Rais Magufuli: Kwanini mtu alipwe tsh 500 million kujenga mortuary?

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
"Hatuwezi KULIPA MIL 500, Hili JIPU LIMEKOMAA, Mfukuzeni, Tukutane MAHAKAMANI" - Rais Dkt John Magufuli, leo Februari 11, amezindua wilaya mpya Kigamboni, Jengo la utawala na Hospitali ya Wilaya jijini Dar.



Mh. Rais ahoji kwanini mtu aingie mkataba wa ujenzi allipwe Tsh 500 million ili kujenga mortuary na kutoa tamko afukuzwe na serikali ili ikutane nae mahakamani.

Juzi siku ya Kuadhimusha Siku ya Sheria ilitamkwa kuwa ni kauli mbiu ni sheria na uwekezaji: Kaulimbiu Uwekezaji na Biashara: wajibu wa mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.

Ikiwa na maana mambo yote yasifanyike kwa matamko bali hali halisi ikiwemo kama hili la leo ambapo kutokana na mkataba si ajabu mtu kudai kiasi hivyo kama 'bei ya soko' ilivyo.

Sasa serikali kulazimisha kumpeleka mwananchi mahakamani ili adai fidia kesi hiyo itasomwa na kufuatiliwa na wengi wananchi na wawekezaji kisha kutia hofu jamii kuwa serikali hutumia mabavu kupata inachotaka bila kujali haki ya mwenye mali/mkataba/kandarasi.

Source: Global TV online
 
February 6, 2020
Kaulimbiu Uwekezaji na Biashara :wajibu wa mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.

Hii ni mara ya tano kwa Rais Magufuli kushiriki maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambayo kwa mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo uwekezaji na biashara :wajibu wa mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.




Maadhimisho ya Siku ya Sheria : ktk Jumba la Mwl. Julius Nyerere Jijini Dsm
AGIZO ALILOLITOA MAGUFULI LEO KWA JAJI MKUU, NI HILI..| TBC1

Streamed live on 6 Feb 2020
AGIZO ALILOLITOA MAGUFULI LEO KWA JAJI MKUU, NI HILI..| TBC1 Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa mahakama ili kutekeleza ukarabati na ujenzi wa miundombinu inayolenga kusaidia kasi ya uendeshaji wa kesi Nchini kwa lengo la kupunguza mahabusu kwenye magereza. Rais Magufuli ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Ambapo amesisitiza suala la mahakama kuharakisha upelelezi wa kesi ili kuondokana na changamoto zinazojitokeza kwa sasa. Kwa upande wake Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma ameelezea mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka mmoja huku akibainisha baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo upungufu wa rasilimali watu.

Naye Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai ametumia fursa hiyo kuipongeza serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya mahakama nchini kwa lengo la kuchochea upatikanaji wa haki na kudumisha Amani nchini. Hii ni mara ya tano kwa Rais Magufuli kushiriki maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambayo kwa mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo uwekezaji na biashara :wajibu wa mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji. Kifungu cha 8 cha Kanuni ya Adhabu (The Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kinabainisha kutomwondolea hatia mtuhumiwa licha ya kutokuwa na uelewa wa Sheria, Hivyo Mahakama nchini inaendelea na mkakati wa kutumia teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuleta mabadiliko kwenye utoaji haki.
 
Kwani anaedai kulipwa milion mia 5 ni mmoja tu na kama ni mmoja kwa nini majirani zake wamekubali kiasi walichopewa lakini kwa nini asilipwe maana nchi hii ni tajiri sana
 
February 11, 2020

Hatuwezi KULIPA MIL 500, Hili JIPU LIMEKOMAA, Mfukuzeni, Tukutane MAHAKAMANI" - JPM Rais Dkt John Magufuli, leo Februari 11, amezindua wilaya mpya Kigamboni, Jengo la utawala na Hospitali ya Wilaya jijini Dar.



Mh. Rais ahoji kwanini mtu alipwe fidia ya mali yake tsh 500 million na kutoa tamko afukuzwe serikali inakutane nae mahakamani. Juzi siku ya Kuadhimusha Siku ya Sheria ilitamkwa kuwa ni kauli mbiu ni sheria na uwekezaji . Ikiwa na maana mambo yote yasifanyike kwa matamko bali hali halisi ikiwemo kama hili la leo ambapo kutokana na bei ya soko ya viwanja Kigamboni si ajabu mtu kudai kiasi hivyo kama 'bei ya soko' ilivyo.

Sasa serikali kulazimisha kumpeleka mwananchi mahakamani ili adai fidia kesi hiyo itasomwa na kufuatiliwa na wengi wananchi na wawekezaji kisha kutia hofu jamii kuwa serikali kutumia mabavu kupata inachotaka bila kujali haki ya mwenye mali.



Source: Global TV online

Bwashee umechanganya madesa!
 
Bwashee umechanganya madesa!

Shukrani , nimeona makosa na kusahihisha bandiko na kutenda haki. Tujiulize itakuwa vigumu sana kufanya biashara si na serikali tu bali hata kuwekeza maana huwezi kujua tamko likitoka juu mkataba utaheshimiwa au utabakia kufuatilia kesi mahakamani. Na mahakama pia itakuwa under pressure kutoa maamuzi yasiyo na haki juu ya biashara ya makubaliano.
 
Back
Top Bottom