Naona tayari ana maadaui wengi ndani ya CCM na baadhi yao wameshajitokeza hadharani kusema watampinga mwaka 2020. Hawa wanaosema hivi si watu wema na wanambinu mbalimbali kuhakikisha Rais Magufuli hagombei mwakani.
Hawa ni watu hatari hata kama katiba inawaruhusu ila Chama chao hakiruhusu kwa kupitia taratibu na kanuni ilizojiwekea bado najiuliza, ni busara gani iliyotumika kwa Mhe Membe kwa mfano kujitokeza sasa kabla ya muda na kutangaza nia yake ya kuomba ridhaa CCM kabla ya wakati?
Naomba Rais wetu awekewe ulinzi wa ziada kwani watu hawa ni wengi waliojipanga kumuangamiza raisi wetu. Lakini sisi watanzania tuko imara na tunakutia moyo na shime Rais wetu uendelee kuchapa kazi kwani wabaya huwa hawakosekani dunia hii. Mwisho wao ni aibu.
Mtu ambaye alikataliwa na Halmashauri Kuu ya CCM mwaka 2015 amepata wapi ujasiri na nguvu ya kufikiria kuwa bado anakubalika ndani ya chama? Lazima kuna genge ambalo linatumia mbinu chafu ya kumuondoa raisi wetu madarakani kabla ama karibu na uchaguzi 2020.
Wana CCM na Serikali lazima tujiulize na kumfuatilia kwa karibu Mhe Membe na kama itabainika anatumia mbinu zinazo hatarisha amani ya nchi yetu ikiwemo usalama wa raisi wetu akamatwe na afikishwe mahakamani haraka kwa uhaini.
Wapi keshawahi tangaza ana nia ya kugombea 2020!,Kama aliyepo aanafanya Kazi vizur i Na anakubalika hovu ya nn kuhofia kushindanishwa?