Rais Magufuli: Mimi ni mzilankende muyango

Rais Magufuli: Mimi ni mzilankende muyango

Msitake kutuletea ujinga wenu katika kipindi mahususi ya kujenga nchi. Hata kama angekuwa hana asili na leo akaamua kuwa Tz na kutusaidia watanzania sie tunaona anatufaa. Hivi tukianza kutafuta mababu na mabibi hapa Jf atasalia nani?
Mjinga ni wewe asiyejua maana ya jamii forum
 
Kalizaliwa 29/10/1959 na Rwanda kulikuwa na Vita kati ya mwaka 1959 mpaka 1961. Hii majibu tu ya swali lako lakini sijasema ni ukweli kazaliwa Rwanda au la, hivyo chukua majibu changanya na akili zako utapata muafaka.
Za mbayuwayu
 
Kweli mtandao wa Jamiiforums ni hazina ya kutunza kumbukumbu.

Natumai kuwa idara ya uhamiaji itafanya kazi kuwatambua kina "Muyango yaani "abayango" hujiita Wazilankende" kama ni raia au la.

Maana kufanya zoezi la uhakiki wa uraia kwa familia ya Askofu Zachary Kakobe pekee inaonesha idara ya uhamiaji ina fanya kazi kwa shindikizo na siyo kwa uweledi.
 
Naona kitendo cha uhamiaji kuthibitisha kuwa kakobe na magufuli wanatoka koo moja, kimemuokoa kakobe kupimwa mkojo, duu ukabila hautaisha afrika
 
Wazee kijijini kwa Askofu Mkuu Zachary Kakobe wamesema kwamba, Askofu Kakobe na yeye ni Muyango Mzilankende.

ANGALIA HAPA:
Uhamiaji waenda kuchunguza uraia wa Askofu Mkuu Kakobe kijijini kwake, wazee mashuhuri kijijini wathibitisha uraia wake

Kumbe Rais John Pombe Magufuli na Askofu Kakobe ni ndugu. Wote ni wa ukoo mmoja, Wayango Wazilankende! HILI NALO NENO!
That is to say HE is not a Sukuma as it is claimed! How did he become a Sukuma? And if Kakobe isn't a Tanzanian, then the other Mzilankende is also not a...! Immigration please!
 
That is to say HE is not a Sukuma as it is claimed! How did he become a Sukuma? And if Kakobe isn't a Tanzanian, then the other Mzilankende is also not a...! Immigration please!

Ukiona subaru nyeupe inakufuatilia nibeep nitakusaidia
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mimi niulize. Wanaosema magifuli ni MHUTU. Eti mama yake alikuja kuolewa akiwa na miba yake kutoka rwanda. Ebu nisaidie hapo
 
Heshima kwenu wakuu,

Juzi rais alipotutembelea huku kwetu Kagera, rais Magufuli alijinasibu kwamba yeye ni Muyango yaani "abayango" hujiita Wazilankende. Akadai babu yake alizikwa pale Bukoba mjini Sehemu inaitwa Uswahilini pale karibu na Sanamu la Mayunga. Jina la babu yake limenitoka nikikumbuka ntaedit niweke hapa ila ni kama alisema aliitwa Mzee Mshalila(?).

Huyu mzee Mashalila alizaa watoto watatu, bahati mbaya hawa watoto wapo hadi leo sema akili zao hazipo sawa. Wapo Uswahili pale Bukoba Mjini.

Kwa wasiofahamu sifa ya Wazilankende ngoja nifafanue kidogo. Nkende ni ngedere, sasa hawa wazilankende ni marafiki wa ngedere. Yaani hata akimuona ngedere barabarani inatakiwa awabebe ndizi. Akikuta ngedere amekufa inabidi alie au anaumwa inabidi amtibie. Hao ndo wazilankende.

Hata ukiangalia kwenye hotuba ya Mbunge wa bukoba mjini Mh. Lwakatare wakati anamkaribisha alisema karibu nyumbani Mzilankende "wayanga waija" hatimaye umekuja(kwa tafsiri isiyo sahihi.).

Ndugu zake rais Magufuli waliopo Bukoba ni Oscar Mashalila, Dotto Mashalila watatu nmesahau jina la mtoto wa tatu, sema ni maarufu tu mjini japo hapo sawa.

Huo ulikuwa ni utangulizi. Swali langu ni;

Rais Magufuli ni nani?
1. Mzilankende
2. Msubi,
3. Msukuma
Au Muyango?

Kusema kweli mtakuwa mumenaidia sana.

Lakini sijawahi kumsikia yeye akisema ni msukuma Bali lafudhi yake ndio ya kisukuma na anakijua kisukuma. Hata Mimi kwetu ni Singida ila nimekulia shinyanga na kisukuma nakijua siwezi kusema Mimi ni msukuma.
Ila yeye binafsi amekiri ni Mzilankende na watu walisema babu yake alizikwa bukoba Mjini nabyeye amekiri alizikwa bukoba Mjini na zaidi ya yote ndugu zake wako bukoba kuliko shinyanga na Mwanza. Usukumani hana uko wala ndugu na hata haijawahi kuishi na hakuna mtu aliyewahi kuleta information yoyote kwamba anatoka usukumani eneo gani na ndugu zake ni wapi
 
Bila kwenda ndani sana ambako mengine si muhimu. Magufuli ni MCHANGANYIKO wa damu kadhaa MIXED BLOOD.
Ana damu ya KISUKUMA na ana damu ya makabila mengine baadhi ya hayo hapo juu.
Wasukuma huwa HAWANA HASIRA kali Magufuli ni MKALI SANA na mwepesi wa KUKASIRIKA!
Hiyo SI hulka ya WASUKUMA! Wasukuma ni WAPOLE!

ACCENT/ LAFUDHI ya Magufuli si PURE KISUKUMA ukimsikiliza kwa makini ana Lafudhi tofauti. kwa sababu ya DAMU mchanganyiko!

Japokuwa Magufuli anakizungumuza Kisukuma vizuri sana lakini si Msukuma kamili.
Japokuwa familia yake the MAGUFULIS huongea KISUKUMA wakiwa nyumbani bado yeye si PURE Msukuma.

Kama ILIVYO KAWAIDA ya Watanzania wengi, Tuko MIXED blood hakuna aliye PURE kabisa labda wa kule ndani sana.
Hata hivyo ukifuatilia BLOODLINE/UKOO utakuta watu wengi si PURE/ KAMILI katika kabila lake

hata Magufuli ni kama WEWE na MIMI. HUO ndo UZURI wa nchi ya Tanzania INTERMARRIAGE /KUOANA makabila tofauti zimevunja UKABILA.

Labda tu umebaki kwa makabila wachache sana WANAOJIBAGUA na KUOANA wao kwa wao!
INTERMARRIAGE kuona nje ya kabila lako kumeisadia Tanzania. Kwa hilo NAJIVUNIA nchi yangu Tanzania!
Hakuna ushahidi wowote kwamba ni msukuma labda lafudhi na kuongea kisukuma lakini sio babu yake wala bibi yake mwenye asili ya usukumani, na hatujawahi kuelezwa usukumani anauhusiano na ukoo upi.
Kama una ushahidi basi mwambie kama babu na babu yake alikuwa msukuma wa wapi. Kuongea lugha Fulani sio kwamba wewe ni wa pale. Wapo wengi wamekulia usukumani na wanaongea kisukuma vizuri tu lakini huwezi kusema ni wasukuma
 
Ili ku summarize. Acha nikusaidie.
Magufuli ni MSUKUMA. Period.
Mengine hayo ni yako.
 
Sa mnabishana kabila la Rais litawasaidia nini? Kama unataka kujua msikilize alipokuwa anafanya ziara mkoa wa tabora alisema wazi ni msukuma!
 
"Abayango" ni koo kati ya koo zinazopatikana katika mkoa wa Kagera, sisi tunaotoka mkoa huo tunazijua koo zetu vizuri sana na tunaziheshimu koo zetu. Sasa msije kuanza kuzitaja kana kwamba ni majina ya nguo zenu mnazovaa ama ikawa kila mtu anatafuta pa kufia, hao wanaojipitisha pitisha huku na huko ili kupata pa kujishikisha waache mara moja. Tunasema tena hao watu waache mara moja. Unasemaje wewe ni Myango wakati maneno yenyewe ya kihaya unababaisha? unajiitaje wewe mzilankende wakati lafudhi yako ni sawa na "washuti"?
 
Mbona mimi nina kabila langu asili. Lakini SIWEZI kuieleza KIKAMILIFU bila kuingiza neno la Kiswahili.
Je mimi si kabila langu?
 
Back
Top Bottom