GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Wakati hivi sasa kila mtu akitafakari hatua ya kishujaa uliyoichukua leo kwa huyo Mama RC na hiyo Njemba RAS na ambayo kwa duru za kidadisi na kiuchambuzi zinasema kwamba hiki ulichokifanya wewe umeweka rekodi yako ya kutukuka kwani hakijawahi kufanywa hata na Mchonga ambaye wengi wetu tunamsifu, kumkumbuka na kumlilia kila siku.
Ila Mheshimiwa Rais kuna kitu nimekigundua na naomba nikiwasilishe kwako na sikulazimishi ukifanyie kazi ila kama utaona inafaa kifanyie kazi tena haraka na upesi sana.
Mheshimiwa Rais kwa jinsi ulivyowaonya hawa Wakuu wako wa Mikoa siku ile unawaapisha huku wengine pale pale ukumbini nyuso zao zilianza kuonekana zimejaa hofu na uwoga inawezekana huyu Mama Anne Kilango Malecela akawa ni mkweli kuwa Mkoani kwake hakuna ghost workers ila huko kwa wengine kwasababu ya uwoga na kutotaka kupoteza vyeo ambavyo wamevipata kwa zali la mentali wanaweza wakawa wamekupa taarifa na figure za uwongo ili tu uwaone wametekeleza kile ulichowatuma.
Nadhani mheshimiwa Rais wangu usingeharakisha kwanza kumuondoa huyu Mama labda mpaka utume watu wako unaowaamini ili na wao wakakuchunguzie vizuri. Inawezekana leo tukakusifu kuwa umechukua hatua stahiki ila huko mbeleni ukweli ukaja kujulikana kuwa ni kweli Mkoa wa Shinyanga ulikuwa hauna hao wafanyakazi hewa halafu huyu Mama ndiyo akaja kuwa Shujaa hadi mwisho wa dunia.
Kwa uzoefu nilionao na kwa jinsi sisi Watanzania tunavyojuana kwa umagumashi na usanii nina uhakika kuna baadhi hata ya hao Wakuu wako wa Mikoa hizo figure walizokupa wamezipika kimkakati tu ili wakuchote akili utiririke nao pamoja na usije ukawatumbua. Binafsi kuna Wakuu wa Mikoa kama watatu hivi ambao kabla hata hujawateua ni WATAALAM wa usanii na ujanja ujanja na hata niliposikia baadhi yao wakitaja figures zao ilibidi tu nicheke na hata wao nikiwapigia simu au tukikutana wanakuambia " kanyaga twende tunacheza mziki ambao DJ ameuchagua na kaupenda ".
Binafsi nadhani mara baada tu ya kuwateua vile basi ungewapa hata miezi mitatu au sita waweke mambo sawa na kwa taratibu ili wakija kukupa TAARIFA basi ziwe ni sahihi kwelikweli huku na wewe unawapa majukumu Watendaji wako hasa RSO's tena kisirisiri wakufanyie hii kazi na nina uhakika mwishowe ungeyajua mengi kuliko hata haya kwani wewe umeona tu huo uozo wa WAFANYAKAZI HEWA ila Mheshimiwa Rais hakuna sehemu ambapo WATENDAJI wako wanapiga HELA za kufa mtu kama huko katika HALMASHAURI na sasa baada ya kuona umekuja na moto mkali na wao wamebadili mbinu ya kuiba je unaijua Mheshimiwa Rais wangu? Siku ukiitaka niambie nikuwekee humu ili sijui ucheke au ulie!
Kataa kubali Mheshimiwa Rais hizo TAKWIMU ulizopewa na hao WAKUU WAKO WATEULE WA MIKOA zichunguze vizuri na kwa umakini kwani 85% zake UMEDANGANYWA kwa kile hawa Marafiki zangu Wakuu wa Mikoa watatu walichokibatiza " kanyaga twende tunacheza mziki ambao DJ ameuchagua na kaupenda ".
Yangu ni hayo tu Mheshimiwa Rais wangu na nakupongeza kwa jitahada zako na nakutakia kila la kheri. Tuna imani kubwa na wewe na tunajua utatufikisha mahala fulani ambako mwenzako hakutaka kutufikisha. Mwenyezi Mungu akupiganie, akulinde na akupe afya bora Wewe, Mama Samia, Waziri Mkuu na Mawaziri wote na Watendaji wengine ili muitumikie vyema hii nchi ambayo kiukweli maendeleo yake yatatokana na jitihada zenu.
Akhsante Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania.