MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Jumla ya miradi mitano kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Songwe ambayo inatarajiwa kauanza oktoba nne mpaka oktoba tano mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jeneral Nicodemas Mwangela akiongea na vyombo vya habari alisema katika ziara hiyo ambayo ni ya kwanza toka aingie madarakani mwaka (2015) kuwa Rais atatembelea miradi mbalimbali kuanzia oktaba nne katika wilaya za Mbozi na Momba ambapo mradi wa maji, barabara,ujenzi wa hospitali ya mji wa Tunduma, kiwanda cha kahawa na mradi wa kutoa huduma kwa pamoja mpakani mwa Tanzania (Tunduma) na Zmbia (Nakonde).
Alisema akiwa wilayani Mbozi oktoba nne (4) mwaka huu Rais atatembelea na kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa maji wa Mantengu Vwawa ambao unategemewa kutatua changamoto ya maji katika mji wa Vwawa na kuzindua kiwanda cha Kahawa cha GDM Mlowo.
Oktoba tano (5) Rais Dk John Magufuli akiwa na Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu watazindua kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani mwa Tanzania (Tunduma) wilayani Momba na Zambia Nakonde.
Mwangela alisema pia Rais wa Jamhuri ya Muungano atamalizia ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa ujenzi hospital ya mji wa Tunduma na katika Mradi wa wa ujenzi wa Barabara ya Mpemba -Isongole Wilayani Momba.
Aidha Mwangela aliwataka wananchi wote mkoani Songwe kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye anayetekeleza miradi yote ya maendeleo kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuuanzisha mkoa wa Songwe.