Siasa Basi
JF-Expert Member
- Jul 10, 2016
- 1,493
- 4,276
Mwaka huu lazima wasome namba kwa herufi kubwa.Mtoa mada nakupongeza kwa dhati kabisa, kwani kwa asilimia kubwa upo sahihi kabisa. Nchi hii watu wengi wanataka mambo makubwa na ya kifahari huku wakiwa wamekaa tu bila hata kujishughulisha kwa namna yoyote ile. Ni watu wenye kuilalamikia serikali kwa kila jambo bila aibu. Ni kizazi kilichokosa uvumilivu na kisichojituma. Ili kubadili hali na mtazamo wa watu wa nchi hii ili wawe wachapakazi ilikuwa ni kumweka madarakani RAIS ambaye ni KOMANDOO, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wote wa ngazi mbalimbali wawe ni wanajeshi na nchi iongozwe kijeshi japo kwa miaka michache tu. Kwa kufanya hivyo bila shaka nchi ingeweza kupiga hatua za maendeleo siku hadi siku. MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI, MUNGU AKUONGOZE, AKULINDE, AKUTIE NGUVU, AKUPE HEKIMA, BUSARA NA UJASIRI ili uweze kuliokoa taifa hili katika janga la umaskini, uvivu, ufisadi, wizi, uzembe, ubinafsi nk.