HEKIMA KWANZA
JF-Expert Member
- Mar 31, 2015
- 2,942
- 3,937
Nani aliomba upuuzi uo labda waulize Mimi cha kwanza kwangu ni Uhuru,
Wa kusema
Kutembea
Kutotharirishwa
Mwambie uchara ajipange tunataka democracy
Kuwa nchi ya kifalme haina maana kuwa ni nchi ya kidekta.Swaziland inaongozwa na Mfalme Mswati III na haipo katika orodha ya nchi za kidikteta.Udikteta ni utawala wa vitisho na kunyamazisha raia kwa kutumia mabavu.Kwani hadi Gaddafi anakufa, hizo moroko na Algeria zilikuwa ni tajiri kuliko Libya? Acheni hayo maneno kabisa, maana hata moroko ilikuwa ni nchi ya kifalme na Algeria iliongozwa na rais boutfikra kwa kipindi kirefu...someni historia muelewe
Walibya walikuwa wakiishi maisha ya hofu.Taifa la libya lilikuwa likiendeshwa na polisi enzi za Gadafffi.It was a police state.Ndo wazungu wanavyo wadanganya? Tafuteni habari kupitia vyanzo vingi
Majuzi Obama amesema kuwa katika jambo analolijutia zaidi ni kuiingiza marekani kuibomoa libya bila kuwa na mpango thabiti wa jinsi ya kuirejesha nchi hiyo katika hali ya kawaida, ya kutawalika
Nchi zingine za kiafrika zina mengi mazuri ya kujifunza kutoka libya na Gaddafi wake. Na ya msingi ni haya - kutumia rasilimali zilizopo kuiendeleza nchi, kuacha kubabaikia mataifa ya nje, kuacha uroho wa mali na ubinafsi
Mengine mengi ni ngonjera tu, tena za kupotezeana muda.
Unamahanisha Magufuli ni kama Gadaffi he will stay in power for over thirty years.Walibya walikuwa wakiishi maisha ya hofu.Taifa la libya lilikuwa likiendeshwa na polisi enzi za Gadafffi.It was a police state.
Tanzania tunaelekea huko na baadhi ya watu kama wewe mnafurahia.
Hapana.Tunaelekea kuwa "police state".Hayo ya mbeleni baada ya 2020 siwezi kutabiri.Unamahanisha Magufuli ni kama Gadaffi he will stay in power for over thirty years.
Hivi na Tanzania huwa kuna first lady?Hivi mama Janeth hajafungua ngo's mpaka sasa hivi, au hapendi hela
Ndo mambo ya ndege wafananao hayo au..?
Mleta uzi unataka Rais magufuli atolee mfano nchi gani zaidi ya Libya hapa afrika? Libya ni mfano mzuri wa nchi ya kiafrika iliyo tumia rasilimali zake bila misaada kunyanyua maisha ya wananchi wake
Kuna mfano bora kama huo hapa afrika? Mi siuoni
Nimesoma hoja zako hapa na nimekuelewa...Lakini ni wazi kuwa kuna issues nyingine inabidi ujiongeze zaidi...Kwa mfano katika masuala ya uhuru wa watu na suala la kuvifungia vyombo vya habari kwa kutaja machache tu....
Anayozungumza JPM kuhusu Libya ni kweli tupu...binafsi nilibahatika kufika Libya wakati wa Gadhafi na nikakaa Tripoli na maeneo mengine machache kwa karibu wiki mbili hivi...Ni siku chache kuweza kuifahamu nchi, lakini ni wazi Libya wakati wa Ghadafi ilikuwa ni 'heaven' ukilinganisha na hali ya sasa....Ni kweli Libya wakati wa Ghadafi walikuwa wanakosa mambo mengi ya anasa kwa vigezo vya nchi za magharibi...kama pombe, vyombo huru vya habari kwa, na yale mambo mengine ya anasa ambayo siwezi kuyaweka hapa...Lakini Libya wakati huo walikuwa na karibu kila kitu kwa bidhaa madukani..vyakula, nguo za bei rahisi kutoka Italy, Spain, Turkey na kadhalika...Kulikuwa hakuna tatizo la ajira..maji na umeme karibu ni wa bure na wanaume kulipiwa mahali wakati wa kuoa...
Ni kweli walikuwa hawana uhuru kwa maana ya kukosoa uongozi...sikuona pia uhuru katika masuala ya internet...hakukuwa na madawa ya kulevya...vyombo vya habari vilikuwa controlled na kadhalika...
Wamarekani na nchi za magharibi hawakupenda ustawi wa Libya...na pale Ghadafi alipojaribu kupendekeza kuwa dhahabu ndiyo itumike kwenye biashara ya mafuta, ndipo walipokula njama za kumuodoa....
Sijafika Libya ya sasa lakini kwa kupitia vyombo vya habari ni wazi Walibya wanajuta...hakuna serikali pale..Kule Benghazi nadhani wana serikali yao...kuna makundi mengi yenye silaha yenye itikadi tofauti na yanapambana yenyewe kwa wenyewe...mafuta yanachotwa ovyo na mabepari wa nchi za magharibi...
Ndiyo maana walibya wengi wanajuta kwa kuona kuwa walihadaiwa.....Pengine ni vema tujiulize hivi tunapodai uhuru tunamanisha nini???? Libya sasa wana uhuru wa kutukana viongozi, kuchukua silaha na kupigana na kuuana wao kwa wao...Yaani kilichoko Libya sasa ni vurugu...Je, sisi Tanzania ndio uhuru tunaoutaka??? Yaani tunataka uhuru wa kutotii mamlaka??? Tunataka uhuru wa ghasia???? Je, sisi watanzania tunataka hayo??? Uhuru ni jambo jema lakini uhuru pasipo wajibu ni vurugu....
Vyombo vya habari vina nafasi ya kujenga mshikamano na kukemea maovu, lakini vyombo hivyo vikianza kutumika katika kuhakikisha kuwa amani na usalama wa nchi unapotea ni lazima vyombo hivyo vya habari 'vishughulikiwe' kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za nchi yetu.....
Sawa lakini democrasia ilipwaya ndo maana wlibya walimchoka, kwahiyo wewe ukoradhi kuingia jera ilimradi tu unapewa kila kitu bure? tena familia yako nayo inatunzwa bure, kwa maana nyingine unaweza kufanya mazuri kwa wananchi wako lakini bila democrasia siku ukiondoka kinahalibika kila kitu, hiyo ndo Libya.Mleta uzi unataka Rais magufuli atolee mfano nchi gani zaidi ya Libya hapa afrika? Libya ni mfano mzuri wa nchi ya kiafrika iliyo tumia rasilimali zake bila misaada kunyanyua maisha ya wananchi wake
Kuna mfano bora kama huo hapa afrika? Mi siuoni
Sasa Libya kuna mabadilikooooo Lowassaaaaaaa wanazama melini na kuliwa na masamakibhNi mara kadhaa sasa nimemsikia mtukufu rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, akiwa anazungumzia suala la amani, akiitolea mfano nchi ya Libya kipindi cha Gadafi.
Kwamba mambo huko Libya yalikuwa safi tu. Vijana waliokuwa wanaoa walipewa hela, nyumba, na mengineyo.
Inawezekana kweli walikuwa wanapewa hivyo vitu lakini je, walikuwa wako huru kiasi gani?
Gadafi alikuwa dikteta. Tena dikteta mkubwa tu aliyeng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu sana hadi walipomfurumsha.
Mtukufu rais Magufuli naye watu wengi wameshaanza kumwona kuwa ni dikteta. Hataki watu wafanye siasa kwenye maeneo yasiyo yao.
Tumeshaona na kusikia watu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa makosa ya kumtukana/ kusema maneno mabaya dhidi yake.
Tumeona vyombo vya habari vikifungiwa kwa sababu zisizo na mashiko.
Sasa haya mambo ya yeye kuisifia Libya ya Gadafi mimi yananitatiza.
Nabaki najiuliza maswali tu. Ina maana yeye Magufuli alikuwa anamwona Gadafi kuwa ni kiongozi bora aliyeweza kutunza amani huko Libya hadi awe anaisifia sifia hivyo?
Kama Gadafi ndo mmoja wa viongozi ambao Magufuli anawaona kama mfano mzuri wa utunzaji wa amani, watu wakimwona na yeye dikteta watakuwa wanakosea kweli?
Ndo mambo ya ndege wafananao hayo au..?
Anamfanyia ubabeHivi na Tanzania huwa kuna first lady?
Unajua mpaka nimesahau kama jamaa waga ana mke.
Kwahyo unataka kusema kwamba Libya ya sasa ndio Libya bora kuliko ya Gaddafi?Ni mara kadhaa sasa nimemsikia mtukufu rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, akiwa anazungumzia suala la amani, akiitolea mfano nchi ya Libya kipindi cha Gadafi.
Kwamba mambo huko Libya yalikuwa safi tu. Vijana waliokuwa wanaoa walipewa hela, nyumba, na mengineyo.
Inawezekana kweli walikuwa wanapewa hivyo vitu lakini je, walikuwa wako huru kiasi gani?
Gadafi alikuwa dikteta. Tena dikteta mkubwa tu aliyeng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu sana hadi walipomfurumsha.
Mtukufu rais Magufuli naye watu wengi wameshaanza kumwona kuwa ni dikteta. Hataki watu wafanye siasa kwenye maeneo yasiyo yao.
Tumeshaona na kusikia watu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa makosa ya kumtukana/ kusema maneno mabaya dhidi yake.
Tumeona vyombo vya habari vikifungiwa kwa sababu zisizo na mashiko.
Sasa haya mambo ya yeye kuisifia Libya ya Gadafi mimi yananitatiza.
Nabaki najiuliza maswali tu. Ina maana yeye Magufuli alikuwa anamwona Gadafi kuwa ni kiongozi bora aliyeweza kutunza amani huko Libya hadi awe anaisifia sifia hivyo?
Kama Gadafi ndo mmoja wa viongozi ambao Magufuli anawaona kama mfano mzuri wa utunzaji wa amani, watu wakimwona na yeye dikteta watakuwa wanakosea kweli?
Ndo mambo ya ndege wafananao hayo au..?