BM Pesambili
Senior Member
- Jul 10, 2016
- 102
- 624
Naililia nchi yangu Tanzania , kila nikitafakari machozi yananitoka nakosa majibu nabaki kujiuliza tutafika kweli? Magufuli kazi unayo sana kuongoza kizazi hiki cha vilaza pole sana!
Limekuwa taifa la ajabu ajabu sana, viongozi wake (UKAWA & CCM)wamekuwa wanafiki, wazandiki, waongo hawaaminiki tena katika jamii. Wameruhusu kiburi na jeuri kuwavika kama mkufu shingoni mwao. Wana mawazo na mapenzi machafu mioyoni mwao. Kila kiongozi amekuwa muongo tu, kauli na videndo haviendani, ni wasaliti wa kwanza wa kauli zao wenyewe. Walimtangaza mchafu nchi nzima watanzania wakaamini hivyo gafla wakageuka tena kumtangaza msafi nchi nzima watanzania wakaamini tena hivyo bila kuwaoji kauli zao zile za mwanzo walizozisaliti wenyewe. Nchi imekuwa ya wanafiki sana hii. Tumekuwa jamii ya watu wa ajabu sana, tumebaki kuangalia mambo juu juu tu, na kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu , jamii iliyojaa wapuuzi na wanafiki wengi.
Kila kukicha upendo unapungua baina ya watanzania, visasi, dhuluma, wizi, ubakaji, ufedhuli, majivuno, matabaka, ukada na umasikini unazidi kutumaliza. Ee Mungu wetu tusaidia kizazi hiki cha vilaza. Tumebaki kuabudu watu weupe na vitu vyao na uchafu wao wote. Tumekubali kuporwa utu wetu na kufanywa vivuli vya wazungu kiasi cha kupoteza hata utamaduni wetu.
Tumekuwa na vijana na wasomi wa hovyohovyo, kushinda kwenye mitandao kuanzia asubuh mpaka jioni kuangalia vipicha vya uchi uchi na ngono( ponograph), Kutukanana na kupost vipicha vya kipuuzi kwenye mitandao. Vinguo vyao wanavyovaa vya ajabu visizo hata maadili. Wanapenda vimagazeti na vijarida vya ngono ngono tu. Mada za mapenzi na mambo ya kipuuzi yanapewa kipaumbele kuliko hata mambo ya kitaifa. Kwenda kulima na kufanya kazi hawataki, viwanda vitakuja kwa muujiza gani?
Magufuli Rais wangu pole sana kuongoza jamii ya mashoga na wasagaji, wavuta bange na madawa ya kulevya. Mandanguro kila kona yamejaa madada poa na makaka poa wanashindania wateja na bahati mbaya wateja wao wengi ni viongozi wetu hawahawa wanaopiga marufuku mchana usiku ndio wateja wao. Taifa lawanafiki sana hili.
Makanisa na misikitini kwetu kama kimbilio na msaada kwa matatizo haya lakini huko ndiko kuna balaa. Hii ya makanisa niache nitaleta mada yake baadae maana inahitaji hekima ya Mungu sana kuijadili. Tumekuwa na uelewa finyu hata katika masuala ya msingi yanayohusu taifa letu, uelewa finyu unatufanya turubuniwe kirahisi au tuelekeze nguvu zetu kwenye mambo ambayo yanaonekana katika nyuso zetu kama ndio utatuzi wa matatizo yetu kumbe ni upuuzi.
Tuna wasomi wengi lakini wameshindwa kujiamini na kujisimamia. Wamekuwa ndio chanzo cha matatizo yetu. Wameshindwa kabisa kujitambua, kudadisi, kujituma, kuwa wabunifu, kupenda kazi, kuwa na mwenendo na maadili mema kama mfano kwa jamii. Wakulima , wafugaji na wavuvi wetu wataendelea kuwa maskini kwa sababu vijana wao baada ya kupata elimu yao ya vyeti wanakimbilia mjini, kutafuta kazi ya viyoyozi na kuvaa Suti. Hawataki kusikia tena habari ya kilimo wala ufungaji, kutwa nzima mitaondaoni na handfone masikioni. Bahati mbaya ajira zenyewe zimeota mbawa. Kizazi hiki kimekuwa kizazi cha hovyo sana kuwahi tokea.
Tanzania yangu jamani umerogwa na nani? Ngoja nishie hapo maana kadiri ninavyoandika machozi yananitoka. Magufuli Rais wangu pole sana. Naomba Mungu akujalie hekima uvumilivu na busara.
Boniphace .M. Pesambili.