumo huo ili waendelee kuifilisi nchi kwa manufaa yao binafsi.

Hata wakurugenzi walitakiwa waajiriwe na Halimashauri za miji badala ya kuteuliwa na Rais. Hizi teuzi za Rais kwenye nchi kubwa kama Tanzania ya watu million 45 Ni lazima kujuana au upendeleo utakuwepo!!
 
Rais lazima awe mkweli na huo ukweli wa JPM naona inawaumiza sana wengine. Sasa, asiyependa ya JPM ajue kwa sasa hana namna mpaka 2020. Kama kweli, JPM hawatendei haki wananchi tutajua then ila kwa sasa you should take back seat and enjoy the ride.
Maigizo Serekali ya Tv na Magazeti
 
hii ni kweli kabisa. huu mfumo wa kuwa na makada chungu nzima wanaoteuliwa kuwa wakuu wa tarafa, wilaya na mikoa kiulaji unapaswa kukoma. ndio maana CCM wanang'ang!ania mfumo huo ili waendelee kuifilisi nchi kwa manufaa yao binafsi.
Na wewe usiye na kazi huifilisi nchi
 
Hata wakurugenzi walitakiwa waajiriwe na Halimashauri za miji badala ya kuteuliwa na Rais. Hizi teuzi za Rais kwenye nchi kubwa kama Tanzania ya watu million 45 Ni lazima kujuana au upendeleo utakuwepo!!
Ndio kulindana na Ukada ukada huko huko ndani
 
Hiki kilwaitama sijui kwanini huwa nikikiona natamani kukizabua vibao.
Yaani hakinaga point,halafu eti nasikia ni mwalimu wa chuo kikuu,no wonder degree fake zimezidi mitaani
weh weh weh weh! huyu sijui ndo lwainini sijui huwa anatwangana vibaoo na matusi juu, ohoo....waulize mwanza airport!!
 
Mkuu wa nchi anatakiwa awe na staha ktk uongeaji.Maneno ya mipasho si haki yake kwa wadhifa alio nao.
 
Mleta mada badilisha kichwa cha habari, neno mchochezi lina maana mbaya. Ni neno kali sana. Nakushauri kwa nia njema sana, unayemzungumzia ni mkuu wa nchi, tafuta neno lisilo na makali kama hili la "uchochezi". Jaribu kuifahamu sanaa ya maongezi ya jamii. Be careful my good friend.
 
Profeseri lipi jema unalolitaka Yale yote ulokuwa ukiyasema hadi kujipa likizo ya Uanachama si ndiyo haya anayofanya yule aishie na kutenda anayoyasema naye ni Mh. Raisi JPM.Wewe tuambie wimbo mpya wa Albamu yako ya sasa
 
Back
Top Bottom