Rais Magufuli kuunguruma Kilimanjaro sherehe za Mei Mosi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
mount-kilimanjaro-2.jpg

Moshi.Rais John Magufuli amethibitisha kuwa atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambazo kitaifa zitafanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza kwa niaba yake, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki amesema kuwa Rais atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo,hivyo wananchi na wafanyakazi wajitokeze kushiriki na kusikiliza hotuba yake.

Sadiki amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na huduma za upimaji wa afya zilizoandaliwa na taasisi za afya hivyo aliwataka wakazi wa mkoa huu na watakaofika kutumia fursa hiyo kupima afya zao.

Chanzo: Mwananchi
 
Kiiirrrruuu... Hana jipya juz tu ametoka kuwapiga biti viongz wa wafanyakaz ikulu sijui kama ana cha maana tutegemee yaleyale matusi yake ya siku zote...
Haajiri hapandish watumish madaraja hajalipa malimbkizo...
Huyu mtu anahis kama anaongoza wafu vile
 
Mkulu hajawahi kufika Moshi toka achaguliwe zaidi ya kupita tuu akiwa anaenda Arusha au Mikoa mingine ya Kanda ya kaskazini. Acha aje kujionea uzuri wa mkoa wa Kilimanjaro na watu wake
 
Kwani huku Mbeya,Iringa,Ruvuma na Njombe tulikukosea nini Mheshimiwa Magufuli.... Maana hujawahi kukanyaga toka uapishwe.
 
Back
Top Bottom