Rais Magufuli hawezi kuwa sahihi katika hili la mikopo chuo kikuu

Hivi ni saidie kwanza tajili ni yupi?,Na madikini ni yupi?....harafu ndipo nitachangie zzaidi.

Ni rahisi tu, tajiri ni yule mwenye uwezo wa kuchagua, na masikini hana huo uwezo yeye atachukuwa kinachopatikana kwa wakati huo na kikikosena basi hawezi kwenda mbele, hivyo basi ni lazima Serikali imsaidie ili aweze kwenda mbele, huyu anayeweza kcuhagua ana njia nyingi na hahitaji msaada wa serikali ukiwepo sawa usipokuwepo pia sawa na anweza kuendelea na masomo!

Hivyo kwenye kusomeshwa na Serikali Chuo Kikuu logic iliyopo ni kwamba kama huyu aliweza kusoma kuanzia shule ya msingi mpaka A-level bila msaada wa Serikali kwa nini washindanishwe kwenye mizani sawa na mtoto aliyesomeshwa na Serikali kwa sababu ya kukosa uwezo?
 
umejenga sana hoja ila kuna kitu umesahau

una shilingi 1000 wamekuja watu wawili kukuomba hiyo 1000 hawajala chakula wana njaa.. mmoja ni mlemavu na mwingine mzima na wote hawajala wanaiomba hiyo buku.. je utampa nani?

Kwa kuwa njaa haina ulemavu muungwana atanunua msosi kulingana na kiasi hicho na kuwa gawia wote, kama msaada ingekuwa baiskeli ya miguu mitatu basi yule mzima ahaimuhusu. Ukiua mzima kwa njaa ukasaidia mlemavu kesho na mlemavu atavuta kwa kukosa msaada.

Hapa ndio mawazo yenu yanapogota, kufikiri nje ya box sio mchezo, mnapolazimisha kuinua maskini na kukandamiza wenye uwezo in the short run it helps lakini kwa mbaali mnapiga marktime tu!
 
Namshukuru wanangu hawatadaiwa lakini nimeungulia kwa kusaidia serikali wajibu wake wa kusomesha Taifa lake napeleka maombi kwa Mungu amwambie mwalimu Mbona hakutuambia pesa alizotusomesha bure tungekuja kudaiwa tena kwa mateso.
 
JPM hajawahi kuongea kitu kwa bahati mbaya, nionavyo mimi ni mkakati wakupunguza fungu bodi ya mikopo, pia ni mkakati wakupunguza idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu..
Wazazi na wazazi watarajiwa tujipange tu kusomesha kwa pesa zetu wenyewe..
Kwa sasa gharama za mkopo kwa 100 % wanafunzi wanapata pesa ngapi? Mie mhenga nilimaliza miaka ya zamani kidogo. Mwenye kufahamu hili atujuze ili tuweze kujiandaa mapema kwa ajili ya wanetu.
 
umejenga sana hoja ila kuna kitu umesahau

una shilingi 1000 wamekuja watu wawili kukuomba hiyo 1000 hawajala chakula wana njaa.. mmoja ni mlemavu na mwingine mzima na wote hawajala wanaiomba hiyo buku.. je utampa nani?

Nitawagawanyisha mia tano tano..manake njaa haichagui na haina mbadala...
 
Ni rahisi tu, tajiri ni yule mwenye uwezo wa kuchagua, na masikini hana huo uwezo yeye atachukuwa kinachopatikana kwa wakati huo na kikikosena basi hawezi kwenda mbele, hivyo basi ni lazima Serikali imsaidie ili aweze kwenda mbele, huyu anayeweza kcuhagua ana njia nyingi na hahitaji msaada wa serikali ukiwepo sawa usipokuwepo pia sawa na anweza kuendelea na masomo!

Hivyo kwenye kusomeshwa na Serikali Chuo Kikuu logic iliyopo ni kwamba kama huyu aliweza kusoma kuanzia shule ya msingi mpaka A-level bila msaada wa Serikali kwa nini washindanishwe kwenye mizani sawa na mtoto aliyesomeshwa na Serikali kwa sababu ya kukosa uwezo?
Sidhani kama uko sahihi sana, je? Unajua kuwa zipo private za laki sits,,,day,,,ambapo walio wengi wanaweza kuzimudu?,,,je? Unajua kuwa kuna wazazi wana uwezo wakutisha Na anaweza akafanya uchaguzi atakavyo lkn yuko shule ya serikali....huyu naye unamusemaje?,,,,,je? Unajua kuwa kuna watoto wanasoma shule binafsi...pengine tu ni msaada wa muda.
 
Ndiyo private schools ni kipimo cha utajiri, Dunia nzima ni hivyo, mtoto wa masikini hawezi kuchagua akasome wapi bali atasoma Shule za Serikali tu kwani ndizo zilizopo kwake, ile tu kwamba unaweza kuchagua ina maana wewe siyo masikini!
Kwa maana nyingine kesho walimu wote wakigoma hata mwezi mtoto wako wa private ataendela kusoma lkn wa Shule za Kata hatasoma na hakuna kitu atafanya!
Sawa mkuu. Kusomesha private school ni utajiri kabisa
 
Sidhani kama uko sahihi sana, je? Unajua kuwa zipo private za laki sits,,,day,,,ambapo walio wengi wanaweza kuzimudu?,,,je? Unajua kuwa kuna wazazi wana uwezo wakutisha Na anaweza akafanya uchaguzi atakavyo lkn yuko shule ya serikali....huyu naye unamusemaje?,,,,,je? Unajua kuwa kuna watoto wanasoma shule binafsi...pengine tu ni msaada wa muda.

Haijalishi bado unahitaji uwezo kuweza kuchagua mtoto wako asome Shule ipi, lkn kuna Watoto wengi wa Kitanzania hawana huo uwezo na njia pekee ya wao kusoma ni uwepo wa Shule za Serikali hivyo hawa walipaswa wapewe upendeleo na kuwaweka sawa na watoto wengine ambao wana uwezo wa kusoma hata kama hakuna Shule za Serikali siyo haki, hivyo naungana na Raisi Magufuli kwa 100%!
 
Sawa mkuu. Kusomesha private school ni utajiri kabisa

Ndiyo , kwa maana unaweza kuchagua, mwingine angependa pia kuchagua lkn hawezi kwa sababu hana huo uwezo, hivyo ni jukumu la Serikali kumpa upendeleo huyu mtoto asiye na uwezo wa kuchagua!
 
Hakuna nchi yoyote ile Dunia hii ambapo Serikali hutumia fedha zake kulipia watoto wa matajiri kusoma Chuo Kikuu, nchi zote Duniani Serikali hugharamia masikini kwanza kwani matajiri wana uwezo wakujigharamia!

Kweli cherehani 4 ni kiwanda!? yaani hapa umejitutumua kusomesha mtoto tusiime we ni tajiri, ada zenyewe watu wanaungaunga hatare. Hiyo dunia uliyokuwemo wewe ni nouma saana.
 
Kweli cherehani 4 ni kiwanda!? yaani hapa umejitutumua kusomesha mtoto tusiime we ni tajiri, ada zenyewe watu wanaungaunga hatare. Hiyo dunia uliyokuwemo wewe ni nouma saana.

Tofauti ni kwamba unaweza kuunga unga na kuipata mwingine hawezi na hawezi kuchagua ili aweze kusoma ni lazima Shule za Serikali ziwepo vinginevyo hawezi kusoma, hiyo ndiyo tofauti, yaani kuna watoto wengi Tanzania hawana wa kuwapigania kama Serikali ikiwaacha wanaangamia, hivyo ni lazima wapewe upendeleo maalumu!
 
Ndiyo , kwa maana unaweza kuchagua, mwingine angependa pia kuchagua lkn hawezi kwa sababu hana huo uwezo, hivyo ni jukumu la Serikali kumpa upendeleo huyu mtoto asiye na uwezo wa kuchagua!
Kwahiyo saizi ni MIKOPO KWA WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KWAAJILI YA ELIMU YA JUU???????
 
Mimi katika hili nadhan wangeorodhesha shule zote zile za kishua za private kama loyola, cannosa, feza, alfa, st mathew na saits zooote, pamoja na shule nyingine za kishua shua ambazo sijazitaja ndio wawanyime mkopo the rest wote wapate mkopo kwakuwa wapo waliokosa c labda moja kujiunga shule za serikali hvyo anaamua kwenda private ya bei za kiloko kabisa.
 
Kwa hiyo aliyesoma private ndiye mzima na aliyesoma serikali ndiye mlemavu.

Nimesema hiki ni kiwango kidogo kabisa cha kufikiri na nimetoa maelezo mengi na ushahidi mwingi kwamba unayemwita mlemavu anaweza asiwe mlemavu na unayemwita mzima anaweza asiwe mzima

Tatizo lako hutaki kuelewa kitu unacho kijua

Kwa kusema eti aliye mlemavu anaweza asiwe mlemavu ndio tayari umeshajihakikishia kwamba sio mlemavu

Utaratibu upo na unafatwa kwa kuhakiki hayo yote e.g yatima,mufisiri,wagonjwa n.k tena wanapitia serikali za mitaa kuhakiki ndio hata JPM alisema labda utuhakikishie wewe ni yatima

Hii yote ni njia ya kuleta msawazo katika jamii hasa kuhusu suala la usawa

Labda huseme kauli hizi zinaleta athari kwa shule za binafsi
 
Tusipende kuunga mkono kila jambo analosema rais. Hapa magu amechemka! Mkopo siyo fadhila ni haki ya kila mtanzania endapo atakuwa ametimiza vigezo kikubwa kikiwa ufaulu. Tunahitaji wataalamu wa kila aina na mtoto kusoma shule binafsi isiwe sifa mojawapo ya kukosa haki ya elimu ya juu. Tanzania sijui ni nani aliyeturoga! Nasikia kule Amerika wataalamu wengi ni Waisrael. Ina maana Amerika inachukua jukumu la kuwasomesha waisrael hata kama siyo raia wa amerika ila inategemea kunufaika kutokana na ugunduzi wao hapo baadae. Itakuwa jambo la ajabu mwanafunzi amesoma shule ya binafsi na kupata ufaulu mfano wa pointi 3 akose kwenda chuo kikuu na apelekwe wa pointi 10 kisa amesoma shule ya umma. Kusoma shule binafsi siyo utajiri wengi wanajinyima na mzazi aliyesomesha mtoto shule ya binafsi kwa kujinyima ni vigumu kumudu gharama za elimu ya juu.
 
Mtaani kwangu nimefatwa na wazazi 2 (hawa ni kwa uchache ninao wajua) wakiniomba niwatafutie kibarua watoto wao ambao wamerudishwa chuo kikuu kwa kukosa mkopo; mmoja alikua anasoma computer science na mwingine sikutaka hata kuuliza alicho kua anasomea; niliwaambia tu, "endapo kutakua na nafasi nitawaunganisha na boss wangu" Huyu aliyekua anasoma computer science O level alisoma shule moja ya ya day ya Roman Catholic, baba yake alikua anauza MAJI kwa watu wa mtaani kwake cause alikua na kisima akajenga na tank, changamoto ipo hivi; kwasasa hiyo biashara sio deal tena kwasababu serikali imeleta maji safi na salama kwenye hilo eneo so hana WATEJA tena; huyu mwingine ambaye sikutaka kujua alicho kua anasomea, yeye baba yake ni KADA mtiifu wa ccm, na ni balozi wa mtaani kwangu, masikini sana. Kijana alikua anasomeshwa na shemeji yake (mume wa dada yake) shule moja ya private (sina hakika na jina la hiyo shule) kwasasa huyo shemeji yake nae ana majukumu na ni mwanajeshi, nadhani watoto wake nae wameanza shule and hence having more responsibility and accountability, ndio hivyo wapo nyumani. Hao ni kwa uchache ninao wafahamu.
Visa kama hivyo havijaanza leo na kamwe haviwezi kuishi
 
Mimi katika hili nadhan wangeorodhesha shule zote zile za kishua za private kama loyola, cannosa, feza, alfa, st mathew na saits zooote, pamoja na shule nyingine za kishua shua ambazo sijazitaja ndio wawanyime mkopo the rest wote wapate mkopo kwakuwa wapo waliokosa c labda moja kujiunga shule za serikali hvyo anaamua kwenda private ya bei za kiloko kabisa.
Bado hujatatua tatizo..Kumbuka mtoto aliyesoma Feza ni mtanzania kama wewe. Hii itakuwa dhambi kubwa kumnyima haki yake ya elimu ya juu. Hela ya mkopo ni kodi zetu sote wala siyo hela kutoka mfukoni mwake.
 
Back
Top Bottom