Rais Magufuli, hii nchi itakutia uchizi

Rais Magufuli, hii nchi itakutia uchizi

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,587
Reaction score
28,750
Rais wangu Magufuli, hakika hii nchi kama una nia ya kweli ya kuirekebisha, soon itakutia uchizi, awamu na nne ilitotangulia imefanya madudu ya kutisha ukiamua kuyafuatilia kwa makini unaweza geuka chizi siku za hivi karibuni.

NSSF imeripotiwa na gazeti la Mwananchi imeitia serikali harasa ya zaidi ya Trillioni 1.33 katika miradi yake miwili tu ya Kigamboni(sio daraja) na Arumeru kati ya mingi iliyonayo , mradi wa Ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni zaidi ya Tshs Billioni 179 zimepigwa na wajanja wachache, ardhi imenunuliwa kwa Tshs Millioni 800 kwa hekari badala ya Tshs millioni 39, huko Arumeru ardhi imenunuliwa kwa Billioni 1.8 kwa hekari badala ya Tshs laki 5 ikizidi sana Millioni 1.

Barrick Gold Mine kwa miaka minne tu nyaraka zinaonyesha imeingiza zaidi ya Tshs Trillioni 1.79 huku kwetu inadai kuwa haijawahi kuingiza hata senti moja kwa kuwa ilikuwa inapata hasara kubwa(ilikua ikijiendesha kwa hasara), cha ajabu mtangulizi wako alikua kila siku akiisifia kwenye majukwaa.
Leo tunakwenda mahakamani tunaishia kulipwa billioni 89.

Wamarekani wanasitisha misaada yao kwa ishu ya uchaguzi wa Zanzibar, Mchina na Mjapani walivyoonekana kuanza kujisogeza sogeza, leo msemaji wa MCC anadai kuwa serikali iende "kuzungumza nao vizuri" na ukienda na "hoja nzuri" na "za kuridhisha" ,wanaachia mpunga, wao "hawana shida", wanapoulizwa vipi kuhusu ile ishu ya Zanzibar mliyodai ndio sababu ya kusitisha msaada wanakataa kuiongelea kabisa, wanaipotezea kimya kimya, wanadai ajenda andaa tu wewe hawakuchagulii na wako tayari kurejesha hizi hela "ukizungumza nao tu vizuri".

Bandari kumeoza, zinaibwa mpaka meli, makontena zaidi ya 11,000 yanayeyuka mchana mchana, na mengine ya flow meters.

Huko bungeni napo wabunge wanakula rushwa utadhani mtu anatafuna karanga mbichi, wabunge wetu tuliowatuma watutetee wana mpango wa kuivunja EWURA kisa inawabana bana kwenye ishu zao za kukwepa kodi kwenye biashara zao za mafuta.

Ishu za madawa ya kulevya nazo zimepamba moto, kinara wa dawa za kulevya Shikuba kakamatwa kaweka gerezani, inadaiwa anaishi kama mfalme huko magarezani, "mfungwa anakula mpaka kuku" ?? nani kazipeleka kuku rosti huko gerezani??
mpaka mkuu wa magereza anaogopa, kamati ya bunge ilivyoenda kumtembelea akaomba aongezewe ulinzi la sivyo Shikuba aondolewe mana kamzidi uwezo.

Hebu angalia timu yako iliyoko hapo ikulu upya, iko upande wako kweli??.
Sio wao waliokuwa wanufaika wakubwa wa haya mambo??

Mukulu aisee, hii nchi hii ukiamua kuifumua sana, soon itakutia uchizi.
 
Kujenga nchi ni jambo lisilo na mwisho.

Hakuna siku itafika tutakuwa tumetatua matatizo yote.

Changamoto ni sehemu ya kawaida ya maisha.

Cha msingi ni kuzibabili changamoto kimkakati endelevu.

Kazi ya ujenzi wa taifa ni kukabidhiana vijiti, kiongozi kwa kiongozi, kizazi kwa kizazi...
 
Katika suala la "kujieleza vizuri" ndo nadhani jembe Magu hatafanya.

Huu ni upuuzi ulioelezwa na Nyerere, Mwinyi na mkapa, kusema kwamba tutafanikiwa kimaendeleo kwa kutembeza bakuli. lazima tujifunze kujitegemea kama mjomba Magu anavyosema..tuna kila kitu na kwa nini tuwe masikini? kwa nini tuombe

Magu usiende we kaa tujenge nchi, if need be, wao ndo waje
 
Masikini Tanzania! Pole Bwana Magufuli, Wanyachusa wasema "Kyala alipo!"
 
nchi hii ilikuwa inamuhitaji mtu aina ya Magufuri tu. Na tuna baht tumempata tumuombee na tuendelee kumsapoti atatufikisha wengi kaanani
 
Rais wangu Magufuli, hakika hii nchi kama una nia ya kweli ya kuirekebisha, soon itakutia uchizi, awamu na nne ilitotangulia imefanya madudu ya kutisha ukiamua kuyafuatilia kwa makini unaweza geuka chizi siku za hivi karibuni.

NSSF imeripotiwa na gazeti la Mwananchi imeitia serikali harasa ya zaidi ya Trillioni 1.33 katika miradi yake miwili tu ya Kigamboni(sio daraja) na Arumeru kati ya mingi iliyonayo , mradi wa Ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni zaidi ya Tshs Billioni 179 zimepigwa na wajanja wachache, ardhi imenunuliwa kwa Tshs Millioni 800 kwa hekari badala ya Tshs millioni 39, huko Arumeru ardhi imenunuliwa kwa Billioni 1.8 kwa hekari badala ya Tshs laki 5 ikizidi sana Millioni 1.

Barrick Gold Mine kwa miaka minne tu nyaraka zinaonyesha imeingiza zaidi ya Tshs Trillioni 1.79 huku kwetu inadai kuwa haijawahi kuingiza hata senti moja kwa kuwa ilikuwa inapata hasara kubwa(ilikua ikijiendesha kwa hasara), cha ajabu mtangulizi wako alikua kila siku akiisifia kwenye majukwaa.
Leo tunakwenda mahakamani tunaishia kulipwa billioni 89.

Wamarekani wanasitisha misaada yao kwa ishu ya uchaguzi wa Zanzibar, Mchina na Mjapani walivyoonekana kuanza kujisogeza sogeza, leo msemaji wa MCC anadai kuwa serikali iende "kuzungumza nao vizuri" na ukienda na "hoja nzuri" na "za kuridhisha" ,wanaachia mpunga, wao "hawana shida", wanapoulizwa vipi kuhusu ile ishu ya Zanzibar mliyodai ndio sababu ya kusitisha msaada wanakataa kuiongelea kabisa, wanaipotezea kimya kimya, wanadai ajenda andaa tu wewe hawakuchagulii na wako tayari kurejesha hizi hela "ukizungumza nao tu vizuri".

Bandari kumeoza, zinaibwa mpaka meli, makontena zaidi ya 11,000 yanayeyuka mchana mchana, na mengine ya flow meters.

Huko bungeni napo wabunge wanakula rushwa utadhani mtu anatafuna karanga mbichi, wabunge wetu tuliowatuma watutetee wana mpango wa kuivunja EWURA kisa inawabana bana kwenye ishu zao za kukwepa kodi kwenye biashara zao za mafuta.

Ishu za madawa ya kulevya nazo zimepamba moto, kinara wa dawa za kulevya Shikuba kakamatwa kaweka gerezani, inadaiwa anaishi kama mfalme huko magarezani, "mfungwa anakula mpaka kuku" ?? nani kazipeleka kuku rosti huko gerezani??
mpaka mkuu wa magereza anaogopa, kamati ya bunge ilivyoenda kumtembelea akaomba aongezewe ulinzi la sivyo Shikuba aondolewe mana kamzidi uwezo.

Hebu angalia timu yako iliyoko hapo ikulu upya, iko upande wako kweli??.
Sio wao waliokuwa wanufaika wakubwa wa haya mambo??

Mukulu aisee, hii nchi hii ukiamua kuifumua sana, soon itakutia uchizi.
[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji15] [emoji15] [emoji15]post murua sana
 
Magu piga kazi kwani uliomba kazi tumekupa! Wengine hatukuwapa kwasababu hawakuwa na nia thabiti ya kutuondolea miungu watu katika nchi yetu!
 
Kote kutasafishwa hata huko ufipa pia hakuna kitakachoachwa bila kusafishwa...
 
Back
Top Bottom