Rais Magufuli, nchi zilizoendelea zilianza na Mapinduzi ya Kilimo sio Viwanda

Rais hajui maisha ya wanainchi anaowaongoza,yaani hajui wanaishije na ndo maana kumsikia akiongelea ustawi wa jamii kwake ni vigumu mno. Is too harshness.
 
Ngoja tujenge viwanda vya mbolea, kusindika mazao ndio Iwe msingi kwa wakulima kunufaika '' ''':'#pembejeo zatutesa sana kisa viwanda vichache
 
Mi nadhani viwanda kwanza ndio kwenye kilimo kwa sababu utahitaji viwanda kutengenezea Machines zitakazotumika kwenye kilimo, utakuwaje na mechanized agriculture bila viwanda kwanza viwanda ndio ndio utengeneze baadhi ya tools kama majembe ya matrekta , motors na machines etc
Tatizo bado hatujafahamu ni viwanda gani tunahitaji kulingana na uwezo tulionao kwa sasa, ila heavy industries kama ulizoelezea ni ngumu kupata kwa mazingira tuliyonayo. Labda chuma cha liganga kianze kuzalishwa ingawa wawekezaji wanasita shida kubwa ikiwa miundombinu hasa reli toka liganga hadi reli ya tazara makambako.
 
Hata heavy industries tunaweza mali ghafi kibao ziko kongo na Zambia
 
Ngoja tujenge viwanda vya mbolea, kusindika mazao ndio Iwe msingi kwa wakulima kunufaika '' ''':'#pembejeo zatutesa sana kisa viwanda vichache
Watanzania Wenzetu akina Bakhresa, Mohamed enterprise, Azania Millers na wengine kibao wana viwanda tayari vya kusindika mazao tayari vya pembejeo sijui sijafanya research lakini vya kusindika hadi vya mafuta ya alizeti vipo na vinatoa ajira kwa maelfu
 
Watanzania tunalala Sana kutwa kuongea siasa na demokrasia badala ya kuongelea namna gani tutumie fursa zilizopo au zinazotuzunguka bunge limekalia tu siasa badala ya kutoa solutions na kushauri serikali vizuri wanakaa kuongelea bashite na ujinga mwingine usio na kichwa wala miguu. Nashukuru bunge kutoonyeshwa live nilikuwa nasikia kichefuchefu kulitizama. Natamani bunge lijalo wote waliopo wasirudi hata mmoja wawe wa upinzani au chama tawala

Please return to the rock from which you crawled from, because you really don't have the rant of the day...
 
Argument ya kitoto hii japani hawana malighafi hata moja kila kitu cha kiwandani wanaagiza nje ya nchi ukubwa wa nchi yao ni sawa na mkoa wa singida lakini ni nchi iliyoendelea kiviwanda duniani. Nchi nyingi zenye viwanda mali ghafi wanatoa nje ya nchi iwe pamba, chuma, madini ya kutengeneza SIMU, nk japani inauza magari mengi mno hata Tanzania wakati yenyewe japan haina machimbo ya chuma cha kutengeneza magari.Pamba yetu husafirishwa maelfu ya kilomita kwenda nje kwenye nchi zenye viwanda ambazo hazina hata mmea mmoja wa pamba lakini zina viwanda vya uhakika kuliko sisi walima pamba
Japan nafikiri sura ya nchi pamoja na size vili-ilazimu kuchagua viwanda moja kwa moja kama njia pekee ya kujiletea maendeleo. Ni nchi ndogo kama ulivyosema na yenye milima mingi. Kifupi wana ukosefu wa arable land.
Kwa upande wetu tuna added advantage. Tunayo ardhi, mito na maziwa ya kutosha kuweza zalisha malighafi za viwanda hivyo ingekuwa vyema kama tungeitumia ipasavyo.
 
Watanzania Wenzetu akina Bakhresa, Mohamed enterprise, Azania Millers na wengine kibao wana viwanda tayari vya kusindika mazao tayari vya pembejeo sijui sijafanya research lakini vya kusindika hadi vya mafuta ya alizeti vipo na vinatoa ajira kwa maelfu
Mkuu yehodaya huwezi amini mbolea, mbegu, dawa za kuua wadudu shambani ni gharama sana, if wakijenga viwanda vya haya mambo i wish tunafanya agrarian revolution
 
Umenena vyema sana mkuu. Watanzania zaidi ya 75% ni walikuma na zaidi ya 40% y'all ardhi inayolimika hailimwi.Tuna maziwa, mito, Bahari na mabonde yenye rutuba lakini wananchi ni masikini. Tunatengeneza SGR na kununua ndege alafu tunategemea viwanda vije,sijui vitakuja kwa mazingaombwe!!!
 
Japan nafikiri sura ya nchi pamoja na size vili-ilazimu kuchagua viwanda moja kwa moja kama njia pekee ya kujiletea maendeleo. Ni nchi ndogo kama ulivyosema na yenye milima mingi. Kifupi wana ukosefu wa arable land.
Kwa upande wetu tuna added advantage. Tunayo ardhi, mito na maziwa ya kutosha kuweza zalisha malighafi za viwanda hivyo ingekuwa vyema kama tungeitumia ipasavyo.
Japani ilijengewa viwanda na marekani baada ya kupigwa bomu la nyuklia,so alichofanya muamerika ni kuifanyavkama mtoto wake kujikosha kwa lile bomu huwezi fananisha na siye
 
Tungehakikisha tunalima mwaka mzima na pembejeo zinafika kwa wakati huku tukitilia mkazo kwanza viwanda vya mbolea na pembejeo za kilimo tungepiga bao
 
Mimi huwa najiuliza, kwani ni lazima uanze na kilimo ndio vije viwanda.? Hiyo ni kanuni ya kibiblia au Qur'an.? Kwani tukianza na kununua ndege tukajenga reli yetu Standard Gauge, haturuhusiwi kurudi kwenye kilimo.?

Kwani Tanzania imeandikiwa ni lazima iendelee mwaka huu.? hizo siku zote tumekuwa na kilimo chetu hiki cha kawaida ni mwaka gani watanzania labda millioni 1 au 2 walikufa njaa moja.?

Mi nashauri, tumwacheni JPM aendeshe gari anavyojua, maadam keshaonyesha ni dereva mzuri, tutulie. mambo ya kukaa unampangia pangia mawazo yako hayana maana. vinginevyo ungekuwa rais wewe basi..!! kama ulikuwa na mawazo mazuri, mbona hukugombea urais tukakupigia wewe kura..??

JPM ni JPM, na anafuata ILANI ya CCM abaayo ndio wananchi waliiridhia, nyinyi ni nyinyi hamna mbele wala nyuma. vinginevyo mnapoteza muda wenu bure.

Acha tujenge reli kwanza, kilimo pia tunakiangalia japo wewe kwa upofu wako wa kujifanya huwezi ona, na sio lazima wewe ndio uyashuhudie mapinduzi ya kilimo unayoyafikiria, atayashuhudia hata mjukuu wako.

Wewe kwa sasa shuhudia mapinduzi ya reli Tanzania, na mshukuru Mungu kwa kukujalia uhai na kuyashuhudia japo dak za mwanzo, kina Mwl Nyerere, Kawawa, Karume, Sitta, Masaburi n.k hawakubahatika kuona matukio makubwa kama haya ya ki nchi.

Uwe na roho ya kuridhika na kuheshimu maamuzi ya wenzio hasa kwa sababu ndio wenye MAMLAKA YA KUAMUA.
Mkuu,wakati mjerumani na muingereza wanajenga reli,lengo ilikuwa kubeba mkonge na kahawa morogoro,tanga,arusha na pia pamba na tumbaku kutoka kanda ya ziwa,sasa tujiulize,hii reli ikiisha itakuwa inatoa bidhaaa gani kanda hizo kama sasa watu wanaondoa kahawa wanapanda mahindi?

Kama sasa Kilimo cha pamba kanda ya ziwa kimekwisha kufa!

Uzalishaji wa kahawa kagera uko hoi

Hata viwanda vya pamba tunavyoviona kama mwatex,sunguratex,kiwanda cha nyuzi tabora,viwanda vya kahawa,viwanda vya mkonge,hivi vilianzishwa baada ya kuwepo Kilimo,viwanda vilifuata Kilimo,mkoloni alipofika alihamasisha Kilimo kwanza ndipo viwanda vikafata
 
Mikoa ya kanda ya ziwa kwa asili ni wakulima lakini wanategemea mvua wakati kuna ziwa na mito mkubwa isiyo na tija katika kilimo. Kwanini haya maeneo serikali inayaacha hivi wakati kijiografia ni fursa (potential) za wazi?
Kigoma lnastawisha sana mawese (sijui kama nimetumia neno sahihi)ambayo yangetuondolea kero ya kuagiza mafuta nje ya nchi,sijui kwa nini serikali isilipe kipaumbele suala la mawese na kuwekeza vilivyo kwa kuhamasisha na kushirikiana wananchi.

Hii ingechochea export kubwa na pia ingechochea viwanda vya kuongeza thamani!-baada ya kustawi kilimo-viwanda hujongea
 
Kabisa aise
 
Mkuu shukrani kwa bandiko......

Kiufupi ungemwambia mkuu kuwa akili yenye njaa na isiyo na matumaini ya kesho haiwezi kuwaza mambo mengine ya maendeleo zaidi ya njaa....
 
Back
Top Bottom