Rais Magufuli ndiye kinara wa mageuzi Barani Afrika

Tao

Member
Nov 10, 2018
95
157
Kutokana na mafanikio makubwa katika kufufua viwanda,ujenzi wa miundombinu,uboreshaji wa sekta ya utumishi wa umma,mapambano dhidi ya umaskini na rushwa ,sheria mpya katika mikataba ya madini,mpango wa elimu bure na ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea nchi nzima pamoja na mradi wa umeme vijijini, Rais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli hakika ndiye kinara wa mageuzi barani Afrika.

Rais mstaafu wa Botswana Ian Khama wa Botswana naye amekuwa akitajwatajwa kama mwanamageuzi lakini kwa kufanya mambo mengi kwa wananchi wake ndani ya muda mfupi ni dhahiri JPM hana mfano wake hapa Afrika.

Uthubutu huu wa JPM ni lazima uungwe mkono na Waafrika wote kwani Bara hili limekuwa kichwa cha mwendawazimu kutokana na sababu kadhaa na mojawapo ni ukosefu wa uongozi bora.

Natambua kuwa mageuzi makubwa huja na changamoto zake,muhimu ni kila mmoja wetu kutambua kazi inayofanyika na hivyo kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake.

Ukitazama kwa jicho la kizalendo utaona kabisa kuwa chini ya uongozi wa Jemedari huyu tutakuwa yaifa lenye uchumi wa kati kufikia 2025.

Nimekuwa nikijiuliza mafanikio haya ya JPM yanasababishwa na nini,hatahivyo natambua kuwa Ngosha huyu ni jasiri,ana maono,ni mzalendo,ana upendo kwa Watanzania na ni mcha Mungu.

Tuendelee kumuunga mkono
Tuendelee kumsaidia na kumuombea.

Bado natafakari mafanikio haya ya JPM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mabadiliko ya kweli kabisa ambayo ni ndoto ya kila mtanzania yanafanyika kipindi hiki cha JPM ila kwa baadhi kwa kutambua au kutotambua wanamkwamisha
 
Kutokana na mafanikio makubwa katika kufufua viwanda,ujenzi wa miundombinu,uboreshaji wa sekta ya utumishi wa umma,mapambano dhidi ya umaskini na rushwa ,sheria mpya katika mikataba ya madini,mpango wa elimu bure na ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea nchi nzima pamoja na mradi wa umeme vijijini, Rais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli hakika ndiye kinara wa mageuzi barani Afrika.

Rais mstaafu wa Botswana Ian Khama wa Botswana naye amekuwa akitajwatajwa kama mwanamageuzi lakini kwa kufanya mambo mengi kwa wananchi wake ndani ya muda mfupi ni dhahiri JPM hana mfano wake hapa Afrika.

Uthubutu huu wa JPM ni lazima uungwe mkono na Waafrika wote kwani Bara hili limekuwa kichwa cha mwendawazimu kutokana na sababu kadhaa na mojawapo ni ukosefu wa uongozi bora.

Natambua kuwa mageuzi makubwa huja na changamoto zake,muhimu ni kila mmoja wetu kutambua kazi inayofanyika na hivyo kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake.

Ukitazama kwa jicho la kizalendo utaona kabisa kuwa chini ya uongozi wa Jemedari huyu tutakuwa yaifa lenye uchumi wa kati kufikia 2025.

Nimekuwa nikijiuliza mafanikio haya ya JPM yanasababishwa na nini,hatahivyo natambua kuwa Ngosha huyu ni jasiri,ana maono,ni mzalendo,ana upendo kwa Watanzania na ni mcha Mungu.

Tuendelee kumuunga mkono
Tuendelee kumsaidia na kumuombea.

Bado natafakari mafanikio haya ya JPM.

Sent using Jamii Forums mobile app
Namba ya Simu tafadhali, usiwe unasahau jambo hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom