Rais Magufuli na Libya

Too touchy, brave and courageful nashangaa sana wajinga wanaompinga huyu jamaa
 
Sasa hivi Tanzania mtu kioa hapewi nyumba wala gari wala Pesa yoyote ya kuanzia Maisha kama alivyokuwa anafanya Gadafi.
Sasa Tanzania kuifananisha na Libya ya enzi za Gadafi sio sahihi
Wamesema bado hajamaliza mwaka tusuburiii
 
Labda Watanzania tumesahau jinsi Gadaffi alivyoungana na Idd Amin kuivamia Tanzania. Kuna Watanzania walipoteza maisha yao kwenye ile vita!!
Sisi tunaangalia alivyotumia rasilimali za nchi yake na ubunifu kuwasaidia watu wake hayo mengine unajua wewe
 
N

Nyani ngabu kweli wewe ni nyani fikiria maisha chini ya gadafi libya yalikuaje fananisha na ss hivi, uhuru unakusaidia katika nchi ambayo ukioa unapewa.na mtaji
 
siwezi kujibu kuegemea alipo mtoa bandiko kwa kuwa hata yeye ameonyesha wapi upande alipo.
mkuu kuna mada aliyo ianzisha huyu huyu aliye anzisha mada hii inasema "nani atawaamini tena chadema" tambua upande wake pia.
 

Kama vipi simama upinge basi kamanda?
 
Ni heri uji wa limao kwenye Uhuru, kuliko pilau ng'ombe na soda utumwani
 
mkuu Hata Rais akifungia vyombo vyote vya habari...kubana Uhuru wa kuongea Tanzania haiwezi kuwa kama Libya enzi za Gadafi..... Serikali imeshindwa kunyanyua uchumi...sukari bei juu...biashara zimedoda..ajira hakuna sasa wanachofanya ni kuwatisha wananchi kwa kigezo cha amani ili waendelee kuwatawala....Hao wanaosema wanataka kuvuruga amani hawana hata fimbo
 
N


Nyani ngabu kweli wewe ni nyani fikiria maisha chini ya gadafi libya yalikuaje fananisha na ss hivi, uhuru unakusaidia katika nchi ambayo ukioa unapewa.na mtaji
Tanzania sasa hivi tuna amani mbona sasa hatifanani na libya chini ya Gadafi? Usifananishe Tanzania na Libya ni nchi mbili tofauti sana amani yetu haijatusaidia kitu chochote
 
Mi namsifu Rais magufuli kumsifia Gaddafi alivyoifanya libya.
Maisha yalikuwa shwari libya. Tupa kule propaganda za wazungu. Mwafrika yoyote mpenda nchi yake angetaman nchi yake iwe kama ilivyo kuwa libya. Full misosi japo wapo jangwani. Nyumba na huduma zingine safi sana. Maisha murua. Utake nini zaid!

Kufanikisha hilo alikuwa anawapenda watu wake na alitaka na kuwa na njia za kunyanyua hali za watu wake. Hakuwa na tamaa na ubinafsi


Huduma za afya na Elimu pia shwari zilikuwa

Wazungu wanatufundsha kuwa jamaa alikuwa mwovu. Badala yake wanaona aibu kumsifia mobutu, kipenzi chao. Naamini Zaire ingekuwa kama libya ya Gaddafi kama si hila za wazungu wakimtumia mobutu.

Maendeleo ya Libya hayajaanza zamani sana. Yameanza kipindi Gaddafi ameishika nchi ile

Naamini tuna vitu kama vya libya, na hivyo tukimpata mtu mwenye akili kama ya Gaddafi lazima tufanikiwe

Tatizo Lita kuwa watu wenye mawazo kama ya kwako. Na wabaya wetu hawatopenda maana wanapendelea watu wa kuwatumia kama mobutu

 
Kama watanzania miaka 50 baada ya uhuru bado tuna watu wanafikiri kupatwa kwa jua kumeletwa na mtu huoni kuwa tuko karne nyingi nyuma?
Hivyo watu kuelewa kuwa uhuru wa kutoa mawazo yako una faida nyingi za kimaendeleo itachukua miaka mingi.
Hivyo watawala wetu wanatumia ujinga wa watu wao kwa jusema kuwa kutoa mawazo tofauti ni uvunjivu wa amani. Kwamba mkuu anaweza kujenga amani nchini kwa kutumia mtutu wa bunduki. Ka mikakati ya bunduki haikusaidia Libya, Iraq, Syria na pengine ni kwa nini yeye anataka
kulazimisha?
 
mkuu kuna mada aliyo ianzisha huyu huyu aliye anzisha mada hii inasema "nani atawaamini tena chadema" tambua upande wake pia.
hata hapo mwanzo alikuwa mmoja kati ya waliunga mkono ule mkakati wa kuidai demokrasia. Lakini kwangu mimi huwa naisemea Tanzania, sisemei chama chochote cha SIASA.

Huyu mwandishi ni mmoja kati ya wanaopinga hata kile kizuri kinachofanywa na SERIKALI. na hilo bandiko kuhusu chadema ni aibu baada yq kuona kile alichokuwa akikipigania kushindikana
 
Ndo wazungu wanavyo wadanganya? Tafuteni habari kupitia vyanzo vingi

Majuzi Obama amesema kuwa katika jambo analolijutia zaidi ni kuiingiza marekani kuibomoa libya bila kuwa na mpango thabiti wa jinsi ya kuirejesha nchi hiyo katika hali ya kawaida, ya kutawalika

Nchi zingine za kiafrika zina mengi mazuri ya kujifunza kutoka libya na Gaddafi wake. Na ya msingi ni haya - kutumia rasilimali zilizopo kuiendeleza nchi, kuacha kubabaikia mataifa ya nje, kuacha uroho wa mali na ubinafsi

Mengine mengi ni ngonjera tu, tena za kupotezeana muda.


 

Nawewe nawe! Una shangaa mtu kutokujua kuhusu hilo? Wew unafikiri hajui kila kitu? Wew unajua kila kitu?

Unaongeleaje kudhoofishwa kwa libya, Syria na Iraq katika mtizamo wa kuifananisha na Tanzania? Libya na Syria iraq zilikuwa na tifutifu na wazungu, kimaslahi zaidi wakati Tanzania hamna kitu kama hicho

Eti bunduki, kuna mtu amepigwa shaba hapa? Au kiongozi wa upinzan kubanwa alipe kodi unafananisha Na mtu kupigwa risasi?

Kama watanzania miaka 50 baada ya uhuru bado tuna watu wanafikiri kupatwa kwa jua kumeletwa na mtu huoni kuwa tuko karne nyingi nyuma?
 
Anatumia Libya km kigezo cha kuendelea kubana demokrasia

Hakika magufuli ataaibika vibaya, siku zaja
 
Kuhusu kutolewa mfano Gadaffi, hata mm siliungi mkono...!!

Pia kusema nipe taarifa anayesumbua hatachukua dak. 5 siungi mkono..!!

Haya maneno sio mazuri sana Mh. Rais kutoa..
 
ok, yawezekana chadema wamefeli kama baadhi wanavyo amini, lakini mi naona madai yao yataendelea kuishi kama selekali haitajirekebisha.
 
bora umemchana asee mm mwenyewe nlkua nafkiria maneno ya kumwambia kama hayo big up kiongozi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…