Kutokana na kipindi hiki cha mpito cha Corona, Walimu changamkieni hii fursa

kigogo1ivi

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
534
323
Wengi tunatambua kuwa kwa sasa Dunia inapitia kipindi kigumu sana kutokana na hili janga la Corona virus. Hii kitu imegusa sehemu nyingi sana.

Naomba niweke wazo langu huenda likasaidia wachache nataka niguse sekta ya elimu kuanzia shule za awali mpaka sekondari.

Nimetafakari kwa kipindi hiki shule zote zimefungwa na hazijulikani zitafunguliwa lini wakati watoto wakisalia majumbani bila kupata msaada wa kimasomo kutoka kwa walimu. Ewe mwalimu unaonaje ukaandaa vipindi vyako kama kawaida na ukatafuta Tv station yoyote mtakayokubaliana kisha uanze kufundisha kupitia tv ukiweza unaweza fundisha hata kupitia na YouTube.

Nina imani ukiandaa kipindi cha nusu saa kinatosha kabisa na utatoa elimu kwa upana sana. Najua uandishi wangu ni mbovu lakini naimani nimeeleweka kwa mwenye mawazo zaidi anaweza kujazia.

Nawasilisha.
 
kigogo1ivi, Wazo zuri sana! Changamoto itabaki kwenye kupata wadhamini wa kipindi hicho au gharama ya kukilipia! Labda iwe katika mfumo wa kuuza kipindi kwa stations zilizotayari kununua

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukithubutu utaweza maana hata waanda vipondi wakiona wazo lako lina faida kwao ni rahisi kukupa kipindi na baada ya kipindi kuanza watapatikana wadhamini
 
Hii inahusu Wizara sio walimu. Mimi nimewaambia walimu wajiongeze

Hilo unalosema haliwezekani bila kuwa na organization ya wizara husika. Lakini kama ni tuition kwa makundi fulani tu na sio wanafunzi wa level husika kwa nchi nzima kunufaika, sawa.
 
Hilo unalosema haliwezekani bila kuwa na organization ya wizara husika. Lakini kama ni tuition kwa makundi fulani tu na sio wanafunzi wa level husika kwa nchi nzima kunufaika, sawa.
Tuition wanakamata mkuu ,huku tuliko mwalimu unakamatwa
 
Back
Top Bottom