Rais Magufuli awataka Jeshi la Polisi, Mawaziri na watendaji wa Serikali wasijihusishe na ufyekaji bangi mashambani

Tena ni rahisi sana; wala hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi ikiwemo kunyanyasa wanakijiji wote. Polisi wakimjua mwenye shamba ni kumuamuru kulifyeka tena akiwa chini ya ulinzi na kwa sababu ushahidi uko wazi anapelekwa mahabusu na bila kuchelewa mahakamani!
Yah uko sahihi,lakini sio wanakijiji wote
 
“Kama kuna jambo linaloniudhi ni Polisi kufyeka mashamba ya bangi. IGP waambie askari wako wasifyeke tena bangi. Hamkuajiriwa kufyeka bangi. Mnazo uniform nzuri mkizitumia kwenda kufyeka bangi mnadhalilisha jeshi la polisi. Kama shamba lipo karibu na kijiji shika kijiji kizima, kuanzia wazee, wanawake, watoto, wapeleke wao ndio wakafyeke. Siku nyingine watamtaja anayelima bhangi"
_

Haya sio maneno yangu ni maneno ya
Rais JPM, Arusha, 07/04/2018.
Sunzu Nimecheka sana
Yani siku imeenda murua
 
Nimemskikis mh raisi akiwaambia maaskari kwamba iwapo watakuta sehemu fulani kumelimwa bangi wasifanye kazi ya kuifyeka na badala yake wanakijiji wa sehemu hiyo ndio watahusika na ufyekaji wa shamba hi wakiwemo wazee, wamama na watot, sasa nimejiuiza swali dogo tu a kijiinga, Hivi kwa mfan hiyo bangi iwe imelimwa huko chato kijijini kwao ina maana na mama yake mzazi naye atahusika katika ufyekaji?
Lakini kingine unakuta bangi inalimwa maeneo ya mbali kutoka wanapoishi watu na mfano mdogo maeneo ya milimani huk morogoro hapa raia si wanatakuwa wanaonewa?
Msikilize hapo chini
[
Achakujjfanya wewe kuwa kipofu ... Hivyo kwa.azingira gani mkulima was jinijini analima na wanakijiji wenziwe wasijuwe kuwa Mwenzao analima..au halimi ..! Wote huwa wanajuana..kilichobakia nj uhunitu...hivyo tamko lipo sawa tena.. Sanaaa!
 
Hahahahaha

Unaitwa Ulinzi shirikishi

Inawezekanaje Bhangi ilimwe mpaka istawi asijulikane Mwenye Shamba
Unapokuwa mjinga usidhani na wengine wana IQ za kilumumba...kula mtu anajua bangi ni madawa ya kulevya!..kuna usiri mkubwa sana kwa mlimaji wa bangi ..je iweje liwe kosa la kijiji kizima kama vile walialikana kwenda kulima mahindi?..hatuna rais kwa kweli..Nyerere aliko huko anafurukuta kwa hasira!
 
nguvu ni kijiji kufyeka au Polisi kufyeka? safari hii Arusha wameshikwa pabaya
Kwa akili yako fupi unafikiri Arusha wameshikwa pabaya...!!!

Kwani Arusha ndio wakulima wa bangi nchi hii...???

Hiyo kauli sio nzuri kama wewe ni mtu kufikiria kwa mapana.
 
yule mwanasheria wa Kenya aliyesema Tz tunaongozwa na m/kiti wa baraza la kijiji kumbe hakukosea!
 
Achakujjfanya wewe kuwa kipofu ... Hivyo kwa.azingira gani mkulima was jinijini analima na wanakijiji wenziwe wasijuwe kuwa Mwenzao analima..au halimi ..! Wote huwa wanajuana..kilichobakia nj uhunitu...hivyo tamko lipo sawa tena.. Sanaaa!
kwahiyo tuseme kama askari mmoja alimpiga risasi Akwilina maaskari wote waliokuwepo wote wanahusika au wapewe adhabu?
 
Hio inaitwa udikteta kamili. Kijiji kizima kupewa adhabu ni kinyume cha utawala wa sheria.
vijiji vitakuwa gulags.
Kama Russia, North Korea
Kwenu,

Baada ya kuzindua nyumba mpya za askari polisi mkoani Arusha; Rais Magufuli akihutubia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, alikataza askari polisi kufanya kazi ya kung'oa bangi wakiwa kwenye operesheni ya kupambana na wahusika wa dawa za kulevya.

Kwa uso wenye hasira, Rais Magufuli aliagiza kuwa ikiwa shamba la bangi litapatikana ndani ya kijiji, basi wachukuliwe wazee, wanawake,wanaume na watoto wa kijiji husika na kupelekwa kwenye shamba la bangi ili waing'oe. Askari wasihusike. Collective punishment!
Hii imekaaje?
 
Mnaopinga tengeni siku ya kumshikia mabango, watanzania sijui mfanyiwe nini yani...
 
Tenaa ikiwezekana wenye mashamba jiran wawe mstari wa mbelekufyeka kuna vitu vingine vinawezekana simple tu basi watu walishazoea kauli za tutaunda kamati tulishughulikie hili wapiiiiii huyu ni JIWEEEE NA mamaaa yanaaaanaenda NGENGEEEEEENGEEER MBONA mtatamani munywe sumuu ndo kwaaanzaaa anaongeza gia cinaja wa saivi wanasema HATUPOI MWENDO WA KIKURUTA WALIOPITIA MAFUNZO YA JESHI hadi 2025 mbona adabu itakuwepoo
 
Hii habari ya kutoa adhabu kwa kijiji kizima haina mashiko. Huko vijijini kila siku tunashuhudia ugomvi wa mipaka ya mashamba.

Kama polisi wameona bangi kwenye shamba fulani, je hawawezi kuuliza uongozi wa kijiji/mtaa ili wajue shamba ni la nani? Na huyo mhusika ndo afikishwe mahakamani (siyo kupiga kama inavyotaka kuzoeleka)? Huu utaratibu wa kauli ya mtu mmoja kuwa sheria siyo sahihi

Yaani mm huku kijijini nianze kazi ya kukagua mashamba ya watu ili kuepuka kipigo cha polisi? Ikitokea bahati nzuri nimeona nitatoa taarifa, lakini nisilazimishwe kujua bangi inalimwa shamba la nani. Sisi huku kijijini hatuna utaratibu na siyo desturi kupita katikati ya shamba la mtu(ikumbukwe tunaongelea shamba la ekari zaidi ya 3 kwa maisha ya kijijni, na siyo plot ya kujenga nyumba kama ilivyozoeleka mjini, mtu akiwa na kiwanja robo ekari utasikia nae anasema nilienda shamba). Kwa maisha ya kijijini, mashamba yako mbali na makazi ya watu ( kumbukeni sera ya vijiji vya ujamaa 1974).

Mara nyingi tumekuwa tunaona kwenye TV polisi waking’oa bangi shambani, na inakuwa imelimwa katikati kabisa ya shamba. Si karibu na njia kiasi kwamba mpita njia yeyote anaweza kuona. Si desturi kupita katikati ya shamba la mtu pasipokuwa na njia, mwenye shamba akikukuta utamweleza unatafuta nini ilihali hapo hakuna njia.

Watu waachane na kilimo cha bangi. Wanakijiji tusifanywe kama watoto wa shule, kwamba mwl wa zamu akisikia kelele darasa fulani anakuja na rundo la viboko na kuadhibu darasa zima, kisa eti mbona hamjaleta majina ya wapiga kelele, kwa hiyo darasa zima mnakula mboko. Sisi ni tabaka la chini sawa, lakini angalau tupewa heshima mbele ya watoto wetu. Yaani unipige teke/virungu mbele ya mke, mtoto, mkwe kwa sababu ya bangi ambayo hata huenda nisijue ni shamba la nani. Siku hizi vijiji vimepanuka sana, siyo sawa na ubalozi wa nyumba kumi-kumi.
Tanzania imekuwa familia ya Magu.
 
Demokrasia gani tena wewe upo jamii forums muda huu kuna mtu anakufuatilia hata uandike nini?? Nenda china au korea uone mambo yanavyokwenda.
 
Back
Top Bottom