Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,473
- 13,624
Jiepushe usije kuitwa muongo. Barack Obama anasema katika mambo anayojutia ni suala zima la Libya na uhusika wa Marekani. Kabla hujaandika chunguza kwa undani uhakika wa chanzo chako.Kuna walibya WALIPOULIZWA Kwanini wanataka Gaddafi aondoke walijibu kuwa wanapenda demokrasia zaid. Wazungu wakasema shwari. Walibya wakasaidiwa kumtoa Gaddafi madarakan, tena kwa aibu kubwa. Kilichofuata ndo kama tunavyoona. Hakuna maendeleo wala demokrasia. Hakuna Uhuru wala fursa. Yaliyobaki ni majuto. Libya imevurugwa
Aina yako ndio mnaofaa kuendelea kutumbuliwa kila kukicha. Kukaa kwako wewe na washkaji zako Bar ni muhimu sana kuliko fedha kuwafikia masikini wa vijijini. Poor Tanzanian friend of mine.Mbona Kikwete alijenga barabara za kutosha kwani udicteta wake hata saa hii unanilisha
Mwambie aachie pesa watu tuludi baa
Yes Gaddafi was a great African leader! Waafrika tuna tatizo moja kubwa sana, uelewa mdogo. Wazungu wanatuchezea na kutuaminisha kwamba sungura ni mbwa! Na tunaamini.Ni mara kadhaa sasa nimemsikia mtukufu rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, akiwa anazungumzia suala la amani, akiitolea mfano nchi ya Libya kipindi cha Gadafi.
Kwamba mambo huko Libya yalikuwa safi tu. Vijana waliokuwa wanaoa walipewa hela, nyumba, na mengineyo.
Inawezekana kweli walikuwa wanapewa hivyo vitu lakini je, walikuwa wako huru kiasi gani?
Gadafi alikuwa dikteta. Tena dikteta mkubwa tu aliyeng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu sana hadi walipomfurumsha.
Mtukufu rais Magufuli naye watu wengi wameshaanza kumwona kuwa ni dikteta. Hataki watu wafanye siasa kwenye maeneo yasiyo yao.
Tumeshaona na kusikia watu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa makosa ya kumtukana/ kusema maneno mabaya dhidi yake.
Tumeona vyombo vya habari vikifungiwa kwa sababu zisizo na mashiko.
Sasa haya mambo ya yeye kuisifia Libya ya Gadafi mimi yananitatiza.
Nabaki najiuliza maswali tu. Ina maana yeye Magufuli alikuwa anamwona Gadafi kuwa ni kiongozi bora aliyeweza kutunza amani huko Libya hadi awe anaisifia sifia hivyo?
Kama Gadafi ndo mmoja wa viongozi ambao Magufuli anawaona kama mfano mzuri wa utunzaji wa amani, watu wakimwona na yeye dikteta watakuwa wanakosea kweli?
Ndo mambo ya ndege wafananao hayo au..?
Sasa kama mtu Role model wake ni Kagame unategemea na yeye atakuwaje?
Moja wapo ya alama ya udiketa ni matamshi ya vitisho kama haya "mtu akikuchezea niambie, haitachukua hata dakika 5"
Huyu ilashaonekana toka anagombea kwake msamiati Demokrasia haupo na haamini kama upo.
walibya walikosa uhuru wa kufanya nini?Hivi wewe ukichukuliwa ukawekwa jela na ukalishwa kila aina ya chakula unachotaka je utafurahia ayo maisha ya kifungoni ( bila uhuru)
View attachment 392762
Yes Gaddafi was a great African leader! Waafrika tuna tatizo moja kubwa sana, uelewa mdogo. Wazungu wanatuchezea na kutuaminisha kwamba sungura ni mbwa! Na tunaamini.
Gaddafi hakutolewa madarakani na walibya eti sababu ya kukosa
demokrasia! No. Gaddafi alitolewa na wazungu, kwa sababu zao na malengo yao, hasa ya kiuchumi.
Kwenye nchi au society yeyote lazima kuna kundi japo dogo
litakalo pinga utawala uliopo, that's natural because societies are not homogenious. Walichofanya NATO na mshirika wao US ni ku amplify upinzani wa kundi dogo na kuendesha
propaganda kwamba walibya wanapigana na Gaddafi, na la kusikitisha kuna waafrika wengi tu, wanaamini huu uongo.
Gaddafi na jeshi lake (lenye nguvu) walipigwa na NATO kwa
kutumia silaha za kisasa na mbinu za kisasa. Ndo mana makombora ya kurushwa yalishambulia central commanding and military bases strategically. Mashambulizi ha
ya hatukuonyeshwa kwenye TV, ila tulikuwa tukionyeshwa mfululizo "wahuni" waliovaa vilemba wakizurula kwenye magari ya wazi na kurusha risasi ovyo ovyo angani. Na
bado propaganda zao zilifanikiwa kuwaghiribu waafrika wengi eti ndio waliomwondoa Gaddafi! Inasikitisha sana.
Hakuna chochote anachojuaAlisema Raia zaid ya Million 30 wa Libya waliishi kwa furaha. Watu million 30!! Wakati libya inawatu wasio zidi million 7. Takwimu za mtukufu ni za mwendo kasi
Mleta uzi unataka Rais magufuli atolee mfano nchi gani zaidi ya Libya hapa afrika? Libya ni mfano mzuri wa nchi ya kiafrika iliyo tumia rasilimali zake bila misaada kunyanyua maisha ya wananchi wake
Kuna mfano bora kama huo hapa afrika? Mi siuoni
Kinachozungumziwa hapa siyo matumizi ya rasilimalI. Wewe ndiyo unachemsha. Anyway, Labda ungemshauri Rais aige hayo matumizi ya Rasilimali na siyo namna ya kulinda amani yetu!! La sivyo tutaishia huko huko ilikoishia Libya!Sisi tunaangalia alivyotumia rasilimali za nchi yake na ubunifu kuwasaidia watu wake hayo mengine unajua wewe
Nakushukuru, hasa baada ya kugusia sababu ya kweli ya wazungu kumwondoa Gaddafi!Nimesoma hoja zako hapa na nimekuelewa...Lakini ni wazi kuwa kuna issues nyingine inabidi ujiongeze zaidi...Kwa mfano katika masuala ya uhuru wa watu na suala la kuvifungia vyombo vya habari kwa kutaja machache tu....
Anayozungumza JPM kuhusu Libya ni kweli tupu...binafsi nilibahatika kufika Libya wakati wa Gadhafi na nikakaa Tripoli na maeneo mengine machache kwa karibu wiki mbili hivi...Ni siku chache kuweza kuifahamu nchi, lakini ni wazi Libya wakati wa Ghadafi ilikuwa ni 'heaven' ukilinganisha na hali ya sasa....Ni kweli Libya wakati wa Ghadafi walikuwa wanakosa mambo mengi ya anasa kwa vigezo vya nchi za magharibi...kama pombe, vyombo huru vya habari kwa, na yale mambo mengine ya anasa ambayo siwezi kuyaweka hapa...Lakini Libya wakati huo walikuwa na karibu kila kitu kwa bidhaa madukani..vyakula, nguo za bei rahisi kutoka Italy, Spain, Turkey na kadhalika...Kulikuwa hakuna tatizo la ajira..maji na umeme karibu ni wa bure na wanaume kulipiwa mahali wakati wa kuoa...
Ni kweli walikuwa hawana uhuru kwa maana ya kukosoa uongozi...sikuona pia uhuru katika masuala ya internet...hakukuwa na madawa ya kulevya...vyombo vya habari vilikuwa controlled na kadhalika...
Wamarekani na nchi za magharibi hawakupenda ustawi wa Libya...na pale Ghadafi alipojaribu kupendekeza kuwa dhahabu ndiyo itumike kwenye biashara ya mafuta, ndipo walipokula njama za kumuodoa....
Sijafika Libya ya sasa lakini kwa kupitia vyombo vya habari ni wazi Walibya wanajuta...hakuna serikali pale..Kule Benghazi nadhani wana serikali yao...kuna makundi mengi yenye silaha yenye itikadi tofauti na yanapambana yenyewe kwa wenyewe...mafuta yanachotwa ovyo na mabepari wa nchi za magharibi...
Ndiyo maana walibya wengi wanajuta kwa kuona kuwa walihadaiwa.....Pengine ni vema tujiulize hivi tunapodai uhuru tunamanisha nini???? Libya sasa wana uhuru wa kutukana viongozi, kuchukua silaha na kupigana na kuuana wao kwa wao...Yaani kilichoko Libya sasa ni vurugu...Je, sisi Tanzania ndio uhuru tunaoutaka??? Yaani tunataka uhuru wa kutotii mamlaka??? Tunataka uhuru wa ghasia???? Je, sisi watanzania tunataka hayo??? Uhuru ni jambo jema lakini uhuru pasipo wajibu ni vurugu....
Vyombo vya habari vina nafasi ya kujenga mshikamano na kukemea maovu, lakini vyombo hivyo vikianza kutumika katika kuhakikisha kuwa amani na usalama wa nchi unapotea ni lazima vyombo hivyo vya habari 'vishughulikiwe' kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za nchi yetu.....
Na kwa mfano huo wa Libya ya Gadafi kuwanyima watu wake uhuru mpaka wakayaona maendeleo hayo aliyoyajenga kama machukizo na hatimaye kuanza mapambano dhidi yake.Mleta uzi unataka Rais magufuli atolee mfano nchi gani zaidi ya Libya hapa afrika? Libya ni mfano mzuri wa nchi ya kiafrika iliyo tumia rasilimali zake bila misaada kunyanyua maisha ya wananchi wake
Kuna mfano bora kama huo hapa afrika? Mi siuoni
Hatuwezi kufanana na Libya, ungemuelewa Magu anasema nini kuhusu Libya usingeniuliza haya maswali. Jamaa anazungumzia amani, amani ambayo waliaminishwa na mataifa ya nje kuwa wanatakiwa kuwa huru. Hivyo wamtoe Gaddafi ndo watakua huru, lakini imegeuka fedhehaUmesema vyema sana.
Sasa maswali ya kujiuliza
1. Tanzania tunatoa Scholarship ?
2. Tanzania tunasaida Africa kulipia Matumizi ya Sattelite ?
3. Raia wa Tanzania tuna Maisha bora kuwazidi watu wengine wote barani Africa ?
Ukijbu haya Maswali utajua kuwa hatupaswi kujifananisha na Libya ya enzi za Gadafi,hatufanani nayo hata Chembe...
Ni vizuri ukajijibu mwenyewe ni kwanini nchi za ki Africa especially Tz tuko hivi karibu miaka 60 baada ya uhuru.Utakula huo Uhuru?
Uhuru ndio utajenga barabara na kuhakikisha watoto wote wanaenda shule na kupata elimu bora? Uhuru ndio utaleta madawa hospitalini?
Ingekuwa hivo nchi za kiafrika zisingekuwa hapa kimaendeleo miaka zaidi ya 50 tangia zilipoanza kupata Uhuru.
Kuna watu wanaandika vitu ambavyo havijui hata kidogo na hawataki kujifunza kabisa,kwa hyo wanaandika ilmradi siku zinakwendaAchana na hawa jamaa ni waongo balaa wamesahau hapa mwisho libya ndio ilikuwa inaifadhili AU kipesa na kimuongozo