Rais Magufuli awakoromea sekretarieti EAC

Rais Magufuli awakoromea sekretarieti EAC

Hapa mzee hata akorome maneno yake hayana mashiko kabisa.
Hii ni jumuiya ya kikanda na yeye hata awe mwenyekiti hana mamlaka ya kuamua chochote.
Ni lazima mzee aelewe mipaka yake kabla ya kuongea au kufanya kitu kinachoweza kuwa fedheha kwa nchi.
Hii jumuiya ya EAC haina tija kwa Tanzania, sema hajatokea kiongozi wa kulisema wazi. Nchi wanachama tu zina uhasama miongoni mwao, sasa kuna umoja gani hapo?
 
Suala la matumizi yasiyo na tija kwenye EAC yameandikwa sana zaidi ya mwaka mmoja sasa. Inaelekea kuna ubadhirifu wa fedha za EAC. Wabunge wa EAC waliwahi kulipigia kelele japo ilikuja kuonekana nao huwa na madai ya ajabu ajabu.

Mimi nadhani wakuu wa nchi wameamua kumpa JPM mwaka wa uenyekiti japo Tanzania ilishamaliza muda wake ili alisimamie hilo kama anavyofanya Tanzania.

Hapo hakuna cha ajabu. Hata EU wapo makini na matumizi yao na Uingereza ni kinara wa kupigia kelele matumizi yasiyo na tija kwenye kwenye EU.
 
Hii jumuiya ya EAC haina tija kwa Tanzania, sema hajatokea kiongozi wa kulisema wazi. Nchi wanachama tu zina uhasama miongoni mwao, sasa kuna umoja gani hapo?
Mkuu, kuna tija kuwepo kwenye EAC. Tatizo uongozi wetu uliopita haukuwahi kukaa chini na kujaribu kuumiza kichwa kupata jinsi ya kuinufaisha Tanzania. Ilikuwa business as usual. Nchi nyingine kama Kenya na Rwanda wanafanya hivyo.

Serikari inaweza kuunda jopo la watalaamu kisiri ili kuangalia namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika. Kwenye mkusanyiko ni lazima kufanya hivyo siyo kufuata upepo tu. Kuna vitu vingi vya kufanya kimya kimya. Ujasusi wa kiuchumi unahitajika sana.
 
Inamaana hao wakuu wa nnchi wangelala guest ? Ya shs 15000 per night . Ni lazima wamebook presidential suit ambayo inawekwa kila kitu vinywaji vya aina yote kwa hiyo iyo bei ni sawa kabisa . Mtu anatumia Mara moja kwa mwaka tu jaman .
Au ikulu ndogo inaweza kuwa accommodate?
 
Inamaana hao wakuu wa nnchi wangelala guest ? Ya shs 15000 per night . Ni lazima wamebook presidential suit ambayo inawekwa kila kitu vinywaji vya aina yote kwa hiyo iyo bei ni sawa kabisa . Mtu anatumia Mara moja kwa mwaka tu jaman .
Nakumbuka kuna rais mmoja huko amerika yeye nyumba yake ni ya kawaida sana, na gari yake ni bito la kizamani, hachukui ata mshahara aise!!
 
Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki amewakoromea Sekretariati ya Afrika ya Mashariki kwa ufisadi wanaoufanya ikiwemo kuwagharamia marais walioalikwa kulala hotel za gharama kubwa ambapo rais mmoja kwa usuiku mmoja analipiwa TZS 3,000,000/-. Yeye binafsi (Rais Magufuli) hulala katika nyumba ya serikali isiyogharimu kiasi kikubwa kama hicho.

Pamoja na hayo, ameonya matumizi makubwa yasiyo ya lazima/msingi ili kuokoa fedha nyingi zinazochangwa na nchi washirika wa jumuiya.

Hapa chini nimebahatika kupata namna gharama zilivyo juu na kuigharimu Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.


View attachment 326987 View attachment 326989 View attachment 326991
Sijaelewa. Mbona hizi gharama za kawaida sana. Kama unabisha angalia Dodoma hotel hamna hata cha maana wana charge nyingi tu.
 
Nakumbuka kuna rais mmoja huko amerika yeye nyumba yake ni ya kawaida sana, na gari yake ni bito la kizamani, hachukui ata mshahara aise!!
Ni Rais wa wapi huyo mkuuu amerika ipi huyo Rais ni mfano wa kuigwa
 
Ni Rais wa wapi huyo mkuuu amerika ipi huyo Rais ni mfano wa kuigwa
Huyu hapa mkuu, anaitwa Jose Mojica :::
He has been described as "the world's 'humblest' president" due to his austere lifestyle and his ... 90 percent of his $12,000 monthly salary to charities that benefit poor people and small entrepreneurs.
 

Attachments

  • images-6.jpeg
    images-6.jpeg
    9.2 KB · Views: 20
Kwanza tuachee Ushabiki !!!

Unyekiti wa EAc
Unazunguka kwa kila nchi mwanachama kwa mwaka moja,

Yeye hajachaguliwa kama mashabiki wake wanavyoleta uvyama kwenye utaifa,
Amepokea kijiti kwa niaba yetu

Mwaka huu ni zamu yetu Tanzania
Mwaka kesho tunaachia wengine

Hizo nyingine ni Mbwembwe tuu Na Maigizo yatapita
Kafanye homework yako, naona hapo umetoka povu tu!Uliza hata mtoto utajua ukweli, mie nakuacha njia panda hivyo, yaani hata hujui mwenyekiti alikuwa nani wa EAC na ni vpi Magufuli kapewa kijiti??Khaa
 
Rais wa raia wenye thamani ya zaidi ya milioni tatu anapokoroma kisa amehudumiwa pahala salama na penye hadhi ya milioni tatu napata tabu kuelewa. Ifike sehemu kick zitafutwe kwa ubunifu badala ya kukoroma juu ya kila kila. Mashangingi ya serikali yamejaa mitani yanatumia gharama kubwa mbona hayajauzwa kuokoa gharama na yapo kila siku tofauti na mkutano wa siku 3.
 
Binafsi, kwa level ya Marais, sioni kama ni shida sana kutumia hizo 3M/-! By the way, kadri ya nijuavyo, sehem yoyote alipo Rais au anapofanya ziara, gharama zake ni kubwa kuliko hizo 3m/-! Tusijiminye sana tusije onekana ni kituko! Viongizi wakuu wanastahiki sehemu VIP kwa hadhi zao
 
Back
Top Bottom