Kwa kujua au kuto kujua, JPJM ndo kamtuma Nape kushughulikia vhyomba vya habari vinavyofanya kazi kinyume cha chama na serikali. Kwa upande wa TBC, hicho ni chombo cha watanzania wavuja jasho na walipakodi. Hata hivyo JPJM amemweka NApe kwa sababu ni mtaalamu wa propaganda na hivyo atasaidia kuweka chama tawala na serikali katika mazingira ambayo kitaendelea kuaminika kwa sababu maovu mengi hayatajulikana.
JPJM hawezi kumuondoa nape kwa sababu amemweka kimkakati zaidi. Sula ni kwamba; mkakati huo ni kwa masilahi ya nani? Tuendelee "kuamini" ni kwa ajili ya Taifa tu na siyo CCM.
Kama kuna udhalimu wowote katika maamuzi yaliyofanyika; kuwanyima watu fursa ya kuona wenyewe kinachojili bungeni, hata hivyo udhalimu huo utafikia mwisho hatimaye!
Mungu ibariki Tanzania