GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,542
- 127,828
- Thread starter
- #101
Ninachofurahi tu ni kwamba mtazamo wangu huu umeenda sambamba na walichokichambua watu wenye akili zao akina Mama Kijobi Simba, Mzee Wasira, Mzee Sumaye na Wanataaluma mbalimbali wa masuala ya Uongozi na Siasa nchini Tanzania. Pia UZI huu umenifanya niweze kujua uwezo wa kuchambua issues kwa Watanzania na kugundua kuwa kumbe bado tuna safari ndefu ya kujikomboa KIFIKRA. Watu wanataka kwakuwa wewe ni Mwana CCM basi kila jambo alifanyalo Rais wewe uliunge tu mkono. Nashukuru Mwenyezi Mungu kuwa mimi ni CCM Makini na siyo CCM JUHA na nasimamia kile ninachokiamini. Mnaosema nimekurupuka au nimwache Rais afanye kazi mbona hamsemi kauli aliyoisema Rais mwenyewe jana kuwa hata katika Ofisi yake IKULU kuwa Wafanyakazi hewa? Je ameshawatangaza? Mbona hajitumbui na kawahi kumtumbua Mama wa Watu tena aliyedumu Madarakani kwa siku 22 tu huku yeye sasa akiwa hapo IKULU kwa miezi 4 kama siyo 5 ambapo wanasema ana uhakika kuwa kuna Wafanyakazi hewa? Ngoja niendelee kuzidi kuzisoma AKILI za Watanzania kupitia huu UZI.