Mackanackyyy
JF-Expert Member
- Mar 26, 2019
- 2,338
- 5,263
Rais Magufuli alipiga marufuku shughuli halali za vyama vya siasa nchini akiamini hatua hiyo itampunguzia upinzani kutoka Chadema, na kwa kiasi flan kutoka kwa watu wanaojitambua ndani ya ccm..
Akakipa nafasi chama chake kifanye siasa, kitukane watu, kidhalilishe watu, kiwapige akina Lissu risasi, kiwapoteze akina Azory Gwanda, akina Ben Saanane...
Sasa wamewamaliza watu wa nje ya chama chao wameanza kutukanana wenyewe ndani kwa ndani, wanabaguana, wamegundua kumbe na wao siyo wamoja...sasa kuna kila dalili wataanza wenyewe kupinduana, kupigana risasi, kupotezana na wao!
Pengine wakimalizana ndani ya chama chao watahamishia siasa zao jeshini...(Mungu aepushe).
Lakini hoja yangu ni kwamba Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM atulie sasa, asipaniki...ni YEYE ALIYETAKA SIASA ZA NDANI, ZA NJE HAPANA. Awaache sasa watu wamfundishe siasa "za ndani" huko.kwenye chama chake!
Nyerere alisema dhambi ya ubaguzi ukishaitenda haiwezi kukuacha salama, itakuandama tu...mtawabagua watu lakini hatimaye mtagundua kuwa na nyinyi si wamoja, mtaanza kuhujumiana, kutekana, kupinduana, kuuana!