Shirika la Afya Duniani lawaasa Wananchi kuzingatia mlo kamili na mazoezi kwa watu wazima kipindi hiki cha Corona

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Tedros Ghebreyesus ametaja vitu vitano ili kukabiliana na janga hatari la ugonjwa wa Covid-19.

Tedros alisema janga hili la Corona limeichanganya dunia na kufanya maisha ya kila mtu kubadilika na kwamba ili kukabiliana na tatizo hilo ni lazima kuwa vizuri kimwili na kiakili kwa kuzingatia vitu vitano, kwanza ni mlo kamili utakaosaidia kujenga kinga imara zitakazoweza kukabiliana na virusi vya Corona.

“Katika kipindi hiki cha mlipuko ni muhimu kuzingatia lishe sahihi yaani ulaji wa chakula ambacho ni mlo kamili, mtu mwenye hali nzuri ya lishe ana uwezekano mkubwa wa kuwa na kinga imara ya mwili na hivyo mwili wake unaweza kupambana na vimelea vya magonjwa ikiwemo virusi vya corona kwa kiwango kikubwa zaidi ukilinganisha na wengine,” alisema.

Alisema mlo kamili ni chakula chenye virutubisho vyote muhimu ikiwemo ni pamoja na wanga, protini, mafuta kiasi, madini joto, vitamini, mbogamboga na maji ya kutosha mara kwa mara.

Jambo la pili kwa wale wanywaji pombe aliwataka kupangilia unywaji wao na kuepuka kunywa kupita kiasi na pia kuitaka jamii kuepuka vinywaji vyenye sukari.

Tedros alisema kitu cha tatu cha muhimu ni kwa wale wavutaji wa sigara kuacha kipindi hiki cha janga la corona kwani sigara si nzuri kiafya na inamuweka mtu kwenye hatari zaidi iwapo atapata mambukizi ya virusi hivi corona.

Mkurugenzi huyo wa WHO pia alishauri watu wazima kufanya mazoezi kwa nusu saa kila siku huku watoto wakifanya kwa saa moja.

“Toka nje fanya mazoezi ya kutembea na hata kukimbia, ila ujipe nafasi usiwe karibu na watu wengine, mazoezi yanasaidia kuimarisha afya ya mwili na akili,” alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa wale wanaofanyia kazi nyumbani, Tedros aliwashauri kuacha kukaa eneo moja muda mrefu kwani sio nzuri kiafya na badala yake wanatakiwa kunyanyuka na kupumzika ikiwa ni pamoja na kunyoosha viungo kwa dakika tatu. Hadi sasa kwa Tanzania walioambukizwa ni 147 huku vifo vilivyoripotiwa ni vitano na 127 wakiwa wamepata nafuu.
 
Hao WHO nao ni kama upepo wa kisulisuli baada ya kuona mwenyezi Mungu anatulinda sana na gonjwa la kibeberu wamekuja kwa style nyingine kwamba tumepona kwa ajili ya lishe

Sent using IPhone X
 
ENYI WALEVI,
ENYI WACHOMA FEGI, BANGI, GOZO NK...
SI MUACHE????? AU MMEROGWA?? SHETANI ATAWACHEZEA MPAKA MWAKA GANI? HATA COVID HAMUMUOGOPI SIO? SUBIRI SASA MUONE INAVYOKUWAGA.
 
Back
Top Bottom