Rais Magufuli, mwondoe Waziri Nnauye kabla hajakuharibia

Nape hajui cheo chake ni kuwatumikia watanzania wote bila kujali vyama,jana nimemsikia anaponda sana wapinzani
Keshaanza na mawio,sasa katunyima haki.ya kuona bunge,kesho ataanza kufungia tv ambazo hazikuisuport ccm,na pia redio..shameee
 
Mimi, kama kada wa muda wa CCM na mtanzania, natoa rai kwako Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli. Ingawa rai yangu imewahi, naitoa kukulindia heshima ya utendaji wako na sifa zako. Mwondoe Waziri Nape Nnauye.

Waziri Nape ni bingwa wa propaganda. Amelemaa kwa hilo. Kiĺa anachosema au kufanya hulenga kuwagusa na kuwakera wapinzani. Kuwadhibiti na kuwakomesha. Nchi haiendeshwi hivyo.

Anaongea vihoja badala ya hoja. Anaongea kwa kiburi na jeuri. Anajiona yeye ndiye yeye, hakuna mwingine. Akiteleza kimaandishi na kimatamshi hataki kukubali. Ya jana, yatakuharibia Mhe. Rais.

Watanzania hawana viwanja vya wazi kupumzika. Wengi hawana shughuli ya siku nzima. Wamejiajiri wenyewe kufuatilia Bunge moja kwa moja. Kufuatilia siasa. Kufuatilia matunda ya kura zao. Iweje wanyimwe hata haki/ajira yao hiyo ya kikatiba?

TBC1 ni chombo cha kiserikali. Serikali haifanyi biashara. Serikali, kwahiyo, haipati faida wala hasara. Iweje TBC1 ilalamikie gharama? Zile pesa zinazotengwa kwa ajili ya shirika hilo ziko wapi? Kukataza matangazo ya moja kwa moja ni kuwakataza wananchi kujua cha Bungeni. Si sahihi.

Waziri Nape aondolewe. Atakuharibia Rais Magufuli!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba)

Umesahau kumweleza kwamba BUNGE siyo serikali.Mwambie tunahitaji BUNGE lenye MENO,siyo BUNGE alilotuchagulia mpaka naibu spika.

Ni aibu kubwa kwa serikali ya MAGUFULI
 
Wasichokielewa watu ni ukweli kwamba Nape ni mfikisha ujumbe na sio mmiliki wa ujumbe. Ni muajiriwa ambaye ajira yake inategemea maamuzi ya rais. Mpaka serikali inapofikisha ujumbe maana yake ni kuwa baraza zima la mawaziri linahusika, sio maamuzi ya Nape kama Nape bali ni ya waziri wa habari anayefikisha ujumbe ambao ni makubaliano ya pamoja ya baraza la mawaziri.
 
nimeangalia tbc muda huu wanaonyesha tu mziki wa bongo fleva. yaaani ni aibu saaana....
 
Hivi hizo TV maofisini waliziweka za nini? Mapambo au ni za kuangalia kinachoendelea nchini na duniani!!!
 
Pasipo shaka ni dhahiri wazi kabisa Waziri wa Habari na Michezo, Moses Nape Nnauye ameonyesha wazi kabisa kushindwa kuendana na kasi, malengo ya Mhe Rais Magufuli ambayo alituahidi katika kampeni za kusaka kura kutoka kwa wananchi.

Nape Nnauye ameonekana kutetea kwa wazi kabisa maslahi ya chama chake cha ccm ambapo awali alikuwa katibu wa itikadi na uenezi kupitia chama hicho kitu ambacho tunategemea Mh Rais alikikataa toka wakati wa kampeni.

Viatu vya uwaziri vimempwaya waziri huyo analiyeanza kutoa ulimi nje ishara ya kuishiwa pumzi kabla hata mbio hazijaanza.

Namuomba Nape ajitathimini upya katika utendaji wake, ajipime na kujiridhisha, ninaamini pale Lumumba panamfaa zaidi kuliko uwaziri huu aliopewa, huku ni kumuonea.

Mh Rais tunaamini utaliona hili na kuchukua hatua za haraka kabla hatujashuhudia vioja vingine vizito zaidi.

Mtu anayetetea maslahi ya chama na kusahau wananchi hatufai.

Nape anataka kuficha maovu ambayo Mh Rais anayasaka kwa udi na uvumba ili ayashughulikie.

Wasalaam...
 
Rais wetu mpya hajamaliza siku 100 lakini ameshaleta maumivu na mateso kwa watu wengi wasio na hatia.
1. Kubomoa nyumba za watu, nao wako destitute/homeless
2. Kufukuzwa/kusimamishwa kazi kwa makosa ya wengine
3. Kutufanya watz wote cleaners siku muhimu ya uhuru wetu
5. waliokuwa wanafaidika na viongozi kwenda nje sasa wanalia njaa kali
6. Kuwanyima wale waliompa kura haki ya kupata habari n.k
Ni vizuri ukifanya jambo uangalie na upande wa pili, ule ambao hupendi hata kuusikia.
 
Huyu ndo aliyeua ccm na kuchukiwa na wengi,magufuli kampa uwaziri sasa atafanya serikali na jitihada zote za magufuli zionekane magumashi
 
Hakuna haja kumsema Nape, mlaumu aliemlisha Kande

Kumbuka MTOTO AKINYA KANDE KATEMEWA
 
Nape ni mmoja wa mawaziri wabovu sana wa Magufuli yeye ccm kwanza kuliko Tanzania
 
Mimi, kama kada wa muda wa CCM na mtanzania, natoa rai kwako Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli. Ingawa rai yangu imewahi, naitoa kukulindia heshima ya utendaji wako na sifa zako. Mwondoe Waziri Nape Nnauye.

Waziri Nape ni bingwa wa propaganda. Amelemaa kwa hilo. Kiĺa anachosema au kufanya hulenga kuwagusa na kuwakera wapinzani. Kuwadhibiti na kuwakomesha. Nchi haiendeshwi hivyo.

Anaongea vihoja badala ya hoja. Anaongea kwa kiburi na jeuri. Anajiona yeye ndiye yeye, hakuna mwingine. Akiteleza kimaandishi na kimatamshi hataki kukubali. Ya jana, yatakuharibia Mhe. Rais.

Watanzania hawana viwanja vya wazi kupumzika. Wengi hawana shughuli ya siku nzima. Wamejiajiri wenyewe kufuatilia Bunge moja kwa moja. Kufuatilia siasa. Kufuatilia matunda ya kura zao. Iweje wanyimwe hata haki/ajira yao hiyo ya kikatiba?

TBC1 ni chombo cha kiserikali. Serikali haifanyi biashara. Serikali, kwahiyo, haipati faida wala hasara. Iweje TBC1 ilalamikie gharama? Zile pesa zinazotengwa kwa ajili ya shirika hilo ziko wapi? Kukataza matangazo ya moja kwa moja ni kuwakataza wananchi kujua cha Bungeni. Si sahihi.

Waziri Nape aondolewe. Atakuharibia Rais Magufuli!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba)
mzee tupa tupa hebu njoo tena
 
Kweli mtu mzima dawa. Mkuu nimesoma maoni yako..japo hayafanani moja kwa moja na yanayo endelea ila kuna point zina ukweli mchungu.

Ni kweli nape hafai uongozi. Nape anapenda kuvuruga na kujitengenezea nafasi yake ya ulaji. Nape anapenda yeye aonekane kuliko wengine katika kundi fulani. Nape anadharau na kiburi. Nape hulewa sifa na hupenda sifa.
Kwa hali ilivyo Nape hafai kuwa chini ya kiongozi la sivyo anaweza kumharibia mtu iwapo matakwa yake hayatasikilizwa. Nape na ccm yake ndo wametufikisha hapa ndi ya chama na nje ya chama. Makundi kuanzia chamani na sasa makundi bungeni. Nani anaweza akamuondoa Nape kwenye Uso wa madaraka ya watanzania kwa sasa? Rais ametuonyesha kwa kuanzia uwaziri. Anaweza asimtoe uanachama kwa sasa alikini namshauri tu 2020 apumzike afanye mengine sana. Nape anatabia za divide and rule.

Baraza la mawaziri kazi yake ni kumsaidia rais lakini kwa akili ya nape yeye katoka kujitofautisha na sio kumsaidia. Nape atakoishia anapajua mwenyewe.
 
Mimi, kama kada wa muda wa CCM na mtanzania, natoa rai kwako Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli. Ingawa rai yangu imewahi, naitoa kukulindia heshima ya utendaji wako na sifa zako. Mwondoe Waziri Nape Nnauye.

Waziri Nape ni bingwa wa propaganda. Amelemaa kwa hilo. Kiĺa anachosema au kufanya hulenga kuwagusa na kuwakera wapinzani. Kuwadhibiti na kuwakomesha. Nchi haiendeshwi hivyo.

Anaongea vihoja badala ya hoja. Anaongea kwa kiburi na jeuri. Anajiona yeye ndiye yeye, hakuna mwingine. Akiteleza kimaandishi na kimatamshi hataki kukubali. Ya jana, yatakuharibia Mhe. Rais.

Watanzania hawana viwanja vya wazi kupumzika. Wengi hawana shughuli ya siku nzima. Wamejiajiri wenyewe kufuatilia Bunge moja kwa moja. Kufuatilia siasa. Kufuatilia matunda ya kura zao. Iweje wanyimwe hata haki/ajira yao hiyo ya kikatiba?

TBC1 ni chombo cha kiserikali. Serikali haifanyi biashara. Serikali, kwahiyo, haipati faida wala hasara. Iweje TBC1 ilalamikie gharama? Zile pesa zinazotengwa kwa ajili ya shirika hilo ziko wapi? Kukataza matangazo ya moja kwa moja ni kuwakataza wananchi kujua cha Bungeni. Si sahihi.

Waziri Nape aondolewe. Atakuharibia Rais Magufuli!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba)

Sasa mkuu unasimamia wapi ktk huu uzi ama ktk u hero wa Nape wa leo?
 
Mkuu ukisema naoe ni hero.. Unakosea sana. Nape alipoona haendani na mwelekeo wa bosi wake ilikuwa ni kuacha kazi. Yeye anaanza uanaharakati palepale kwenye cheo cha kupewa na aliyekupa. Kwa sasa inamuuma sana. Nape hafai kuwa popote. Nape huleta mugawanyiko sehem yoyote ile. Hata iwe nyumbani nape nataka aonekane wa maana kuliko wengine.

Kwa sasa anaenda kulialia jimboni kwake badala ya kupeleka maendeleo anapeleka chuki zake na watu wasio wa jimbo lake. Chuki yake na Makonda inawahusu nini wanamtama kama sio kutojielewa?

Mgawanyiko alio ufanya nape chamani enzi zake na sasa bungeni hafai tena kukaa sehemu yeyote ile.
 
Back
Top Bottom