Rais Magufuli fanya hivi uwasaidie Watanzania kipindi hiki kigumu Cha kukabiliana na Corona virus

Rais alivyosema juzi kwamba kila mtu afanye kazi sanaa kwani kuna uwezekano wa Njaa kali kutokea hukumuelewa!??

Maana yake nini, ukipata njaa ufe kivyako.. Ulishapewa tahadhari zote. Usitegemee back up yeyote toka serikalini. Hakuna hata mia mtapewa.

Chapeni Kazi.
 
Huu ushauri wako ni Mzuri, ukizingatia pia tayari kuna pesa zimechangwa na wadau wengi mbali na akiba ya maafa ambayo ipo siku zote serikalini.

Kama Tanzania na Rais wanajali watu wake wanapaswa watoe msaada wa kifedha au chakula japo kidogo hata kama hakuna Lockdown.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bujibuji, Mkuu Unajua ulaya watu walikua na hela Lakini walikufa kwa njaa, cha msingi Ni stoku Ya chakula chakutosha ikiwezekana maghala yaongezwe ,Kila familiar, Kila kijiji na Kila mkoa uwe na ghala za chakula chakutosha hapa tutapiga hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umeshauri vyema kiaina, ila tuna watu wapenda hela hivyo kuigawa bure haiwezekani, ni mafisadi wanaoipenda hela, wanaoamini bila kufanya kazi hupati hela!
 
Bilioni 8 kwa watu milioni nane ulosema basi kila mtu atapata elfu elfu sijajua hiyo milioni ulipiga hesabu za Polepole au?

Pia nakumbuka mara ya mwisho walisema laini zilizo sajiliwa ilikuwa milioni 24 sikufatiliaga tena hapo na ilikuwa mwezi wa kwanza hiyo.
 
Umeanza kujitambua ,safi sana
Mh Rais, pole na kazi.

Hapa pana ushauri mdogo tu wa namna ya kuwasaidia raia wako kupunguza movements na kuwapunguzia ukali wa maisha kipindi hiki kigumu kiuchumi na kiusalama wa kiafya pia.

Fanya filtering kwenye database ya biomedical TCRA, Kisha tupate namba ya watu waliojisajili. (Alama zako za usajili zitumike kukutambua).

Ukijulikana idadi, basi Kila mtu apewe sh. Million moja, najua waliojisajili hawazidi million nane, hivyo serikali itenge billion nane kutoka mfuko wa maafa wa waziri mkuu wapewe wananchi waliosajili line zao (tunaamini ni watu wazima wenye majukumu), Kisha funga bar zote, pubs, groceries, vilabu, mikusanyiko yote na starehe zote

Hii itapunguza mihangaiko, wale wenye biashara ndogo watakaa na kutulia majumbani na kuepuka hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona a.k.a kolona Kama tunavyoita uswazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bujibuji, watu milion nane, kila mtu apate milion moja hela itatoka wapi nyingi namna hiyo

8,000,000 X 1,000,000= 8,000,000,000,000, sawa na trilioni nane,

Haitakuja tokea kwa tanzania. Labda baada ya millenium moja ijayo.
 
Back
Top Bottom