Rais Magufuli ni mchochezi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
RAIS John Magufuli anatajwa kuwa ni rais mchochezi na anayefanya mambo yake ili kuonesha anaendesha mapambano dhidi ya wapinzani wake,

------

Dk. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, yapo baadhi ya mambo ambayo Rais Magufuli amekuwa akiyafanya ili kukomoa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Mfano, siku chache baada ya kumteua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliongea kauli tata akaendelea na kauli hizo tata.

“Kuteuliwa kwa Makonda inatafsiri mpambano utakaokuwepo baina ya Meya mpya na yeye (Makonda) kwa kuwa, wanaoteuliwa na rais siku zote huwa wanajiona kuwa juu,” amesema Dk. Lwaitama.

“Hata Makonda nimemuacha Dar es Salaam ili wabaya wake wamuone akipanda cheo, wenye chuki wajinyonge zaidi,” amenukuliwa Rais Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi namba mbili.

Amesema Dk. Lwaitama, Rais Magufuli anatakiwa kufanya kazi bila upendeleo kwa kuwa lengo ni kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.

Dk. Lwaitama anasema hayo wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikilitumbikiza taifa kwenye sintofahamu ya kisiasa na kwamba, ni wakati wa wananchi kukataa utumwa.

Dk. Lwaitama anasema, wananachi wanapaswa kuondoka kwenye minyororo ya utumwa na kusimama katika kuhakikisha wanapigania haki pale inapoonekana kupokwa na watawala.

Anatoleo mfano ushindi wa vyama vinavyoundwana ukawa kuchukua Umeya wa Jiji la Dar es Salaam ambapo ndio Mji Mkuu wa Kibiashara Tanzania na kwamba, hatua hiyo inaanza kufungua minyororo.

“Wananchi wanatakiwa kujiandaa kimabadiliko na kuukataa utumwa kwani kwa muda mrefu walikuwa utumwani kwa kuongozwa na chama kimoja,” anasema Dk. Lwaitama.

Anasema, wananchi wa Dar es Salaam amekuwa wakijiuliza sababu za kughairishwa uchaguzi huo mara kwa mara “yote hii ni kwa sababu CCM inang’ang’ania madaraka.”

Akizungumza na mtandao huu leo Dk. Lwaitama anasema jeuri ya watawala wa nchi hii inatokana na ubovu wa Katiba na kwamba, udhaifu huo unakwenda mbali ikiwa ni pamoja na kuteua viongozi wabovu.

Miongoni mwa viongozi anaowaona kutokuwa na mantiki ya kuwepo kwao licha ya rais kuwa na mamlaka ya kuwateua ni pamoja na Wakuu wa Mikoa.

“Binafsi sioni kama kunahaja ya kuwa na wakuu wa mikoa wala wakuu wa wilaya kwani hao wanaonekana kuwepo kwa ajili ya kujitengenezea ulaji tu.

“Lakini kazi kubwa inatakiwa ifanywe na Meya wa Jiji ambaye ni mchaguliwa wa wananchi kwa kupitia madiwani.”

Dk. Lwaitama anasema, “Inatakiwa tukubali kurudi katika Katiba ya Warioba ili kuondoa mfumo huu wa kuwa na viongozi wengi ndani ya mkoa mmoja.

“Tunatakiwa kubaki na Mkurugenzi wa Jiji na Meya wa jiji tu ambaye amebeba ndoto za wananchi na sio Mkuu wa Mkoa ambaye ameteuliwa tu.”
 
hii ni kweli kabisa. huu mfumo wa kuwa na makada chungu nzima wanaoteuliwa kuwa wakuu wa tarafa, wilaya na mikoa kiulaji unapaswa kukoma. ndio maana CCM wanang'ang!ania mfumo huo ili waendelee kuifilisi nchi kwa manufaa yao binafsi.
 
Wanatia aibu sana
 
Poleni sana. Magufuli hakopeshi. Anakutwanga mchana kweupe
magufuli ni mnafiki mkubwa. kama kweli amelenga kubana matumizi ya serikali kwanini aendelee kuwa na wakuu wa mikoa, wilaya na tarafa wanaotumia matrilioni ya fedha za umma bila sababu za msingi?
 
Hiki kilwaitama sijui kwanini huwa nikikiona natamani kukizabua vibao.
Yaani hakinaga point,halafu eti nasikia ni mwalimu wa chuo kikuu,no wonder degree fake zimezidi mitaani
 
Muda wa kampeni umeisha. Sasa hivi ni kazi tu.

Atulie sindano zimuingie vizuri.
 
Mkuu wa mkoa kada wilaya kada tarafa kada unategemea nini kwani hata kama makonda angepandishwa huo ukada alafu akapangiwa kwingine hao wabaya wake wasinge jua kapandishwa cheo cha ukuda zaid?
 
Hiki kilwaitama sijui kwanini huwa nikikiona natamani kukizabua vibao.
Yaani hakinaga point,halafu eti nasikia ni mwalimu wa chuo kikuu,no wonder degree fake zimezidi mitaani

Anaongeaga hadi mate yanamtoka halafu points hana.
 
Hiki kilwaitama sijui kwanini huwa nikikiona natamani kukizabua vibao.
Yaani hakinaga point,halafu eti nasikia ni mwalimu wa chuo kikuu,no wonder degree fake zimezidi mitaani
Kwa hyo unakili kwamba maprofesa wetu nifeki?Maana mwenye vyeti vyeki anazalisha mwanafunzi feki ?
 
Magufuli ni Msukuma, sijui Msonjo (anayejua kabila lake arekebishe nafsini mwake) lakini ni bingwa wa mipasho zaidi ya Mswahili, JK.
 
mkuu mdudu halisi magufuli kabila lake siyo msukuma yule ni mccm.Maana kule ccm ndo kwao na akina khadja kopa mzee yusufu
 
Hiki kilwaitama sijui kwanini huwa nikikiona natamani kukizabua vibao.
Yaani hakinaga point,halafu eti nasikia ni mwalimu wa chuo kikuu,no wonder degree fake zimezidi mitaani
Pole pole tu huna haja ya kuongea na mate kinywani una tutemea,huyu ni profesa makini sana, akipiga ana lenga target kama lime kufika pole na stahamili tu yatapita,vibao gani vya mbuzi?
 
Anaongeaga hadi mate yanamtoka halafu points hana.
Kama hana Points wewe huwa unamsikilizaga wa nini?...tuwe na tabia za wazungu hulipendi jambo unaliweka kando unashughulika na mengine...mtu humpendi ila bado unamfuatilia hii inaonesha kuwa unashughulika na uwepo wake.
Dr Lwaitama ni mmoja kati ya watu walioenda Chuoni kutafuta Elimu na sio kushangaa majengo tu.
 
Hiki kilwaitama si jui kwanini huwa nikikiona natamani kukizabua vibao.
Yaani hakinaga point,halafu eti nasikia ni mwalimu wa chuo kikuu,no wonder degree fake zimezidi mitaani
We utakuwa mwanasiasa kindakindaki ulielewa maji ya bendela kijani. Au mteule wa mkuu. Dr. kagonga ikulu enhee...... lazima iume
 
Back
Top Bottom