Rais Magufuli: Kama una korosho na huna shamba hutalipwa

Inatia hasira sana
 
Hakuna indicator ya matumaini mbele,
Tulia kidogo, hebu fikiria ukipeleka kitambaa cha nguo kwa fundi...ile anaanza kukata kata huwezi elewa nini kinatokea baadae! jamaa naona anakata kata! Hizi hela za madalali wa kangomba ndio huwa zinawanunulia mama zetu kanga na vilemba vya "Chagua CCM" matokeo tunawakilishwa na akina ......ndiyoooooooo!
 
Aliyetapeli ni dalali aliyefata mkulima akanunua kilo 200 yeye akaenda kuuza 3200.. Nipo pamoja na rais wangu.. Imefika kipindi mkulima afaidike na wala si wajanja wajanja wachache
Kwann wanunue korosho za utapeli kwann wasiende nunua shambani
 
Wasiache kulima kitafufuka tena Giza likipita
 
Ni mpaka 2027 penda usipende, majiizi na wapiga madili waendelee kulia tu! 2025/2026 tutashuhulika na katiba mpya, 2027 ndiyo itumike kwa uchanguzi mkuu(general election)! In short Dr Magufuli ni mpaka 2027. 2020 anapita bila kupingwa!
Tunaomba wakati inashugulikiwa hiyo katiba asiwepo huyu mkuu... Tutavumilia tu mpaka 2025 ila si zaidi ya hapo.
 
Hawa viongozi Hivi hawajawahi kuishi maisha ya kawaida ya huko vijijini unakuta mkulima wakati wa kuandaa shamba Lake hana hela anakwenda kukopa kwa hao kina kangomba?

, wamejiandaa kuwakopesha. Wakulima wakati watakapokuwa na uhitaji?
Ndio maana wanasema kweli serikali ni chombo cha mabavu.
 
Thus hana BARAKA kwa kila afanyalo linafail
Jamaa ni dhulumati sana mpaka rambirambi anachikichia huyu mtu sembuse awalipe korosho?Hao wakulima wasikilizie maumivu.Na hiyo hela ya mauzo ya korosho hata mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali anaweza asizione kwenye hesabu zake!
 
Kiuhalisia huu ni unyang'anyi,kwani hata hao kangomba hakuna anaemfuata mkulima kwa rungu bali mkulima anauza kwa maridhiano.Na pia iwapo kangomba utapita mashambani na bei ndogo hakuna atakaekuuzia.

Hebu kwanza tujenge hoja,leo hii mkulima anaanza maandalizi ya shamba mwezi wa 8 lakini pesa ya mauzo ya kwanza ya korosho huanza kupatikana mwezi wa 11.Mkulima ni mtu wa Hali ya chini na Serikali haijamuwekea utaratibu wa kukopeshwa pesa ya kujikimu kipindi cha maandalizi ya mashamba, hivyo korosho zake lazima kidogo aziuze ili apate pesa ya kujikimu na zilizobaki atazipeleka ghalani.

Hivyo kwa mantiki nzima kangomba ni mkombozi wa mkulima na si mnyonyaji,kwa maana bila kangomba hakuna uzalishaji. Mkulima anafahamu fika kangomba huwa na bei ndogo kuliko bei za minadani lakini mpaka anaridhia kuuza kwanini serikali haijiulizi swali?

Serikali itafute mbinu za kuwalinda wote,mkulima na kangomba.Lakini si kutumia nguvu kwa kuwataifisha ilihali mauziano yao ni maridhiano na hakuna mkulima aliejitokeza kulalamika.
 
Ingependeza kweli wanaochati katika huu uzi wakaacha kuchati kwanza tukawaeleza ukweli watawala wasiozingatia maisha ya wenzao katika maamuzi yao!. Hii ishu ni serious mno kwa mustakbali wa wananchi na Taifa

Watu tulisha Sema sana kuhusu huyu Mkuu wa Nchi juu ya Maamuzi yake lakini wapiga vigelegele wakatuita Majina kibao ili tu kumpamba Mtu wao.Ile Ajali ya Luck Vicent Arusha na Tetemeko la Ndugu zetu kule Bukoba maamuzi yalio tolewa mwenyewe uliona.Hapa ni kama anapita mule mule na bado Watu wanakaa kimya tu.

Kuna Watu Maisha yao yame badilika/yame pinduka kuanzia alipo itoa Kauli yale ,anatuumiza na kutuonea sana sisi Raia na analijua hilo..
 
Ni dhulma ya wazi iliyopewa jina lililorembwa la kumkomboa Mkulima ili kuuzuga umma udhani eti hizi moves ni kwa ajili ya kumsaidia mkulima kumbe hamna kitu!

Wanajifanya eti kumuonea huruma mkulima dhidi ya madalali wa Kangomba, Ni lini Mkulima amewahi kulalamika kuwa Kangomba ni shida kwake?
Madalali wa Kangomba hawamshikii fimbo wala bunduki mkulima, Mkulima yeye mwenyewe kwa ridhaa yake anauza mali yake, sasa serikali kwa nini iwanyang'anye watu wa Kangomba Korosho zao walizozinunua kwa maridhiano kutoka kwa mkulima?

Serikali ina haki ya kununua korosho kwa mkulima lakini haina haki ya kuchukua na kushikilia korosho za watu waliozinunua kwa haki kutoka kwa mkulima!
 
Kuna haja ya kutengeneza kuliko kubomoa bora to wakanunua kwa FEDHA kangomba walizonunulia na sio kutaifisha jamani ataua watu baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…