Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Raisi Magufuli anasema RPC Mbeya afukuzwe kazi. Raisi Magufuli anaweza kutuambia kosa la RPC kwa ajali hii ya Mbeya ni nini hasa? Au ni ile kawaida ya kutoa kauli za kisiasa kwa jambo ambalo sio la siasa?
Kama kuna mtu wa kukukuza kazi basi ni Meneja wa Tanroads wa Mbeya, Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkurugenzi wa jiji.
Kazi ya Traffic Polisi ni kusimamia usalama wa barabarani kulingana na miundo mbinu iliyopo, sio ku-design miundo mbinu ili ajali zisitokee. Hapo ndipo utaona Raisi Magufuli anahitaji ushauri kabla ya kutoa matamko ya kisiasa kwa matukio nchini yasiyo ya kisiasa.
Tuangalie tukio la ajali. Hizi kauli za lori kufeli breki ni za kiasiasa na uongo. Ukweli ni kwamba wakati lori likishuka huu mteremko, kuna Hiace ailijaribu ku-overtake coaster na ikakutana na hili lori likishuka. Hapo ndipo kimbembe kilipoanza katika harakati za kukwepa na kukwepana, na kusababbisha ajali yote. Hakuna dereva wa lori la mzigo mwenye akili atashuka huu mteremko kwa kasi. Ni mteremko mkali ambao kila dereva wa lori anajua anapaswa kushuka kwa low gear zikisaidiana na breki, kwa hiyo suala la kusema lori likikuwa likienda kasi ni za kutunga.
Sasa Meneja wa Tanroads Mbeya, Mkurgenzi wa Jiji na Mkuu wa Mkoa wote wanajua hili ni eneo la hatari sana, kwanza kila wakati wanapita njia hii kwenda Songwe airport. Hawaoni kuwa angalau hata walipaswa kuweka climbing lane kwenye hili eneo baada ya ajali nyingi sana na watu wengi kufa katika sehemu hii? Si mara ya kwanza, nadhani mtakumbuka huko nyuma gari ya mbunge ilipata ajali hapa na kuungua na watu kadhaa kufa, sababu zikiwa zile zile ku-overtake sehemu hii.
Na pia Mbeya kwa sasa hii barabara ya Tanzam kuanzia eneo la Uyole ni tatizo. Ina msongamano mkubwa wa magari unaoweka hatarini waenda kwa miguu na magari. Nilishaweka post humu ndani kwamba hili ni tatizo linakua kila siku. Siku nyingi sana niliweka post humu JF na kuuliza kama Tanroads hawalioni hili tatizo, ukizingatia Mbeya ni jiji, na nikatoa pendekezo barabara double (dual carriageway) ijengwe kuanzia Uyole hadi Mbalizi. Kama ushauri huu ungefuatwa vifo vingi sana eneo la mteremko wa Mbalizi vingeepushwa.
Ushauri nilioweka hapo nyuma;
Mbeya msilale, shurutisheni serikali iwatengee fedha za kupanua barabara ya Tanzam eneo la Mwanjelwa hadi Mbalizi
Kwa msisitizo, kama Raisi Magufuli anataka kutumbua watu kutokana na hii ajali basi wanaopaswa kuwajibishwa ni Meneja wa Tanroads, Mkurugenzi wa Jiji na Mkuu wa Mkoa. RPC mnamwonea tu.