Rais Magufuli chukua tahadhari hii haraka!

Rais Magufuli chukua tahadhari hii haraka!

Hiii ni kengele kwa viongozi wengine waliopewa DHAMANA ya uongozi wanapaswa wawe makini sana! Tusikubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Ukimuona mwenzio ananyolewa...............:::.........

Pia ni vyema ukajipima mwenyewe kama kasi hii ya JPM ina kutisha bora ustape down maana ina onekana unaweza ukaangukia pua!
 
mkuu kubali tu kwa leo hiki ulichoandika umetokota,
unaandika eti unamshauri raisi afanye uchunguzi kujiridhisha, upi zaidi ya huo uliogundua watumishi hewa 45?
ikiwa yeye alisema hakuna hata mmoja.

naheshimu mtazamo wako lakini kubali tu kwa leo umeandika "PUMBA"
 
Gentamycine we ni nyoko.......angalizo nyoko yangu ni ya sifaa.....mkuu hivi kumbe unauwezo mkubwa hivi Wa kufikiri.........
Kwa nini usitumie tu ID yako ya Gentamycine unajisifia mwenyewe..., JF KAZI KWERI KWERI[emoji16]
 
Hiii ni kengele kwa viongozi wengine waliopewa DHAMANA ya uongozi wanapaswa wawe makini sana! Tusikubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Ukimuona mwenzio ananyolewa...............:::.........

Pia ni vyema ukajipima mwenyewe kama kasi hii ya JPM ina kutisha bora ustape down maana ina onekana unaweza ukaangukia pua!


Mistari kuntu. Kabisa mkuu, this strategically serves as a weak-up call kwa RCs wote.

Huko kwenye halmashauri kumeoza hatareee, so lazima watendaji wanastruggle kufunika fyongo zao to the extent possible. As such, yale mazoea ya Senior Officials kushinda tu ofisini kwenye 'kipupwe' kungonjea uletewe Reports na uchungulie kwenye 'executive summary' tu, wengi sana wataingizwa chaka la miashoki.
 
Wakati hivi sasa kila mtu akitafakari hatua ya kishujaa uliyoichukua leo kwa huyo Mama RC na hiyo Njemba RAS na ambayo kwa duru za kidadisi na kiuchambuzi zinasema kwamba hiki ulichokifanya wewe umeweka rekodi yako ya kutukuka kwani hakijawahi kufanywa hata na Mchonga ambaye wengi wetu tunamsifu, kumkumbuka na kumlilia kila siku.

Ila Mheshimiwa Rais kuna kitu nimekigundua na naomba nikiwasilishe kwako na sikulazimishi ukifanyie kazi ila kama utaona inafaa kifanyie kazi tena haraka na upesi sana.

Mheshimiwa Rais kwa jinsi ulivyowaonya hawa Wakuu wako wa Mikoa siku ile unawaapisha huku wengine pale pale ukumbini nyuso zao zilianza kuonekana zimejaa hofu na uwoga inawezekana huyu Mama Anne Kilango Malecela akawa ni mkweli kuwa Mkoani kwake hakuna ghost workers ila huko kwa wengine kwasababu ya uwoga na kutotaka kupoteza vyeo ambavyo wamevipata kwa zali la mentali wanaweza wakawa wamekupa taarifa na figure za uwongo ili tu uwaone wametekeleza kile ulichowatuma.

Nadhani mheshimiwa Rais wangu usingeharakisha kwanza kumuondoa huyu Mama labda mpaka utume watu wako unaowaamini ili na wao wakakuchunguzie vizuri. Inawezekana leo tukakusifu kuwa umechukua hatua stahiki ila huko mbeleni ukweli ukaja kujulikana kuwa ni kweli Mkoa wa Shinyanga ulikuwa hauna hao wafanyakazi hewa halafu huyu Mama ndiyo akaja kuwa Shujaa hadi mwisho wa dunia.

Kwa uzoefu nilionao na kwa jinsi sisi Watanzania tunavyojuana kwa umagumashi na usanii nina uhakika kuna baadhi hata ya hao Wakuu wako wa Mikoa hizo figure walizokupa wamezipika kimkakati tu ili wakuchote akili utiririke nao pamoja na usije ukawatumbua. Binafsi kuna Wakuu wa Mikoa kama watatu hivi ambao kabla hata hujawateua ni WATAALAM wa usanii na ujanja ujanja na hata niliposikia baadhi yao wakitaja figures zao ilibidi tu nicheke na hata wao nikiwapigia simu au tukikutana wanakuambia " kanyaga twende tunacheza mziki ambao DJ ameuchagua na kaupenda ".

Binafsi nadhani mara baada tu ya kuwateua vile basi ungewapa hata miezi mitatu au sita waweke mambo sawa na kwa taratibu ili wakija kukupa TAARIFA basi ziwe ni sahihi kwelikweli huku na wewe unawapa majukumu Watendaji wako hasa RSO's tena kisirisiri wakufanyie hii kazi na nina uhakika mwishowe ungeyajua mengi kuliko hata haya kwani wewe umeona tu huo uozo wa WAFANYAKAZI HEWA ila Mheshimiwa Rais hakuna sehemu ambapo WATENDAJI wako wanapiga HELA za kufa mtu kama huko katika HALMASHAURI na sasa baada ya kuona umekuja na moto mkali na wao wamebadili mbinu ya kuiba je unaijua Mheshimiwa Rais wangu? Siku ukiitaka niambie nikuwekee humu ili sijui ucheke au ulie!

Kataa kubali Mheshimiwa Rais hizo TAKWIMU ulizopewa na hao WAKUU WAKO WATEULE WA MIKOA zichunguze vizuri na kwa umakini kwani 85% zake UMEDANGANYWA kwa kile hawa Marafiki zangu Wakuu wa Mikoa watatu walichokibatiza " kanyaga twende tunacheza mziki ambao DJ ameuchagua na kaupenda ".

Yangu ni hayo tu Mheshimiwa Rais wangu na nakupongeza kwa jitahada zako na nakutakia kila la kheri. Tuna imani kubwa na wewe na tunajua utatufikisha mahala fulani ambako mwenzako hakutaka kutufikisha. Mwenyezi Mungu akupiganie, akulinde na akupe afya bora Wewe, Mama Samia, Waziri Mkuu na Mawaziri wote na Watendaji wengine ili muitumikie vyema hii nchi ambayo kiukweli maendeleo yake yatatokana na jitihada zenu.

Akhsante Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania.
Mkuu wewe si CHADEMA?
Lowassa anauhitaji zaidi ushauri wako?
 
Wewe jamaa siku hizi ni genius! Asubiri usanii wa kibongo sasa,watakuwa wanamwambia tu kile kitu wanajua anataka kusikia,mwisho wa siku atadumbukia kwenye shimo la giza.watu sio wazuri hata kidogo!
 
Huna maneno mengine zaidi ya hayo uliyoyakariri na ambayo unakuja nayo katika kila UZI ninaouanzisha? au nikufundishe maneno mengine ili uyatumie kwani haya yameshakuwa too monotonous si tu kwangu bali najua hata kwa members. Unaweza ukadhani unasifiwa kumbe wenye akili zao na wanaojua au kutambua mchango wangu humu JF wameshakudharau na kukupuuzia muda mrefu. Mwisho kabisa nafurahi sana kwa jinsi unavyokuwa unanifuatilia kila mara katika either posts zangu or threads zangu humu JF kwani hii inaonyesha ni jinsi gani uwepo wangu humu UNAKUKUNA kwani nimegundua unanichokonoa makusudi ukidhani labda nitahamaki nianze kujibizana nawe au kutukanana ila bahati mbaya au sijui nzuri GENTAMYCINE yule uliyemzoea wewe siyo huyu wa sasa na utafanya kila aina ya PROVOCATIONS zako kwangu na nitabaki KUKUPUUZA tu. Hata hivyo nashukuru kwa kuchangia kwani angalau katika posts zilizokwishatumwa sasa katika UZI huu wangu tayari nina post moja wapo ya JUHA wewe.
Afadhali umemwambia Ukweli.

Huyu binti sijui ni kwanini yuko tofauti na mabinti wenzie humu.
Hana adabu kabisa.
 
Hivi uchunguzi gani mwingine ulikuwa unahitajika zaidi ya huo uliowaweka hao ghost workers hadharani !!!!!!!!....

Ule muda wa kuunda tume hata katika masuala madogo umekwisha...
Ingawa mama huyu ninamuhusudu sana hasa michango yake bungeni iliyokuwa inaegemea katika matatizo ya wananchi wake zaidi ya kukisifu chama lakini kwa hili alikuwa wrong sana
 
Ushauri wa kijinga kabisa huu haufai hata kusikilizwa, inaonekana wewe ni miongoni mwa watu waliokuzwa na mfumo wa Kikwete wa kubebana.
 
pumba tu who are you kumpa Raisi ushauri wako wa kijiweni huna hata Elimu ya juu.

swissme
Duh inamaana kuandika maoni lazima uwe Na shahada 7.Sasa weye unazo ngapi za kumjibu Mtoa Uzi?
Chakushangaza umemkubali JPM Na
Umemsaliti the don.
Yuda weyeee
 
Umeshaambiwa katuma watu wake na kagundua wafanyakazi hewa 45, na bado wilaya mbili!

Ingawa namkubali Anna Malecela, ila namkubali JPM kwa alichokifanya ili iwe fundisho kwa wanasiasa "Watawajibika kwa maeneno na vitendo vyao"
Kwa kweli Gentamycin sijui amekurupukaje leo kumshauri raisi bila hata kusoma kuwa raisi nae alishtuka aliposikia mkoa mzima hauna mtumishi hewa. Mwenyewe raisi tena akiwa bado likizo na bila kumjulisha mkuu wa mkoa aliteua kamati kufuatilia ukweli huo na kama tulivyomsikia wote hadi jana usiku walishagunduliwa watumishi hewa 45 na tayari walishalitia taifa hasara ya shs.ml.339 kwani tayari walishalipwa.Hata hivyo bado uchunguzi wa wilaya mbili katika mkoa huo kuhusu watumishi hewa unaendelea. Nakubaliana na Gentamycin kuwa zoezi hili kwa wakuu wa mikoa na wilaya lilipokelewa kwa hofu kubwa ya kutumbuliwa. Pia muda uliotolewa kwao ulikuwa mfupi ukielewa karibu wote na maras wao walikuwa wageni kwenye mikoa hiyo.Hivyo na wao kwa hofu ile ile na vitisho vile vile wakawaagiza watendaji wa chini yao na kuwapa muda mfupi zaidi ili waweze kufanya majumuisho kuwahi deadline ya raisi.Hapa ndipo makosa yalipo na nasema kabla ya kuwafuta hata hao hewa waliogundulika zoezi la verification kwa mikoa yote lifanyike sio Shy tu wameboronga ni mikoa mingi.Kumfuta kazi kimakosa mtumishi kumrejesha tena kwenye payroll na kumb kumb zake pana adha ya kutosha umakini unatakiwa.Kwa huyu mkuu wa mkoa raisi hakuwa na njia nyingine kwani alishasababisha hasara kwa serikali.
 
Huna maneno mengine zaidi ya hayo uliyoyakariri na ambayo unakuja nayo katika kila UZI ninaouanzisha? au nikufundishe maneno mengine ili uyatumie kwani haya yameshakuwa too monotonous si tu kwangu bali najua hata kwa members. Unaweza ukadhani unasifiwa kumbe wenye akili zao na wanaojua au kutambua mchango wangu humu JF wameshakudharau na kukupuuzia muda mrefu. Mwisho kabisa nafurahi sana kwa jinsi unavyokuwa unanifuatilia kila mara katika either posts zangu or threads zangu humu JF kwani hii inaonyesha ni jinsi gani uwepo wangu humu UNAKUKUNA kwani nimegundua unanichokonoa makusudi ukidhani labda nitahamaki nianze kujibizana nawe au kutukanana ila bahati mbaya au sijui nzuri GENTAMYCINE yule uliyemzoea wewe siyo huyu wa sasa na utafanya kila aina ya PROVOCATIONS zako kwangu na nitabaki KUKUPUUZA tu.baelezee. anadhani rais hawezi kushauriwa na raia? kwani huo urais kashuka nao toka mbinguni? ni kura za raia.
 
pumba tu who are you kumpa Raisi ushauri wako wa kijiweni huna hata Elimu ya juu.

swissme
Sio elimu ya juu, hilo jamaa ni pompoma flani hivi halafu lilifeli secondary tu. Na lilivyokua jehu utaliona litakavyo tokwa na mapovu kama limeramba OMO. Sheitwani urajimi hahahahahah[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Umeandika Taka taka tupu na hakuna wakuchukua...! Ikulu imefanya uchunguzi full stop.

Hebu niondolee hiki KINYAA chako kilichoanzia katika UBONGO wako. IKULU utaijua wewe? Hao watu wa IKULU walikuambia wamefanya huo uchunguzi? Swine.
 
Acha kujikomba gentamycine. Wewe ongea kama dume acha sifa za kike. Watu wamemkosoa pamoja na kuwa unaita ushujaa. Umeniudhi wakati gentamycine ni jina kubwa humu

Siyo lazima siku zote nikukune na jaribu kuheshimu mawazo au mtazamo wa Mtu. Unataka nikukune au nikufurahishe wewe " PUNYENYE " ukiwa kama nani kwangu?
 
Sasa ww unafikiri amemtumbua bila kujiridhisha.. Usalama wa Taifa wapo kazini tatizo hamjui

Usalama wa Taifa ndiyo akina nani Mkuu? Huwa nawasikia sana humu wakityajwa tajwa je hawa ni nani hapa Tanzania?
 
Kwa nini usitumie tu ID yako ya Gentamycine unajisifia mwenyewe..., JF KAZI KWERI KWERI[emoji16]

Sina ID humu JF zaidi ya hii ya GENTAMYCINE hata hivyo kama una uhakika na hizo ID's zangu zingine nakuruhusu uzitaje hapa ili moderators wazifute. Sipendi na nimechoka sasa na uzushi wenu kuhusu ID za humu. Mara mnifananishe na Wanasiasa fulani mara tena mnifananishe na ID zingine humu. I am fed up please!
 
Back
Top Bottom