Rais Magufuli azindua kiwanda cha Saruji cha Dangote, ataka Dangote apewe eneo la kuchimba Makaa

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,813

Rais Dr J.P.Magufuli ananguruma kutoka kanda ya kusini mjini Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea kiwanda cha saruji cha Dongote akizindua magari ya kisasa ya kiwanda hicho ya kusafirisha mizigo.

Rais ameagiza kiwanda hicho kipatiwe umeme wa uhakika ili kiweze kuajiri watanzania wengi,kulipa kodi na kuchangia katika pato la Taifa. Anaendelea.

======

UPDATE;

======

=> RAIS John Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini impe mfanyabiashara Aliko Dangote eneo la kuchimba makaa ya mawe na agizo hilo liwe limetekelezwa ndani ya siku saba kuanzia leo.

=> Ameiagiza kuwa, makaa ya mawe yakiisha kwenye eneo atakapopewa Dangote, apewe eneo lingine. Ametoa maagizo hayo leo mkoani Mtwara kabla ya kuzindua magari 580 ya Dangote yatakayokuwa yakibeba saruji kutoka kiwandani.

=> “Nia yangu nataka kiwanda hiki kifanye kweli ili ikiwezekana ujenge viwanda vingine…ujenge hata kumi” amesema Rais Magufuli.

=> Amemruhusu Dangote auze makaa hayo kwa watu wengine ili Serikali ipate fedha.

=>Ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kukusanya mapato ya uchimbaji wa makaa hayo kwa Dangote mwenyewe.

=> Rais amemhakikishia Dangote kuwa, ndani ya siku saba atakuwa amepata kibali cha kuchimba makaa ya mawe kwa ajili ya kiwanda cha saruji kilichopo Mtwara.

=> Ameiagiza menejimenti ya kiwanda cha Dangote iwasiliane na serikali moja kwa moja badala ya kupitia kwa watu wengine.

=> Rais amesema, dunia inakwenda haraka sana hivyo uamuzi kuhusu changamoto zilizopo lazima ufanywe haraka ili Tanzania iendane na kasi hiyo.
 
Mwenye ndevu PEKE yake hapa Tanzania Mh. Rais Dr J.P.Magufuli ananguruma kutoka kanda ya kusini mjini Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea kiwanda cha saruji cha Dongote akizindua magari ya kisasa ya kiwanda hicho ya kusafirisha mizigo. Rais ameagiza kiwanda hicho kipatiwe umeme wa uhakika ili kiweze kuajiri watanzania wengi,kulipa kodi na kuchangia katika pato la Taifa. Anaendelea
Is this news! New news?
 
Anasema hataki kuona lobbyst ambao wanataka kupata pesa bila kufanya kazi
 
Anamkaribisha dereva mmojawapo azungumze kwa niaba ya madereva wenzake kueleza kero zao
 
Kweli hivi vituko yeye kujiari hataki alafu anasema dangote ajiri alipe kodi sasa hizo kodi zinaenda wapi maana kila secta njaa tupu au anampa Daudi bashite akale bata marekani
 
Wizara ya nishati na madini wamepewa siku 7 kumpatia Aliko Dangote kipande cha ardhi chenye makaa ya mawe akachimbe mwenyewe, hata akiamua kuwa distributer wa kuchimba na kuwauzia viwanda vingine.
Mmm yan ajichimbie mwenyewe@ i smell somethn fishy@.
 
Kuhusu gesi, una kampuni dalali ya "aqua" ambayo ndiyo mnunuzi wa gas ambayo ndio mnunuzi anayetakiwa kumuuzia tena Dangote, JPM kawapa onyo Kali...
 
Madereva wanatumbua jipu hapa. Kuna mhindi mmoja dalali amejianzishia kampuni ndani ya kampuni anahujumu kampuni na kuna ubabaishaji wa mameneja wa kiwanda
 
Akimaliza ya Dangote tunataka kusikia kuhusu ku forge vyeti je ni halali kwa serikali yake???? Ajibu hapo likae kwenye maandishi
 
Wametajwa majina watu hapa subirini muone jipu likitumbuliwa. Kuna wahindi wanafanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na watz
 
Back
Top Bottom