Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Ni kweli mubashara....Delegation karibu yote imeshawasili hapa wakiwemo mawaziri,Mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, mameya, wenyeviti wa bodi mbalimbali. rais wa Benki ya dunia ndio mgeni maalum wa tukio hili.
Kinachosubiriwa ni kufika kwa Rais wa Nchi Mh. DR MAGUFULI ili uzinduzi rasmi ufanyike.
========
UPDATES;
Balozi wa china ameingia hapa. Ngoma mbalimbali zinaendelea kutumbuiza kusherehesha shughuli hii muhimu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewasili kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu, Ubungo,(Ubungo interchange).
Rais Magufuli na mgeni wake rais wa benki ya dunia wanakuja Ubungo kwa kutumia Mabasi ya Mwendokasi wakitokea Moroco Jijini Dar es Salaam
Rais Magufuli ameshaingia hapa ukumbini baada ya kuwa amekuja kwa kutumia mwendo kasi. Pia amefuatana na mama Janeth Magufuli.
Mradi huu ni kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na benki ya dunia
RC Makonda: Barabara ya kuingia Kituo cha daladala cha Mawasiliano imeshatengewa bajeti na karibuni itaanza kujengwa
TANROADS: Muda wa magari kupita ktk mataa ya Ubungo utapungua kutoka takribani saa 1 hadi dakika 3 barabara hii itakapokamilika. Hivi punde Rais Magufuli ataingia hapa akifuatana na rais wa benki ya dunia Jim Liyong Kim.
TANROADS: Ujenzi wa Barabara hii utagharimu takribani Shilingi Bilioni 177 na utachukua miezi 30 kukamilika. Fidia zimeshalipwa...!
Waziri Mbarawa: Mradi wa DART umepunguza msongamano Barabara ya Morogoro lakini bado kwenye makutano ya Ubungo kuna tatizo...
Waziri Mbarawa: Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS tutasimamia viwango vya barabara vizingatiwe na ujenzi kuchukua muda mfupi
1148hrs: Sasa amekaribishwa Rais Magufuli na anatambua uwepo wa viongozi na wananchi waliohudhuria kwenye tukio la Ubungo.
Magufuli: Nampongeza sana Jim kuwa rafiki wa watanzania na duniani kote wanamtegemea yeye, kwa mtu mkubwa namna hii kuamua kuja Tanzania kwa mara ya kwanza ni kitendo cha kumpongeza, asante sana mheshimiwa Dokta.
Moja ya kero kubwa Dar ni swala la msongamano wa magari bararabarani, wakati wa kampeni tuliendeleza jitihada, nafurahi utekelezaji wa ahadi yangu na chama changu unaendelea vizuri, tulijenga barabara ya Morocco- Mwenge kwa kutumia fedha za sherehe za uhuru na imepunguza msongamano.
Pia tuliweka jiwe la msingi ujenzi wa flyover ya Ubungo, tumezindua daraja la Kigamboni na barabara za mwendo kasi, sasa hivi watu wanatumia wastani wa dakika 45 kutoka kivukoni hadi Kimara badala ya masaa mawili hadi matatu.
Suala la kuhamia Dodoma pia litapunguza msongamano katika jiji la Dar Es Salaam, tumeanza kujenga kituo cha ICD Ruvu na ikifika bandarini inapelekwa moja kwa moja.
Matengenezo ya reli yapo kutoka bandarini kuelekea Ruvu kwa sababu malori makubwa hayataruhusiwa, tupo katika mchakato wa kujenga ya njia sita kutoka Ubungo hadi Chalinze.
Hapa Ubungo ndio langu kuu la barabara kwa nchi yetu, hata magari ya mwendokasi huwa yanakwama, nafurahi hapa leo tunasaidi mkataba wa mkopo na namshukuru Rais wa benki ya dunia na mradi utakuwa na ghorofa tatu, matedereva ambao hawajui kuendesha kule juu itabidi wasipewe haya magari, haya ndio maendeleo.
Interchange ikikamilika itatoa sura ya pekee kwa Dar es Salaam, haya ni maendeleo ya pekee, kwa niaba yenu namshukuru sana Rais wa benki ya dunia na wafanyazi wote wa benki ya dunia.
Huu si mradi wa kwanza kufadhiliwa na benki ya dunia, wamefadhili miradi mingi. Mradi wa ujenzi wa miundombinu katika jiji la Dar na utahusisha ujenzi wa Flyover ya hapa Ubungo, na mwendokasi awamu ya nne na tano, mkataba wa pili ni mkataba wa maji. Mikopo tuliyopata leo kutekeleza miradi ni dola milioni 780 za kimarekani sawa na trilioni 1.74.
Ametoka kote huko kuja Dar es Salaam ya Makonda, huwezi kumkopesha mtu asiyekopesheka.
Tumepata mkopo kutoka South Korea kujenga daraja la juu kutoka Coco Beach mpaka Agha Khan Hospital, sambama na barabara kuna mpango wa kuboresha miundombinu ya reli na kandarasi yuko kwenye site na itakuwa ni reli ya kimaifa na inaendeshwa na umeme.
Niwaombe wizara ya miundombinu na wakandarasi simamieni mradi ukamilike. Sioni sababu mradi huu ukachukua mpaka miezi 30, wakati kuna usiku na kuna mchana. Hakuna sheria duniani inayokataza kufanya kazi usiku, angalau basi miezi 20.
Mradi huu unajengwa kwa gharama kubwa na ni mkopo, naomba tulipe kodi tuweze kurejesha hizi fedha pia wahusika wasiibe vitu vitakavyotumika hapa.
Rais Magufuli: Tumejielekeza mno katika masuala ya udaku ambayo hayatuongezei chochote, hayatusaidii chochote na ndio yanachukua muda wetu mwingi. Tuzungumze uchumi, tujielekeze katika mambo ya maendeleo na hayana chama na nafurahi kumuona mstahiki meya na ni wa CHADEMA.
Kampeni zilishakwisha, ulie ugalegale Rais ni Magufuli. Ndio maana hii interchange inajengwa kwenye jimbo la CHADEMA, nawaomba watanzania wa vyama vyote tujifocus kwenye suala la maendeleo.
Mnahangaika mnapost kwenye vipost vyenu, mpaka watu wengine wanaingilia uhuru wangu, mimi huwa sipangiwi mambo. Mimi ni Rais ninayejiamini, siwezi kupangiwa, hata siku ya kuchukua fomu nilienda mwenyewe.
Nitaamua mwenyewe nani akae wapi, kwa hio Makonda wewe chapa kazi, nasema chapa kazi. Najua wamenielewa, kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata mimi naandikwa kwenye mitandao, Kwahio nijiuzulu Uraisi?
Mimi ningefurahi hata kwenye mitandao tungekuwa tunapata ushauri jinsi ya kufanya, tunajadili personality na sio ideas, tuchape kazi kwa manufaa ya watanzania.