Aaron
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 3,019
- 4,693
Habari zenu wanajukwaa.
Hili andiko ilibidi nilipeleke jukwaa la elimu ila ni vyema lijadiliwe hapa kwa kuwa huyu anayeivuruga elimu ni mwana siasa.
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu niliyeadiliwa kwa mfumo TCU online.
Juzi baada ya jpm kutoa kauli yake juu ya TCU kuwapangia vyuo wanafunzi wasio vitaka. Ila ukweli ni kwamba tcu haiwezi kumpangia mwanafunzi chuo ambacho hakuchagua na kikubwa zaidi inamsaidia mwafunzi aliyekosa ushindani kwa vyuo ulivyovichagua. Hili linaeleweka na waliodahiliwa kwa mfumo huu watanisaidia kuongezea hapa.
Sasa baada ya kauli ya Rais wakati akifungua mabweni pale udsm. TCU wameamua isiwe shida kila chuo kipokee maombi na kupeleka TCU baadae. Kwa jicho la haraka ni kwamba wanafunzi wengi watakosa vyuo na udahili huu utakuwa mgumu sana.Mfano leo chuoni kwetu wametoa tangazo la kuanza kupokea maombi na ada ya maombi ni elfu 50.
Ina maana kama unataka kuomba vyuo zaidi ya kimoja ili kujiweka kwenye mazingira ya kutokosa chuo itabidi ulipie fomu ya kila chuo.. Wakati tcu online tulikuw tunalipia elfu 50 na kuomba vyuo vitano.
Sasa ili uombe vyuo vitano itabidi utumie 250000 hapo bado huna uhakika wa kupata nafasi kulingana na ushindani wakati tcu ulikuwa unalipia mara moja elfu 50.
Mapungufu ya mfumo huu ni mengi na hapa vyuo lazima vifanye udanganyifu na kuwadahili wanafunzi wasio na sifa. Yale ya miaka ya nyuma yanajirudi.
Serikali mjirudi na TCU waendelee kufanya udahili huu.. Na mapungufu yatakayojitokeza muwahukumu hawa TCU.